Ni masikitiko makubwa kwa Watanzania wapenda mpira wote,kama mnavyojua jana timu yetu ya taifa imeangushiwa kipigo cha magoli 7 bila majibu.
Kimtazamo ni kweli Algeria wametuzidi sana kiwango katika mchezo wa mpira wa miguu,Wana wachezaji wazuri wanaocheza ligi kubwa Ulaya na kwingineko.Wachezadi kama Riyad Mahrez,Brahine na Islam aliyetufunga goli mbili mechi ya nyumbani ni wachezaji wenye kiwango sana ukilinganisha na wa kwetu.
Lakini na sisi tuna wachezaji wazuri kama Mbwana Aly Samatta,Thomas Ulimwengu ,Elius Maguri ila ni wachache sana.
JE NI KWA NINI SABA BILA?
Kwanza kabisa UBORA wa Algeria kama nilivyokwisha kueleza hapo juu
Pili ni MCHEZO WA KWANZA nyumbani uwanja wa Taifa tulidominate mchezo ule na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga japo tulizipoteza,hii yote ilitufanya Tuwachukulie poa Algeria na kuona kua wanafungika kirahisi.
Tatu ni SAIKOLOJIA ya wachezaji na Waalimu wa timu yetu,Hili naomba kufafanua kidogo wachezaji wetu wengi hawana exposure tuna Mbwana Samatta na Ulimwengu tu ambao wamepata nafasi ya kucheza dhidi ya timu mbalimbali zikiwemo za waarabu hawa mfano USM,Suala la saikolojia hapa linakuja kwamba wachezaji hawa wanakua hawana hofu sana na hawa watu tofauti na wachezaji wetu wa ndani wakifika kule kuanzia mapokezi hadi uwanjani wataona mazingira ambayo ni tofauti sana na yanaweza kuwajengea hofu.
Ndani ya uwanja timu kama Algeria wakiwa nyumbani jana waliamua kushambulia kuanzia sekunde ya kwanza kwa kasi ya ajabu,Sikuona haja ya wachezaji wetu nao kujibu kasi ile,kimchezo mwenzako anapojaribu kucheza mpira aliopanga kucheza wewe inatakiwa umbadilishe kwa mbinu.Stars walitakiwa kupooza mpira ule sio na wao kwa kushambulia au kucheza kwa kasi.Hapa ndipo linapoingia swala la SAIKOLOJIA ya mwalimu na uwezo wake,nadhani anafahamu yote haya vizuri.
JE TUMEDHALILIKA?
Nilijaribu kujifanya sijali sana mchezo ule lakini utanzania ukaniumbua nikajikuta nimesogea hadi sehemu za kuangalia mpira mbele ya projector kubwa kabisa nikaketi nikisema lolote na liwe "by the way" tutafungwa nyingi tu
Lakini ukweli ni kwamba niliumia sana hasa kuona tumefungwa WIKI.Ndio tumedhalilika lakini sio kwamba hatuna wachezaji wazuri swala kubwa ni kama nilivyokwisha kueleza hapo juu EXPOSURE.Wachezaji kama Mudathir Yahaya,Himid Mao wanahitaji kucheza nje ya Tanzania ili kukua MENTALY katika mpira.
NINI KIFANYIKE?
Mipango ya muda mrefu kama kuwekeza kwenye soka la vijana,wachezaji kujituma zaidi na kutoridhika na klabu zetu kubwa za ndani namaanisha watafute opportunities za kucheza soka la nje hata kama ni ligi za daraja la pili.
Ligi iboreshwa zaidi panapowezekana n.k.Lakini yote haya yamekwishasemwa sana.Binafsi nina imani na mipango ya under 17 inayoandaliwa kwaajili ya 2017.(nitakuja kulielezea hili zaidi).
TUTAZUGA TU KWAMBA HATUJALI MATOKEO YA TAIFA STARS LAKINI WENGI WETU TUNAUMIA NDANI KWA NDANI.