Taja faida za kuishi peke yako

Taja faida za kuishi peke yako

sijawahi kuona faida ya kuishi mwenyewe..... ubinafsi uoga wa maisha na kutokua mwanaume kamili kunawaponza sana vijana wenzetu ukiangalia sababu nyingi ni uoga na ubinafsi alafu swala la uhuru ni jambo pana sana...
huwezi niambia nilale mwenyewe kama panga au nikae dinning mwenyewe kama mjusi Kisa uhuru sjui kunyetuka..... tukumbuke kama mwanaume ww ndio Mkurugenzi wa maisha yako unalotaka liwe litakua usikurupuke tu ukaona maisha machungu.....


Nafikiri furaha nipatayo na wanangu eti nianze kukaa mwenyewe alooo siwezi......
Kama wewe huwezi usifikiri wote hawawezi.

Na kamwe usikariri maisha kwamba jinsi ulivyo wewe basi dunia nzima watu wapo kama ulivyo wewe.

Pia usiforce vitu usivyoweza unafikiri utaweza haya mambo mengine ni asili ya mtu tu kama sio asili yako lazima uhisi unateseka kwa sababu unalazimisha maisha yasiyo yako.
 
Baada ya 14 years of marriage na vita visivyokoma Nilikubali kuwa mjinga
Nikamuachia kila kitu Kwa sababu ya watoto wangu. Nikaondondoka na Gari yangu na nguo tu. Nikaenda kupangisha Nikanunua fenicha nikaanza maisha upya kabisa from 0
Huu ni mwaka wa Tatu tangu nimekuwa Bachelor. Niko huru Sana. Nina furaha Sana
Ila sikuwahi kujua kuna kitu linaitwa Upweke
Hiyo hali ikija unatamani utafute tu mahali
hapafungwi usiku ukakae hapo
Upweke Ni tatizo lingine Na Nikifikiri kuoa upya Ndio naona narudi kule kule
Ukiona unasumbuliwa na kitu kinachoitwa upweke ujue unalazimisha maisha yasiyo upande wako.
 
Upweke hauja wahi Kuna mbabe, halafu kukaa mwenyewe mi langu na sio lako mkuu
Ukiona unasumbuliwa na upweke ujue maisha ya peke yako si aina ya maisha yaliyo upande wako.

Acha nikuambie kitu kimoja watu wanaopenda kuishi peke yao changamoto inayo wakabili ni kuzungukwa na watu na wala sio upweke wewe upo kinyume na hicho nilicho andika ujue hujazaliwa kuishi peke yako.
 
NGAPI??

1. Asubuhi naondoka siachi kodi ya meza.
2. Naangalia TV uku nimevaa headphones
3. Nakula ninachotaka na muda nnaotaka.
4. Ndani hakipotei kitu ovyo ovyo
5. Haina haja ya kutandika nikiamka wala kukunja neti
6. Bili ya umeme na maji ndogo
7. Sina haja ya kulipia DSTV wala Azam kila muda.
8. Na nikilipia, guess nagombania remote na nani?? MYSELF.
9. Nachagua pa kulala leo chumbani kesho sebuleni.
10. Mbu zimeboreka damu taste moja zimehama.


HASARA
1. Ikitokea ume umwa ghafla. Ukizidiwa. Shida sana
2. Ukikosa hela ya kula unalala njaa.
3. Unakula vibaya mara nyingi chips au kilichopo kwa mama ntilie
4. Sometimes nikishaongea Ijumaa kazini jioni siongei na mtu ana kwa hadi j3 tena kazini
5. Depression
6. ..
 
Back
Top Bottom