Taja jina la shule ya msingi uliyosoma enzi hizoo

Taja jina la shule ya msingi uliyosoma enzi hizoo

Kinondoni Pr School ' 61 - ' 66 Enzi za mzee chipwete. Nnani anamkumbuka?? Mw Malendeja??
 
Hamukoko Primary School, ukerewe mwanza. Nakumbuka nilikuwa kwenye brass band, kwaya, ngonjera. Nilikuwa nacheza nafasi ya kwanza au ya pili darasa la kwanza mpaka la saba. Tulifaulu wawili tu, wakati namaliza form four nikasikia mwenzangu alifariki wakati tukiwa form two
 
Iburieni primary school 1995-2001 wilaya ya Rombo KLM. Darasa la tatu nilichapwa fimbo zisizo na idadi baada ya kumwita msichana darasani na kumwonyeshea ishara ya kumtaka kimapenzi. Niliumwa wiki , nilijiuguza kimya kimya. Darasani 2-5
 
shule ya msingi Yamu-kirua vunjo, katika kipindi chetu tulitembelewa na wageni wa serikal,mama zakia megji, pr sarungi na mkuu wa mkoa kipindi hicho. tulipewa nguruwe wa mradi
wakati fulani zilipita parachut 2 mwalim mkuu akagonga kengele ishara ya kitu chaajabu ambacho hakijawai kushuhudiwa na mtu yoyote, tulijificha chini ya madawati na waalimu.

Bila shaka watu wabaya walikuwa wanapita na maprachuti, Ulisali sala gani chini ya Dawati? Hahaha...
 
Mzumbe Primary (1-4) Nikahamia Nyoko P/S . Nilikuwa wa mwisho darasani wastani marks 90% .Masomo 8 jumla alama 768/800.
Darasa lilikuwa hatari. Nikafaulu Tabora boys.
 
Tuwe watulivu. Lengo la huu Uzi ni kujikumbusha ya enzi hizooooo!
Pia kuna wengine kupitia hii washawapata Schoolmates au classmates humu.

Amani itawale.

Ila mpaka sasa cjapata nliyesoma naye shule Moja.

Nakupenda Sana Mama Yangu
 
Back
Top Bottom