Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Jana nilitazama kiwango cha Taifa Stars ikicheza na Somalia nikafurahi jinsi timu ilicheza kwa balance ya hali ya juu huku ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, Sureboy, Farid na Feisal wakiharakisha mashambulizi mwanzo mwisho ukuta wa Mwamnyeto, Job, Kibwana na Msheri ukiwazuia Somalia kwa akili kubwa na kitaalamu zaidi nikashangaa imekuwaje tena huwa hatuchezi hivi baadae nikaona wazi kumbe Nabi alikuwa kwenye psychology ya wachezaji wa Yanga aliowafundisha kutulia na kucheza mpira.
Kuna muda niliona wachezaji wa Simba kutokuwa makini na wakipoteza sana mipira na kucheza kwa papara zisizo hitajika! Tshabalala hakuwa mchezoni na alibabaika mara nyingi na kugawa mipira kwa wapinzani wetu Somalia! Mzamiru alitoa pasi nyingi zisizo na macho na zikapotea na ilionekana kama vile Manula mechi ilimshinda kwa kutokuwa makini langoni akaomba kutolewa japo Kibu Denis nae alijitahidi kuruka ruka tu bila maajabu yoyote.
Pengo kubwa la wazi lilikuwa la Zawadi Mauya ambae nafasi yake ilichezwa na Mzamiru ambae alizembea sana na kupoozesha mashambulizi ambayo kila mara Dickson Job aliyaanzisha! Mzamiru alikuwa slow sana akikosa kabisa akili ya kushambulia kama wenzake wa Yanga yeye akiwaza kukaba, kupora mipira na kurudisha nyuma akifuata formula za Simba, Yanga wao formula yao daima mbele, peleka mpira mbele kafunge sio kuupakapaka rangi tu!
Jana nilihesabu wachezaji nikaona Yanga tulitoa karibu Robo tatu ya timu ya Taifa na ikatawala mchezo na kushinda vizuri tu, jee hii imekaaje? hii ina maana gani kwa mustakabali wa national team? Je Nabi na Eng Hersi waongezwe benchi la ufundi?
Huu msemo umejidhihirisha ni wa ukweli " Asikwambie mtu Yanga tamu" usipoila utainywa usipoinywa utaioga! ukiziba masikio utaiona kwa macho , ukifumba macho utaisikia tu mirindimo na fataki zake zikirushwa nchi nzima kutokea Sheikh Amri Abeid stadium!!