Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

...kwetu shinyanga... Kuna hizi kanuni...

1.Mwenye macho mekundu(hasa wanawake wazee)...ni mchawi... na kula panga ni jambo la kawaida(nashukuru mungu saivi haipo)
2.ikinyesha mvua yenye upepo mkali na vi mawe... Marufuku kesho kwenda shamba(50% wameshtuka)
3.ni marufuku kufunika koleo, kula mayai, miwa sehemu wanapochimba dhahabu...
4.ni marufuku kuchinja ng'ombe wa nyumbani...
5.mtu akikutapel au kukudhulumu usimshtaki wala kumroga... Jipe moyo ukijisemea "maguzu masese" maana yake manguvu yapo ya kutosha ko atapata tu mali tena...
6.ni marufuku kumdharau mgeni(mtu asie msukuma) hii sijajua maana ake...
7.mtoto ukila kiazi kikubwa au chakula chochote kama vile nyama, mhogo n.k... Utaangukia mlangoni
8.ni marufuku kufanya mapenzi na mvulana au binti wa jirani...
9.ni marufuku kuvaa nguo nyekundu wakati wa mvua... vinginevyo unakula radi...
10.uchawi wanachukulia kama michezo mingine kufanya maonyesho... Ukiutumia kwa nia mbaya au kuroga... Utajua ujui...

naleta zingne niwaulze wazee...
 
Sisi kikwetu kummega Mamaako au Dadaako wa Damu Ni Laana kubwa Sana hutotoboa muda mrefu unaumaliza Mwendo au unadata a.k.a Network Search Dish linayumba..!
Kuna family fulani hivi madogo walimpigaga mama yao mtungi, lakini wao n watu wa pombe kuanzia mama hadi watoto, na hao madogo wao ni pombe saa 24
 
Namba 4: Ukitaka kuchimja mnabadilishana na mfugaji aliye mbali au umaenda kununua mnadani?
 
1. Ikinyesha mvua ya mawe unatakiwa kuchota chumvi kidogo unaitupia huko nje kwenye mvua ili hayo mawe yasinyeshe au unapuliza filimbi.

2. Chombo (kama vile kikombe, bakuli au sahani) kikidondoka chini na kujifunika hiyo ni ishara ya mkosi.
 
Ukiwa na maumivu ya shingo mtafute mtu mashoto (left-handed) akushike na mashoto yake kama vile anakuzungusha shingo maumivu yatakoma mara moja.
 
Namba 4: Ukitaka kuchimja mnabadilishana na mfugaji aliye mbali au umaenda kununua mnadani?
...eeh sana sana huwa wanaenda kununua mnadani... Na msukuma mwenye ng'ombe anathamini ng'ombe kama mwanae... Tena mwanae awe wameshibana...
 
Mimi mwiko wangu ni kupeana mkono na mtu wakati tunasalimiana hasa kiganja cha mkono ,mtu aking'ang'ana sana kunipa mkono nakunja ngumi nampa kwa juu ya kiganja , huu ni mwiko kwangu, haiusiana na imani yoyote ni just mwiko tu.
 
Kwetu sisi ukipiga mdudu aina ya vunja chungu na kumuua, hyo hali inawez kukuletea kifo ama madhala flan juu yako
 
1. Ikinyesha mvua ya mawe unatakiwa kuchota chumvi kidogo unaitupia huko nje kwenye mvua ili hayo mawe yasinyeshe au unapuliza filimbi.

2. Chombo (kama vile kikombe, bakuli au sahani)kikidondoka chini na kujifunika hiyo ni ishara ya mkosi.
Namba mbili. Hata sisi tuliopitia kwa waganga wa nazi. Ile nazi inaandikwa manuizo yako kwa Maka peni nyekundu afu mganga anakupa anakwambia nenda njia panda kanuie afu vunja chini.
Sasa is ishara pekee ya manuizo yako kua hayajakubaliwa ni ile nazi kuvunjika na vipande kujifunika. Ila vipande vikijifunua apo umewini.
 
1. Ukiwa porini ukaona kiota cha ndege utakaporudi nyumbani usiseme wala kusimulia kuhusu kiota hicho ukiwa karibu na mafiga. Ukijichanganya ukasema chochote, kesho ukienda utakuta ndege kahama (kabla ya kumtega).

2. Ukiota ndoto mbaya usiku, amka uteme mate na geuza upside down shuka au blanket ulilojifunika. Hii itasaidia kutupilia mbali jinamizi hilo.
 
Kwetu mwanamke/Binti ukiwa unaongea na mwanaume/mvulana anaekuzidi umri ni lazima uinamishe kichwa. Ni marufuku kumuangalia usoni kwake
Nidhamu mbele kama tai. Wapi hii mkuu?
 
Desturi ya nyumbani kwetu ukisonga ugali ukimaliza mwiko lazima uuoshe. Marufuku kuacha mwiko mchafu. Hata sijui ina maana gani ila nimekua nayo mpaka leo nikimaliza kusonga ugali lazima nioshe mwiko kabla hata chakula hakijafika mezani.
Mkuu sorry kidogo unazungumzia mwiko ule ule wa ugali au mwiko mwingine maana mm akili yangu sijui n vip
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…