Taifa Stars imeshinda kwa kudra za Mungu tu, haikustahili

Taifa Stars imeshinda kwa kudra za Mungu tu, haikustahili

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huu ndio ukweli unaofichwa, shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu pekee, baada ya Stars kufunga goli, dk zote zilizosalia tumepumulia mashine, kuna wakati nimeshangaa wachezaji wa Namibia kukosa magoli ya namna ile mbele ya difensi yetu mdebwedo kiasi cha kushangaza na kuleta maswali ya kutaka kujua walikookotwa mabeki wetu.

Timu haijui kujilinda wala kukaba kiasi kama tukikutana na timu yenye kasi tutapigwa kontena la magoli .

Sijivunii ushindi tulioupata maana ni ushindi wa Bahatisha Ndulute.
 
Lkn hakuna cha ajabu miaka yote tupo hivyo hivyo kikubwa usiwe na matokeo yako mfukoni
 
Mimi bado ntaendelea kumlaumu kocha....hakufanya vizuri kwenye kuchagua wachezaji....Kuna baadhi ya wachezaji wazuri amewaacha...wangeweza kusaidia timu angalau....kuliko hao alionao.
 
Tukifungwa: Kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunza kunyoa.

Tukishinda: 1. Tumebahatisha wala timu haikucheza vizuri
2. Wametuachia tu kwakuwa wao hawakuwa na pressure na hii match (Eg. TZ vs Ug)

Sijawahi kuwaelewa waTanzania wenzangu.
Japo nakubali timu bado sio nzuri. Ila sijawahi kuona hata siku moja tukaikubali timu hata kama siku hiyo tumeshinda au tumefungwa.
 
Mm bado ntaendelea kumlaumu kocha....hakufanya vizuri kwenye kuchagua wachezaji....Kuna baadhi ya wachezaji wazuri amewaacha...wangeweza kusaidia timu angalau....kuliko hao alionao.
Yeye na mwajiri wake walimgwaya yule mzee mjuaji wa kila kitu. Binafsi siwezi kuwalaumu, ingawa ni ukweli ulio wazi! Ndairagije uwezo wake ni wa kufundisha tu vilabu.

Kupewa timu ya Taifa, tena kubwa kwa Ukanda huu wa Afrika Mashariki la Tanzania, huku yeye mwenyewe akitokea ka nchi kadogo kama Burundi, hakika ni dharau kubwa kwa Makocha Wazawa. Hawana budi kujitafakari na kuona ni kwa namna gani hawaaminiwi na TFF.
 
Huu ndio ukweli unaofichwa, shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu pekee, baada ya Stars kufunga goli, dk zote zilizosalia tumepumulia mashine, kuna wakati nimeshangaa wachezaji wa Namibia kukosa magoli ya namna ile mbele ya difensi yetu mdebwedo kiasi cha kushangaza na kuleta maswali ya kutaka kujua walikookotwa mabeki wetu.

Timu haijui kujilinda wala kukaba kiasi kama tukikutana na timu yenye kasi tutapigwa kontena la magoli .

Sijivunii ushindi tulioupata maana ni ushindi wa Bahatisha Ndulute.
Na kweli.
 
Back
Top Bottom