Taja JF member au members ambao una hamu kabla hujatangulia mbele za haki angalau uwe umewajua

Taja JF member au members ambao una hamu kabla hujatangulia mbele za haki angalau uwe umewajua

Naamini kabisa kwamba wote tuliopo humu jf tuna umuhimu wetu kwa namna moja au nyingine ila hata hivyo haiondoi ukweli kwamba kuna baadhi ya wenzetu humu ( members ) ambao michango yao na uwasilishwaji wake huwa na mvuto sana kiasi kwamba inafika muda mtu unakuwa una hamu sana siku itokee tu uweze kuonana nae au umuone mubashara kabisa ili roho yako isuuzike.

Hivyo leo nimeona siyo vibaya nikiwashirikisheni nanyi ili kwa pamoja tuweze kuwataja hao members au member ambaye labda unaombea usitangulie kwanza kwa Mwenyezi Mungu Mbinguni kabla bado hujaonana au hujakutana nae kwani labda unampenda kiuchangiaji wake humu na anakuvutia sana na kila mara hukosi kumfuatilia mabandiko yake au mada zake.

Kwa kuanzia tu mimi natamani sana siku moja niweze kuonana na hawa members wa jf wanaonivutia na kunifurahisha mno hasa kwa aina ya michango yao na hata uchangamfu wao wa kiuchangiaji:
  1. Maxence Melo
  2. Mike Mushi
  3. Asha Dii
  4. Bridger
  5. Active
  6. Reserved
  7. Silencer
Karibu na Wewe Mkuu uweze kutaja members wako unaowakubali sana hapa jf.
Ningeanza na wewe mtoa mada maana najua una undugu na huyu hapa
GENTAMYCINE
Barbarosa
Illovo
TAMITO TOMATO
General Galadudu
 
Haha hapa inabidi niongee na mzee Asprin aniweke un'gen'ge siunajua kuhamia mitaa ya kishua bwana.

Maana huku uswahilini tushazoea kuongea kiswaengilish
Ha ha ha huku kwetu kama kalambwnda mkazuzuz
 
Ha ha ha huku kwetu kama kalambwnda mkazuzuz
Sehemu kama hizo lazima un'gen'ge ukae vizuri bwana. Zile yes you know kwenye comments hazitaniisha jiandae kutafuta dictionary [emoji3][emoji3]
 
Sehemu kama hizo lazima un'gen'ge ukae vizuri bwana. Zile yes you know kwenye comments hazitaniisha jiandae kutafuta dictionary [emoji3][emoji3]
Ha ha ha usjal mzee ukifika muda wa kuandikishiana niite Mie kama shahid hata dole gumba linatosha
 
Back
Top Bottom