Taifa Star kufungwa, tatizo ni uwezo mdogo wa kocha?

Taifa Star kufungwa, tatizo ni uwezo mdogo wa kocha?

Timu za Taifa za Tanzania na Kenya zimetolewa kwenye hatua ya kufuzu kombe la dunia nchini Urusi-2018 kwa kufungwa ugenini kwenye mechi za marudiano. Taifa Stars ya Tanzania iliingia uwanjani jana dhidi ya Algeria wakiwa na akiba ya sare ya 2-2 kwenye mechi ya awali.

Taifa Stars ilizabwa mabao 7-0 katika mechi ya jana na kutupwa nje kwa jumla ya mabao 9-2. Kati ya sababu zilizowapoteza Taifa Stars ni kuimarika kwa kikosi cha Algeria,kwa kuwepo kwa Yacine Brahimi wa Porto ya Ureno,pamoja na kucheza pungufu baada ya Mudathir Yahya kulimwa kadi nyekundu. Pungufu kwa Algeria!? Algeria pia walipewa penati mbili nyepesi sana-za kupendelewa.

Kwa upande wa jirani zetu Harambee Stars ya Kenya,waliingia uwanjani kurudiana na Cape Verde wakiwa wameshinda bao 1-0 nyumbani. Jana walitandikwa mabao 2-0 na kusukumwa nje kwa jumla ya mabao 2-1. Harambee Stars imeponzwa na kucheza kwa kujihami na kutokuwa na msaidizi wa kueleweka wa Victor Wanyama kwenye kiungo. Cape Verde walicheza kwa nguvu kubwa.

Hayo yameisha, tugange yajayo

Hao Yanga na Azam bure kabisa!just a joke mkuu,nakumbuka enzi zile za Maximo tukibishana kuwa Yanga (Stars)imeifunga Burkina Faso!
 
wapigwe tu maana hakuna namna mtu unaambiwa usifanye hiki unafanya utapigwa tu

Tatizo liko kwenye uongozi wa TFF; tuliwaonya kuwa huyo Malinzi hajui mambo ya mpira anataka kwenda kufanya biashara ya kukusanya $$$$ hamkutusikiliza !!! Sasa mnaona tangu Tenga ameondoka timu ya Taifa na mpira kwa jumla imedorola!!! As long as bojo Malinzi yupo hapo timu ya Taifa itapata kipondo tu.
 
attachment.php
 

Attachments

  • Screenshot from 2015-11-18 10:06:09.png
    Screenshot from 2015-11-18 10:06:09.png
    61 KB · Views: 227
7-0 tumegeuka Djibout! Kweli mtu ukizeeka sana unarudia utoto!:what:
 
In 1956 Tanzania 0-9 Kenya.....leo Algeria 7- 0 Tanzania...baada ya miaka 50 tena tunapunguza idadi ya magoli....hivo kufikia level ya kuwin foreign games abroad itakuwa after 200 years to come...that's development🙉🙉🙉🙉🙉
 
Ni masikitiko makubwa kwa Watanzania wapenda mpira wote,kama mnavyojua jana timu yetu ya taifa imeangushiwa kipigo cha magoli 7 bila majibu.
Kimtazamo ni kweli Algeria wametuzidi sana kiwango katika mchezo wa mpira wa miguu,Wana wachezaji wazuri wanaocheza ligi kubwa Ulaya na kwingineko.Wachezadi kama Riyad Mahrez,Brahine na Islam aliyetufunga goli mbili mechi ya nyumbani ni wachezaji wenye kiwango sana ukilinganisha na wa kwetu.
Lakini na sisi tuna wachezaji wazuri kama Mbwana Aly Samatta,Thomas Ulimwengu ,Elius Maguri ila ni wachache sana.

JE NI KWA NINI SABA BILA?
Kwanza kabisa UBORA wa Algeria kama nilivyokwisha kueleza hapo juu

Pili ni MCHEZO WA KWANZA nyumbani uwanja wa Taifa tulidominate mchezo ule na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga japo tulizipoteza,hii yote ilitufanya Tuwachukulie poa Algeria na kuona kua wanafungika kirahisi.

Tatu ni SAIKOLOJIA ya wachezaji na Waalimu wa timu yetu,Hili naomba kufafanua kidogo wachezaji wetu wengi hawana exposure tuna Mbwana Samatta na Ulimwengu tu ambao wamepata nafasi ya kucheza dhidi ya timu mbalimbali zikiwemo za waarabu hawa mfano USM,Suala la saikolojia hapa linakuja kwamba wachezaji hawa wanakua hawana hofu sana na hawa watu tofauti na wachezaji wetu wa ndani wakifika kule kuanzia mapokezi hadi uwanjani wataona mazingira ambayo ni tofauti sana na yanaweza kuwajengea hofu.
Ndani ya uwanja timu kama Algeria wakiwa nyumbani jana waliamua kushambulia kuanzia sekunde ya kwanza kwa kasi ya ajabu,Sikuona haja ya wachezaji wetu nao kujibu kasi ile,kimchezo mwenzako anapojaribu kucheza mpira aliopanga kucheza wewe inatakiwa umbadilishe kwa mbinu.Stars walitakiwa kupooza mpira ule sio na wao kwa kushambulia au kucheza kwa kasi.Hapa ndipo linapoingia swala la SAIKOLOJIA ya mwalimu na uwezo wake,nadhani anafahamu yote haya vizuri.

JE TUMEDHALILIKA?
Nilijaribu kujifanya sijali sana mchezo ule lakini utanzania ukaniumbua nikajikuta nimesogea hadi sehemu za kuangalia mpira mbele ya projector kubwa kabisa nikaketi nikisema lolote na liwe "by the way" tutafungwa nyingi tu
Lakini ukweli ni kwamba niliumia sana hasa kuona tumefungwa WIKI.Ndio tumedhalilika lakini sio kwamba hatuna wachezaji wazuri swala kubwa ni kama nilivyokwisha kueleza hapo juu EXPOSURE.Wachezaji kama Mudathir Yahaya,Himid Mao wanahitaji kucheza nje ya Tanzania ili kukua MENTALY katika mpira.

NINI KIFANYIKE?
Mipango ya muda mrefu kama kuwekeza kwenye soka la vijana,wachezaji kujituma zaidi na kutoridhika na klabu zetu kubwa za ndani namaanisha watafute opportunities za kucheza soka la nje hata kama ni ligi za daraja la pili.
Ligi iboreshwa zaidi panapowezekana n.k.Lakini yote haya yamekwishasemwa sana.Binafsi nina imani na mipango ya under 17 inayoandaliwa kwaajili ya 2017.(nitakuja kulielezea hili zaidi).

TUTAZUGA TU KWAMBA HATUJALI MATOKEO YA TAIFA STARS LAKINI WENGI WETU TUNAUMIA NDANI KWA NDANI.
 
In 1956 Tanzania 0-9 Kenya.....leo Algeria 7- 0 Tanzania...baada ya miaka 50 tena tunapunguza idadi ya magoli....hivo kufikia level ya kuwin foreign games abroad itakuwa after 200 years to come...that's development🙉🙉🙉🙉🙉

Mwaka 1956 Tanzania ilikuwepo katika bara gani?
 
Huwezi fundisha mbwa mzee mbinu mpya. Wachezaji walisha haribikiwa na makocha wakizungu, sasa ndo kwanza mkwasa anaanza kukinoa upya. Tumuache kocha aendelee kupata vijana wapya. Mbwana na mwenzio ni watu wawilitu na hawawezi kucheza wao kama wao. Kwahio tunahitaji akina mbwana angala sita au saba.
 
Tatizo wala CIO kocha ni uwezo wa wachezaji wenyew km nafasi wanapata za kufunga ila uwezo ndy hakuna utalaum makocha bure.
 
Hicho kiingereza sasa!
Maghwangala hivi hujui humu ndani hata sisi wa division 5 nasi tumo.Usipate shida hata sisi tulitamani kusoma shule za watakatifu lakini ndiyo hivo wazazi wetu wameishia kulipa kodi ili ziwasomeshe akina Maghwangala kwenye shule za watakatifu.
 
Nilisoma kwenye gazeti moja jana likidai kuwa wameahidiwa (sijui nani kaahidi) milioni 500 wakiitoa Algeria na ndio nikajua kuwa uswahili bado unaendelea sio kwa wachezaji tu bali viongozi na mashabiki! Kama kweli una nia si unatoa tu hiyo 500m ili waitumie kujiandaa na kuongeza morali!?
Hizi story za kutegea siku mbili kabla ya mchezo alafu watu wanaanza kujitokeza kwenye TV 'kuwataka Watanzania waisapoti timu', mara wachezaji eti 'watafia uwanjani' na ujinga mwingine kama huu ndio unatufikisha hapa.
Kwa walio angalia mchezo wa kwanza watajua kuwa Algeria ni nzuri lakini tulicheza vizuri pia, aibu ya magori saba ni mengi. Suala la fitina halina mashiko sana, ndio maana zikawa mechi mbili (nyumbani na ugenini).
 
Watanzania wengi ni washamba japo wanajifanya muchknow,wengi walegevu japo wanajifanya wakakamavu,wengi wavivu kuanzia akili mpaka mwili.Kila jambo Watanzania nı kulalama tu hata hawajishughulıshı.Watu wanakaa vijiweni wanapga umbea na siasa!Kiufupi Watanzania hakuna eneo hata moja mnaweza ku-excel kwa tabia hz na sio tu mpira!Yani km Magufuli anaweza,aweke baadhi ya sheria pembeni ili hawa watu waswagwe kufanya kazı na waache mambo ya kipumbavu kwa nguvu.

Acha maneno mengi!! Timu imepigwa 7-0, sema nini kifanyike???
 
Mimi siku zote huwa nasema makocha wazalendo wa kitanzania uwezo wao huwa mdogo lakini huwa wanataka kulazimishia mambo makubwa matokeo yake ndo 7-0

Tanzania kama tungekuwa tumepiga hatua kisoka tungeona mchango wa hawa makocha wazalendo lakini kwa hali hii ni sawa kumchukua mwalimu aliyefail mtihani akafundishe wanafunzi halafu mtegemee wanafunzi hao kufaulu.

Sasa Tanzania tunahitaji kocha wa kigeni mwenye rekodi nzuri ya ufundishaji na mwenye kukizi viwango vya kimataifa.

Sijawahi ona duniani kocha wa timu ya wanawake anafundisha kikosi cha timu ya taifa wanaume!
 
Tatizo kubwa hatuwekezi kwenye kuendeleza soka la watoto na vijana.
 
Tulimkata maximo

Kweli kabisa Mkuu.Maximo aligundua sisi ni todlers kwenye soccer tunahitaji kwenda taratibu hadi kufikia mafanikio sisi tukawa tunaforce mafanikio ya haraka...hakuna shortcut kwenye mpira wa miguu
 
Back
Top Bottom