Taifa Stars mmejua kutudhalilisha sisi Wachambuzi

Taifa Stars mmejua kutudhalilisha sisi Wachambuzi

Ningekuwa na Mamlaka na Wizara yao ya habari, ningewaundia Chombo cha Kiaaluma kwamba watakaoruhusiwa kufanya kazi ya Utangazaji,

Ni wale wenye fani hiyo na lazima wawe wamesajiriwa na Bodi kama ilivyo Wahandisi, Madaktari, Wagavi na Wanunuzi, MaSekretari n.k ili kuondoa Ukanjanja wao

CC Pascal Mayalla
Watakufa njaa.
 
Kwenye sheria ipo sijui kwanini mpaka sasa bado haijaundwa!
P
 
Kwenye sheria ipo sijui kwanini mpaka sasa bado haijaundwa!
P
Kuna haja wangeharakisha huo Mchakato ili kutuondolea Waandishi wasio na weledi.

Sasahivi imekuwa kawaida kuona mtu yeyote maarufu eti naye anakuwa Mtangazaji au Mchambuzi wa Habari.

Hali imayopelekea wale waliosomea taaluma husika kukosa ajira lakini pia kufanya mmomonyoko wa maadili miongoni mwao.
 
Kumbe Ng'ombe wa maskini hazai. Makala ndeefu tulizoandaa kuweka magazetini na mitandaoni tumelazimika Kuzifuta kimyakimya. Mpaka Sasa wengi tuko vitandani hatujaamka tunahisi tukitoka nje tunaonana na Kibu Denis akiwa kashikana mkono na Dickson Job wakituukiza "Mlisema hatufiki mbali hapa ni wapi?"

Taifa Stars nyie siyo wa kutifanyia hivyo Sisi na hadhi yetu! Leo ilikuwa siku ya kukusanya maokoto Kwa kauli mbiu ya "Tulijua tu, kiko wapi?"

Taifa Stars mlichotufanyia Wachambuzi Bora tukajifiche Kizimkazi.
wengi walishaandaa makala za kuwa wamefungwa na wameshindwa kufuzu. hata mimi niliamini itakuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom