Taifa Stars waenda Cape Verde bila Dreamliner

Taifa Stars waenda Cape Verde bila Dreamliner

Tuache kudanganyana hapa!Mimi nimekaa Cape Verde takribani miezi sita.Wenzetu wana ndege kubwa tatu :airbus mbili na boeing 737-800 Next Generation ambayo ina uwezo wa kubeba abiria si zaidi ya 230. na zote zinapiga masafa ya Europe mpaka Caribbeans sasa huyu mzushi anayesema eti "hawana uwanja wa ndege wa kutua dreamliner ya Tanzania anaumwa au ni mgonjwa?"
HIvi visiwa vinapokea watalii zaidi ya mia sita kwa siku.
WATANZANIA ACHENI UZUSHI WA KIJINGA!
 
October 9, 2018
Dar-es-Salaam, Tanzania


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania – Taifa Stars kitaondoka usiku wa leo kuelekea mjini Praia, Cape Verde kwa ndege ya kukodi kuifuata timu ya taifa ya huko kwa ajili ya michuano ya kufuzu kwa michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kambi ya timu hiyo Waziri Mwakyembe amesema, mabadiliko ya safari hiyo kutoka Dream Liner na kuamua kukodi ndege yanatokana na ufinyu wa uwanja wa ndege wa Mjini Praia ambao hauwezi kutua ndege kubwa. Aidha Waziri Mwakyembe amewataka wachezaji wa Taifa stars wakacheze kwa kujituma ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo huku akiwasihi watanzania kuiombea timu hiyo. Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia na Nahodha Msaidi wa Taifa Stars Himidi Mao wameelezea maandalizi ya mchezo huo.
Habari & Video kwa hisani kubwa ya:
Source: Global TV Online

Sio kweli kuwa uwanja ni kikwazo, kwakuwa viwanja vyote vinajulikana
 
Cheki madege makubwa uwanja wa kimataifa wa Cape Verde kwa jina la Praia Nelson Mandela international airport (RAI) ikiwemo hili la shirika la ndege la Cape Verde, Cabo Verde Airlines. Uwanja wa kimataifa wa Cape Verde ulipanuliwa mwaka 2012 na kuwekewa vifaa vya kisasa kuhudumia ndege zote kubwa pamoja na ongezeko la abiria kutokana na kisiwa hicho kuwa kivutio kwa utalii wa kimataifa.
Nmeamin ule msemo wa "njia ya muongo ni fupi"
 
Uwanja wa ndege cape vede ni mdogo!??????

Walipokuwa wanatwambia tutakwenda na ndege yetu walikuwa hawaujui huo uwanja???

Lakini kubwa ni kwamba,wametudanganya kabisa,uwanja wa ndege wa cape vede ni international airport, sio kweli kwamba hauna uwezo wa kupokea dream liner!!!

Watwambie tu kuwa bwana mkubwa amekataa!!!
Sema hivi. Dereva wetu ndiyo mdogo kutua kwenye uwanja huo mkubwa kumzidi.
 
" Dream Liner na kuamua kukodi ndege yanatokana na ufinyu wa uwanja wa ndege wa Mjini Praia ambao hauwezi kutua ndege kubwa" mmh sijawahi kushuhudia uongo wakijinga kama huo....badala ya kusema abiria wakuchangia wamekosekana hizo $1500 na 2000 sio mchezo kwa usawa hu....cape verde haina kiwanja cha kimataifa Dreamliner kutua ni kichekesho
upo sahihi ...... ina maana hawakujua tangu mwanzo kuwa wanna ni mdogo ?.... mpaka hata kukata ticket? uwongo huu ni kiboko
 
Routes
There are 192 flights on 28 different routes from Praia Nelson Mandela International Airport, connecting RAI to 27 different cities in 14 different countries. The most popular routes connect Praia
Aeroporto internacional da Praia Cabo Verde
Icelandair lands at Praia Nelson Mandela airport

Njia ya mwongo fupi......
 
Back
Top Bottom