Tairi ya Gari upepo ni 35, Baiskeli ni 60 na Trekta lile kubwa kabisa ni 15.60. Why and How?

Tairi ya Gari upepo ni 35, Baiskeli ni 60 na Trekta lile kubwa kabisa ni 15.60. Why and How?

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,053
Reaction score
3,259
Sielewi kabisa binafsi hii physics imenishinda, inakuaje Tairi la Gari normal Cars upepo wake kwa kutumia ile geji huwa zinaingia 30, 35 na nyingine kubwa kama cruser huingia 40, Baiskeli tairi lake kwa kutumia geji hiyo hiyo upepo wake unaingia 60, lile tairi kubwa kabisa la Trekta upepo wake unaingia 15 kwa kutumia Geji hiyo hiyo.

Nimewaza kuhusu kipenyo hapana haiingii akilini.

Je! Kuna siri gani ya physics kwenye hili?
 
Mmmh..ngoja nisubiri wajuzi. Je, kizio Ni sawa? PSI au mm Hg
 
Mambo mengine yanashughika tu akili zangu
 
Swali zuri Sana. Ngoja wataalam wake tuone inakuaje. Ila maudamvu udamvu yangu. Pressure is equal to force over area.
The higher the area the lower the pressure.

Sasa ule mji tairi wa trekta una bonge la area linagusa ardhi. Pressure ni ndogo kwa maana hiyo. Baiskeli kaji area kadogooo pressure kubwaaaa.

Sijui lkn.
 
Kadhalika kwa mabati ya kuezekea na ya kutengenezea mabodi ya magari

Geji 32 ni kama karatasi
Geji 30 ina thickness kubwa kidogo
Geji 28 ina thickness zaidi ya 30
Na kuendelea
Hili nimemuuliza mtaalam ngoja nisubr majib
 
Hapa nionacho Logic ya haraka hapa ni kwamba namba ikiwa inaonekana kubwa kitarakimu ndio ndogo ktk volume na mchawi ni meter ilivyotengeneza isome ila sio kilichomo ndani...and vice versa
 
Pressure = Force/Area. Kwa mfano tumeinginza force ya 12, lakini pia tuna area ya mpira wa baskeli ni 3, mpira wa gari ndogo ni 4 na mpira wa prado ni 6. Hapa tukitafuta pressure maana yake baskeli ni 4, gari ndogo ni 3 na prado ni 2. Na hizo ndo data ambazo ni calculated kwenye gauge
 
Ebu tuanze na Volume & Pressure.
- the greater the Volume of air in the tyre, the less Pressure it can withstand.
Kwa hiyo kutokana na Ukubwa wa tairi la trekta, Pressure itakuwa ndogo ukilinganisha na tairi la baiskeli ambalo Volume yake ni ndogo.
 
Back
Top Bottom