Taja Jina zuri Kwa mtoto

Happy

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Aniva

Shamila


sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Heshima Comrades.

Nimefuatilia kwa umakini mpana sana uzi huu. Nilichojifunza ni kwamba "Tumekosa Utamaduni Uhuru. Tunaelekea kuuzima kabisa utamaduni wetu", sababu ni nini lakini?. Usomi, utumwa mamboleo, ulimbukeni na maisha au nini?.

Yaani hatuguswi kabisa kuuenzi utamaduni wetu kupitia majina?. Majina ya kizunugu, kiarabu, kijerumani ya nini?.

Kuanzia Wachina, Waarabu, Wajapani, Wakorea, Wayahudi, Wafini, Waswedi na orodha inaendelea wana Majina yao ya asili. Kwanini sisi Afrika ndiyo wenye kasumba ya kuazima majina yao?.

Halafu eti mtu ana-comment {Fuata mambo yako, si uyataje na wewe jina unalolipenda} ?, serious?. N'nani alisema kuwa mtu mmoja mmoja ana uwezo wa kuwa mjenzi wa maaadili?. Na kwanini tu wepesi wa muendelezo wa falasafa ya kila mtu na lkwake badala ya kuwa sauti moja, utamaduni mmoja na kadhalika?. Shabaha yetu kama Taifa ni ipi katika Utamaduni, sanaa na michezo?.

Jina kama Francis, Errard, Dickson, Ekhart, Nasrat, Yvonne ya nini haswa wakati hata kuyatamka na uandishi wake hatuuwezi?.

Mbona tuna majina mengi mazuri ya kiswahili?. Ni kwanini tusijivunie hayo?. Tutafakari...

Tuguswe na kuendeleza utamaduni wa Mwafrika kupitia majina, mavazi, vyakula, nywele, rangi ya ngozi na kadhalika.

Wapo Wamarikani wengi wa Kaskazini wenye majina ya Kiswahili ambao nimewapenda mno kwa kuuenzi utamaduni wa Kitanzania. Kwa uchache tu ni kama wafuatao;

Talib Kweli (mwanamuziki wa Rap), Amiri Baraka (mwandishi, mwanaharakati, na mshairi), Haki Madhubuti (mshairi), Maulana Karenga (mwanzilishi wa sikukuu ya Wamarekani Weusi yenye jina la Kiswahili, Kwanzaa na Mkurugenzi wa Idara ya Masomo ya Waafrika katika Chuo Kikuu cha California, Berkley) na mke wake Tiamoyo Karenga, Maisha Ongoza, Mapinduzi Leo, Rafiki Mtumishi, Malaika Jabali (mcheza sinema), Fani Adili, Harambee Afrika, Ujamaa Muhammad, Akili Mali, Sheria Haki, Mtoto Wa Afrika, n.k.

Elimu ya kweli ni kujielewa, kuielewa jamii na kuuelewa ulimwengu. Usipoijua historia yako unakuwa sawa na mti usio na mizizi-Marcus Garvey (Yohana Mbatizaji wa watu weusi)

USHAURI.

Tuachane na Utumwa Mamboleo. Tuuenzi utamaduni wetu kwa kuwapa Wenetu majina ya Asili yetu na Utanzania. Tuachane na majina ya Kiarabu, Kiyahudi na Kizungu. Tuchague majina yetu yenye tafasiri nzuri na Kuwapa wenetu.

Ruhuksa kunikosoa na Kunielimisha.

Hekima Ni Uhuru.
 
Kwani shida ipo wapi?

Wewe ukiona haujapendezwa na hili jina we pita kimya kimya halafu utoe la kwako unaloliona lipo sawa.

Heshima Mkuu!

Unauliza kwani shida ipo wapi?, inaonekana hujui shida ilipo na hufanyi bidii yoyote ya kuutafuta ukweli ulipo ili kuzima kiu yako. Ungeomba ufafanuzi kwa naumbu nadhani ingefana sana kuliko kumwambia wewe ukiona hujapendezwa...

Halafu kupendezwa ndiyo jambo gani?, hapa naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hili (Nb: kwa kutumia mantiki).

Hoji kila unachokiona, dadisi, saili, uliza na kadhalika. Baada ya hapo unaweza kujiponya nafsi na hata upofu wa roho na macho. Usipofanya hili ubongo wako unakuwa huna tofauti na ubongo wa mbuzi ambao kimantiki unasubiri kuliwa na binadamu.

Ni kama vile Walter Russels, mwanamaono, msanii na mvumbuzi wa Marikani kaskazini alivyopata kunena "Mediocrity is self inflicted, genius is self bestowed". Katika lugha yake akimaanisha "Udunya ni maradhi ya kujitakia, kipaji ni kujiponya".

Jifunze si tu kubaki na unachokifahamu. Dunia nzima i mkononi mwako, kabila zote, asili zote, tamaduni zote na kadhalika. Msimamo ama itikadi kali juu ya chochote si jambo la kujisifia na kujiona u mtemi, ni udunya na maradhi ya kujitakia.

Elimu ya kweli ni kujielewa, kueelewa ulimwengu na kadhalika. Tuige kila kitu kutoka kila kona ila msingi na maudhui ni hapa nyumbani.

Hekima Ni Uhuru.
 
Heshima Comrade?.

Umesema majina huwa yanaamua hatima (Fate) ya watu maishani?. Kivipi?, naomba ufafanuzi katika hili.

Hujawahi kuwaona kina Masumbuko, Taabu, Shida, Kabaya, Matatizo, na kadhalika wametoboa maishani?. Unaishi wapi uje nikuonyeshe hao watu unaowaita hawajawahi kutoboa?. Pia ulikokuita kutoboa ndiyo nini?. Ni kwa kutumia vigezo vipi vya kimantiki ndipo mtu awe ametoboa kwako?.

Pia n'nawafahamu kina David, Davy, Daud na kadhalika ambao wana maisha ya kawaida tu na hawana vigezo hivyo ulivyovitaja. Pia ulikokuita kupendwa na Mungu ndiyo jambo gani?. Unaweza kulithibitisha hili la Mungu kumpenda mtu?.

My Take,

Kama ni Majina tuwape wenetu majina ya Kiafrika na yenye tafsiri yenye kuzingatia mantiki na si nje ya hapo. Kukopa jina kwa namna yeyote ile kutoka ng'ambo ni kielelezo cha namna Fikra zetu zilivyo za hovyo (kumradhi).

Hekima Ni Uhuru.
 
wewe ni Mpuuzi kweli yaani uzae wewe Jina ulitake kwetu? nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiria
Kwanini unatumia Lugha iso na staha katika Baraza?. Kwani kuuliza ni ujinga?.

Mleta mada kaleta ombi/ushauri. Kumuita Mpuuzi si sahihi kabisa, na ufanye kumuomba radhi. La sivyo nitaomba uongozi ukuchukulie hatua za kinidhamu haraka iwezekavyo.

Iishi "signature" yako. Usikwaze, usiudhi na kadhalika. Pia hutokwazwa, hutoudhiwa pia.
 
Kwahio mzee unataka kunishurutisha niombe radhi? Hahahahaa afu utawaambiaa mods sioo.....Kazaa yeye au mimi? au kasaidiana na mods kuzaa??...kuzaa mzae nyiee keroo mtupe sisi Hahahaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…