Mkwasa hastahili lawama wachezaji wa stars uwezo wao ni mdogo mno! ?
Nionavyo:
1. Tatizo la Soka letu sio kocha, siyo wachezaji, siyo Simba na Yanga. Ni kutojua mfumo saahihi wa kuendeleza Soka lenyewe kutoka lilipo. Huwa tunadhani tu kwamba labda tunahitaji kocha mgeni, labda exposure, n.k. Lakini kuzuka tu na kutafuta exposure ama kocha bila ya kwanza kuchambua hali ya Soka letu ili kujua njia ya kufuata ni sawa na kumtia maji baridi mgonjwa wa homa anayeunguza, tukidhani ndio tumemtibu.
2. Serikali, TFF, Vilabu na wadau wengine watafute wataalamu wa kuendeleza soka ili waitafiti hali yetu na kutushauri la kufanya. China wameshafanya hivyo na hivi sasa ndio wanaendeleza mikakati iliyotokana na ushauri kama huo. Tusikurupuke tu kuanza na makocha ama akademi.
3. Wakati tunajiandaa na hilo, tusitarajie kupiga hatua ya maana kwenye Soka. Ama tuwache kushiriki michuano ya kimataifa kwanza, au tuwe tunaridhika na matokeo. Sisemi kwamba tusitafute makocha ama wachezaji wazuri. Nasema kabla ya utafiti nilioupendekeza na utekelazi wa maono yake, tusitarajie matokeo mazuri yaliyo endelevu.
4. Tunapotathmini wachezaji na makocha wetu, tuelewe mipaka ya uwezo wao. Mbwana Samata si wa kiwango tunachomkuza, ingawa ndiye fowadi wetu bora kwa sasa. Kwa sifa na mategemeo tuliyomwekea, alipaswa kufunga angalau magoli matatu peke yake kwenye kipindi cha kwanza cha mechi ya awali. Kadhalika Ulimwengu. Mchezaji wa kiwango tunachompakazia Samata lazima awe na uwezo wa kutoa goli kutoka mfukoni mwake pale timu inapozidiwa; ndio huambiwa ameibeba timu. Ingawa Mkwasa ndiye kocha bora kabisa tuliye naye kwa sasa, hatuwezi kumfananisha na makocha wa kigeni wa timu nyingi tunazokutana nazo, ikiwamo Algeria. Ndio maana yeye na Kibadeni wetu walishindwa hata kukadiria kwamba Algeria wangeingia kivingine kipindi cha pili cha mechi ya awali na Algeria; sikwambii hiyo ya marudiano. Tatizo halikuwa substitution, tatizo ni sisi kutobadilisha namna ya uchezaji baada ya wao kubadilisha
5. Uzalendo ni mzuri, ila usizidi uhalisia. Kweli tunapenda makocha wazalendo wapewe timu ya Taifa, lakini tuwe tukijua pia kwamba hata timu zilizotuzidi sana uwezo zina makocha wa kigeni walio bora. Anayebisha kwamba kwa ujumla wao makocha wazalendo wa Kiafrika siyo bora, anitajie mmoja wao tu anayewaniwa na klabu yoyote ya Ulaya Kama vile wanavyowania wachezaji wa Kiafrika. Kwa timu zenye uwezo unaofafanana, yenye kocha bora zaidi ndio hutegemewa kushinda. Lakini iwapo timu tunayocheza nayo ni bora kuliko yetu, na kocha wake ni bora kuliko wetu, tutegemee nini kama siyo 7-0?
6. 'He who shall not when he may, when he will he shall have nay.' Kwa Kipemba tungesema 'Apewaye asitake akaringa, aja taka asipate akizinga (akitafuta)'. Tulipewa nafasi kadhaa za magoli kipindi cha kwanza cha mechi ya kwanza lakini hatukuzitumia, tulipokuja kuzitaka hatukuzipata. Wenzetu kila walipopata hawakufanya ajizi. Mkwasa anahusianaje na hilo?
7. Na kadhalika.