Taja faida za kuishi peke yako

Kuna likizo moja waifu alikua anaenda kwao akabeba watoto wote nikabaki mm tu nyumba inaniangalia .Siku ya kwanza nikajisikia ka uhuru furani sisikii kelele za madogo nikaona haya ndo maisha nimepiga wiki moja tu yakanishinda maana nilikua nimewamiss wanangu na wife hatari nikagundua uwepo wao ni faraja kubwa sana kwangu👋🏽
 
NGAPI??

1. Asubuhi naondoka siachi kodi ya meza.
2. Naangalia TV uku nimevaa headphones
3. Nakula ninachotaka na muda nnaotaka.
4. Ndani hakipotei kitu ovyo ovyo
5. Haina haja ya kutandika nikiamka wala kukunja neti
6. Bili ya umeme na maji ndogo
7. Sina haja ya kulipia DSTV wala Azam kila muda.
8. Na nikilipia, guess nagombania remote na nani?? MYSELF.
9. Nachagua pa kulala leo chumbani kesho sebuleni.
10. Mbu zimeboreka damu taste moja zimehama.


HASARA
1. Ikitokea ume umwa ghafla. Ukizidiwa. Shida sana
2. Ukikosa hela ya kula unalala njaa.
3. Unakula vibaya mara nyingi chips au kilichopo kwa mama ntilie
4. Sometimes nikishaongea Ijumaa kazini jioni siongei na mtu ana kwa hadi j3 tena kazini
5. Depression
6. ..
 
Pole kiongozi, ni kweli usemalo upweke unatesa sana aisee.
 
Kaka hebu tulia, maana we huwezi elewa hii
 
Hahahaaaa taja faida kwa ñini unaishi single!

Faida ni nyingi sana Mkuu,kuanza kuorodhesha hapa hatutamaliza leo wala kesho mfano hapa nimerudi home viatu nimevulia kibarazani suruali nimevulia mlango mkubwa wa kuingia sebuleni begi nimeweka kwenye kiti shati nimeenda kuvulia chumba cha kati ambapo kuna kabati la nguo kisha nikatoka na taulo kwenda masterbedroom kuoga nikarudi tena sebuleni na taulo kujikausha maji huku nipo uchi nafanya mambo mengine na stress nilizo nazo hii leo kungekuwa na jini kisirani angevimbisha mdomo kama kapatwa na stroke na kelele juu,alafu kwenye swala la kula leo sina njaa sasa angekuwepo hapa angeanza Umetoka kwa malaya zako wamekulisha huko una fika huku hutaki kula mara akuambie urudi ukalale uliko kula.bora kuwa peke yako maisha ni kuchagua.
 
Kwenye msosi ni kwel aiseee kununua misos kunachosha, Kuna mwali akijaga naenjoy misosi kinoma mara ndizi, pilau, ugali n.k


Upweke, ni kipengele sana mda mwingine jf, you tube, insta na fb zinakukampan lkn bado upweke ni upweke


Ukiwa mwenyewe kuna namna nyumba kama inakua nyepesi hv
 
Wewe mshukuru Mungu tu. Usiombe yakakukuta.
 
kumbe majibu unayo hongera sana
 
Kuna mtu kakomaa Eti ukiona upweke, ujione hayo SI maisha yako😆.
Hajui upweke ni unkwepekabo
 
No 5😂 siku ya 4 leo
 
Umenshindaaa tabiaaa khaa ninechekaa sanaa
 
Nilikuwa naenjoy nilipokuwa msichana mdogo, I was a loner, who enjoys her own company. Nyumba safi, vitu vichache. Hasara yake nilikuwa naipata muda wa kula... chakula hakipiti kibaya hatari, that's when nilipojifunza kunywa supu ndio niliona hainipi kero....

Now it's almost impossible kuwa mwenyewe, siku mbili nyingi sitoboi nakonda hadi macho yanadumbukia ndani. So yeah to me naona it works better with age.

Watu wakiwepo wanaipa uhai nyumba, People need people.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…