Taifa Star kufungwa, tatizo ni uwezo mdogo wa kocha?

Taifa Star kufungwa, tatizo ni uwezo mdogo wa kocha?

Timu imeenda jumapili Algeria, wamekaa almost three days, walikuwa wanakula wapi? Walienda na chakula chao? Najaribu kuliangalia hili kutokana na fitna za waarabu hasa wanapotambua timu wanayocheza nayo siyo ya kudharauliwa.

Inawezekana walifakamia mabiriani bila tahadhari, ni mtazamo wangu tu, maana goli saba ni nyingi kwa timu ile ile iliyotuonyesha kandanda safi pale Dsm.
 
Hapa Dar tulikuwa na uwezo wa kuwapiga Algeria hata goli saba lakini Ukosefu wa umakini wa Wachezaji matokeo yake tukakosa migoli ya Wazi



Sasa mkuuu hapa kwa jibu lako wewe umeona tatizo ni kocha ama wachezaji?....nimeuliza kwa mtazamo wa mleta mada
 
Lakini si nimesikia kuwa JECHA kafuta hayo matokeo mpaka watakapotangaza tena moja ya sababu ni kuwa Rais Maghufuli bado hajaruhusu safari za nje ya nchi?
Au nimedanganywa wakuu msaada please kwa mwenye taarifa za kufuta matokeo atujuze.
 
Wabongo kwa kujipa matumaini tunaweza angalia kikosi chao kilichoanza halafu linganisha na cha kwetu ndipo utagundua ni ndoto kuwafunga:

1.R.M'Bolhi (Antalyaspor)
2.A.Mandi (Reims)
3.F.Ghoulam(Napoli)
4.M.Zeffane(Rennes)
5H.Belkaroui(Club Africain)
6.C.Medjani(Trabzonspor)
7.Y.Brahimi(Porto)
8.W.Mesloub(Lorient)
9.N.Bentaleb(Totternham)
10.I.Slimani(Sporting Lisbon)
11.R.Mahrez(Leicester city)
 
Mpira ni tactics, mbona hushangai ronaldo kujiangisha angusha au barca, kama wao walijiangusha wakashinda kwanini na sisi tusingejiangusha tushinde???

Michezaji mikubwa lkn mijinga kuanguka ovyo ovyo utadhani inapata dege degeee, mfyuuuh Aibuuu. Nashangaa eti hiyo hiyo kila mwaka ndo inaliwakilisha bara la africa kombe la dunia, Aibuuuuu
 
TATIZO Letu sio Kocha wala sio wachezaji....NI SERIKALI YA CCM ILIYOFELI KILA SEKTA

Tusipoiondoa CCM Msitarajie jema lolote
 
Michezaji mikubwa lkn mijinga kuanguka ovyo ovyo utadhani inapata dege degeee, mfyuuuh Aibuuu. Nashangaa eti hiyo hiyo kila mwaka ndo inaliwakilisha bara la africa kombe la dunia, Aibuuuuu

nyie mmezuiwa kujiangusha

achen visingizio
 
Mkwasa hastahili lawama wachezaji wa stars uwezo wao ni mdogo mno! ?
Nionavyo:
1. Tatizo la Soka letu sio kocha, siyo wachezaji, siyo Simba na Yanga. Ni kutojua mfumo saahihi wa kuendeleza Soka lenyewe kutoka lilipo. Huwa tunadhani tu kwamba labda tunahitaji kocha mgeni, labda exposure, n.k. Lakini kuzuka tu na kutafuta exposure ama kocha bila ya kwanza kuchambua hali ya Soka letu ili kujua njia ya kufuata ni sawa na kumtia maji baridi mgonjwa wa homa anayeunguza, tukidhani ndio tumemtibu.
2. Serikali, TFF, Vilabu na wadau wengine watafute wataalamu wa kuendeleza soka ili waitafiti hali yetu na kutushauri la kufanya. China wameshafanya hivyo na hivi sasa ndio wanaendeleza mikakati iliyotokana na ushauri kama huo. Tusikurupuke tu kuanza na makocha ama akademi.
3. Wakati tunajiandaa na hilo, tusitarajie kupiga hatua ya maana kwenye Soka. Ama tuwache kushiriki michuano ya kimataifa kwanza, au tuwe tunaridhika na matokeo. Sisemi kwamba tusitafute makocha ama wachezaji wazuri. Nasema kabla ya utafiti nilioupendekeza na utekelazi wa maono yake, tusitarajie matokeo mazuri yaliyo endelevu.
4. Tunapotathmini wachezaji na makocha wetu, tuelewe mipaka ya uwezo wao. Mbwana Samata si wa kiwango tunachomkuza, ingawa ndiye fowadi wetu bora kwa sasa. Kwa sifa na mategemeo tuliyomwekea, alipaswa kufunga angalau magoli matatu peke yake kwenye kipindi cha kwanza cha mechi ya awali. Kadhalika Ulimwengu. Mchezaji wa kiwango tunachompakazia Samata lazima awe na uwezo wa kutoa goli kutoka mfukoni mwake pale timu inapozidiwa; ndio huambiwa ameibeba timu. Ingawa Mkwasa ndiye kocha bora kabisa tuliye naye kwa sasa, hatuwezi kumfananisha na makocha wa kigeni wa timu nyingi tunazokutana nazo, ikiwamo Algeria. Ndio maana yeye na Kibadeni wetu walishindwa hata kukadiria kwamba Algeria wangeingia kivingine kipindi cha pili cha mechi ya awali na Algeria; sikwambii hiyo ya marudiano. Tatizo halikuwa substitution, tatizo ni sisi kutobadilisha namna ya uchezaji baada ya wao kubadilisha
5. Uzalendo ni mzuri, ila usizidi uhalisia. Kweli tunapenda makocha wazalendo wapewe timu ya Taifa, lakini tuwe tukijua pia kwamba hata timu zilizotuzidi sana uwezo zina makocha wa kigeni walio bora. Anayebisha kwamba kwa ujumla wao makocha wazalendo wa Kiafrika siyo bora, anitajie mmoja wao tu anayewaniwa na klabu yoyote ya Ulaya Kama vile wanavyowania wachezaji wa Kiafrika. Kwa timu zenye uwezo unaofafanana, yenye kocha bora zaidi ndio hutegemewa kushinda. Lakini iwapo timu tunayocheza nayo ni bora kuliko yetu, na kocha wake ni bora kuliko wetu, tutegemee nini kama siyo 7-0?
6. 'He who shall not when he may, when he will he shall have nay.' Kwa Kipemba tungesema 'Apewaye asitake akaringa, aja taka asipate akizinga (akitafuta)'. Tulipewa nafasi kadhaa za magoli kipindi cha kwanza cha mechi ya kwanza lakini hatukuzitumia, tulipokuja kuzitaka hatukuzipata. Wenzetu kila walipopata hawakufanya ajizi. Mkwasa anahusianaje na hilo?
7. Na kadhalika.
 
Jamani Bongo kwa Mpira wachezaji wengi hawajitumi sawa sawa, hata kama ungeleta kocha wa Barcelona ni kupoteza mali za Taifa bure. Kikwete aliwekeza bajeti kubwa kwa timu hii na kuipa exposure za kutosha ikiwa ni pamoja na kuleta makocha kibao lakini wapi? Nashauri watanzania tuwekeze nguvu hata katika sekita ya Afya walau iboreshwe kuliko kupoteza mamilioni ya pesa kwenye Mpira.

Wewe na wengine wengi mnaolaumu Taifa Stars ni watu wa ajabu sana. Mimi nataka niulize jambo: Ukiachilia mbali huo mpira wa miguu, ni FANI IPI au JAMBO GANI Tanzania iliwahi kushika nafasi nzuri? Usinitajie rushwa na magonjwa, nauliza vitu positive.

Palikuwa na program inaitwa Airtel Inter university Challenge ikiendeshwa na kampuni ya Airtel ambapo vyuo vikuu mbali mbali vya Afrika vilishindanishwa kwa masuala ya kitaaluma. Ni lini uliwahi kuona chuo kikuu cha Tanzania kimefika angalau robo fainali?

Hakuna haja ya kuwalaumu watu wanaocheza mpira kwa kujitolea tena wakiwa na elimu ya darasa la saba ikiwa tunao waliofika chuo kikuu na bado wanatusainia mikataba mibovu. Tuwe fair, tatizo lipo tangu wizarani.
 
Mimi siku zote huwa nasema makocha wazalendo wa kitanzania uwezo wao huwa mdogo lakini huwa wanataka kulazimishia mambo makubwa matokeo yake ndo 7-0

Tanzania kama tungekuwa tumepiga hatua kisoka tungeona mchango wa hawa makocha wazalendo lakini kwa hali hii ni sawa kumchukua mwalimu aliyefail mtihani akafundishe wanafunzi halafu mtegemee wanafunzi hao kufaulu.

Sasa Tanzania tunahitaji kocha wa kigeni mwenye rekodi nzuri ya ufundishaji na mwenye kukizi viwango vya kimataifa.


Bill Clinton ana rekodi nzuri ya uchumi wa Marekani, vile vile Paul Kagame na Narendra Modi wa India. Kwa mtazamo wako huo, tukilinganisha na kiwango cha rasilimali zilizopo nchini, kuna haja ya kumleta mmojawapo kati yao kuwa mkuu wa nchi yetu?

Acheni mawazo ya kitumwa, tunapaswa kujitathmini kama Taifa. Sio kila siku lawama kwa watu wadogo wadogo, kuna lipi tulilofanikiwa kama Taifa?

1. Mkonge HOI
2. Kahawa HOI
3. Chai HOI
4. Tumbaku HOI
5. Pamba HOI
6. Urafiki HOI
7. Fishnet KUSHNEI
8. TAFICO KUSHNEI (Pamoja na bahari yooooote hii, samaki unaowaona mitaani wakiuzwa kwenye maboski wanatoka Msumbiji)
9. Mlima Kilimanjaro umepoteza theluji kwa 80%
10. Kiwango cha elimu kimeshuka hadi tumeongeza gear number 5, hakuna neutral

Huku kwoooote huku ni Mkwasa?

Tuanze na Rais wa kigeni basi
 
Michezaji mikubwa lkn mijinga kuanguka ovyo ovyo utadhani inapata dege degeee, mfyuuuh Aibuuu. Nashangaa eti hiyo hiyo kila mwaka ndo inaliwakilisha bara la africa kombe la dunia, Aibuuuuu
we ni mtanzania mwenzangu, sote tunaumia kwa kichapo!! ila tusijipe moyo mahali pasipo faa, we unaona aibu kuanguka wenzio ndio washasonga mbele!!
 
Back
Top Bottom