Taifa linafanyiwa ubadhirifu na wahuni wachache halafu mnabaki kumletea lawama Waziri Majaliwa kisa tu ajali ya ndege Bukoba

Taifa linafanyiwa ubadhirifu na wahuni wachache halafu mnabaki kumletea lawama Waziri Majaliwa kisa tu ajali ya ndege Bukoba

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Leo hii mgao wa umeme umekuwa kero kwa taifa letu kiasi cha kuporomosha uchumi wa wananchi lakini mnachukulia poa.

Hiyo kampuni ya Mahindra group iliposaini mkataba wa bil 78 kuiboresha TANESCO mbona haijaboresha?

Bunge linapitisha kuwa serikali ikope tril 10. Halafu zinakopwa tril 15 bila idhini ya bunge. Hamuoni kuwa wahuni wanatuumiza?

Tokea tumepata uhuru. Taifa letu kwa ujumla hatukuwahi kupata raisa aliyekuwa tayari kuweka kipaumbele katika kupambana na majanga. Hata magari ya zimamoto mpaka sasa hivi hayapo baadhi ya wilaya. Ndio mumbebeshe mzigo Kassim?

Tunajua ni mkakati wa 2025 wa wahuni wapigaji wa CcM
 
Kunatakiwa mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri.
 
Sure lakin na kule juu mtihani maana now ng'ombe wa mbele ndo anachelewesha msafara anapigwa bakora ng'ombe wa nyuma
Mimi tatizo ninaloliona tatizo ni Ng'ombe wa nyuma anatamani kiti cha Ng'ombe wa mbele too early.
 
Mimi tatizo ninaloliona tatizo ni Ng'ombe wa nyuma anatamani kiti cha Ng'ombe wa mbele too early.
Viongozi wangewekwa kama makocha uzembe ungepita mbali. Machawa wasingekuwa na nafasi
 
Back
Top Bottom