1. Ni mwiko kuingia shamba la mtu la miwa au mahindi na kuvunja Kisha kuondoka nayo, inaruhusiwa kama ni miwa basi ikate kdhaa, kaa humohumo shambani kula Kisha uondoke au kama ni mahindi unaruhusiwa kuwasha moto kwenye hilo shamba Kisha kata mahindi yanayokutosheleza kula na kushiba Kisha choma kula maliza, zima moto na uondoke.
2. Mwiko kuhadithia hadithi mchana, utaota mkia.
3. Kwenye ukoo wetu kula utumbo wa mnyama yeyote mwenye miguu minne ni mwiko.
4. Ni mwiko Kupuliza moto kwa pamoja na ikitokea mmepuliza pamoja mmoja anatakiwa kutema mate juu na mwingine chini. Inaaminika msipofanya hivyo basi mtakuja kufa kwa siku moja.
5. Kuna mchezo mmoja tunauita 'buriburi' mnaketi chini kwa mzunguko kunakuwa na kimkaa au kijiwe unakificha kwa mikono nyuma na unaitoa mbele anayekufuatia anaonesha umekificha mkono gani, akipata unampa anaendelea yeye na anayemfuata hivyohivyo. Akikosa basi unakuwa ni ushindi na unaendelea kucheza. Sasa mkitaka kuanza kucheza ni lazima aanzishe mtu ambaye baba yake au mama yake alishatangulia mbele ya haki. Kama wote Wana wazazi basi mtoto wa mwisho kuzaliwa aliyepo hapo ndio huanzisha huo mchezo. Kwahiyo ni mwiko kwa mtu yeyote tu kuanzisha huo mchezo.
6. Kusonta kaburi na kidole ni mwiko.
7. Mwiko kulima usiku yaani jua likizama huruhusiwi kulima.
8. Kupanda mbegu shambani kwa kifaa chenye masizi ni mwiko, huashiria mbegu kutokuota maana ni kama unapanda mbegu zilizokaangwa.
9. Ni mwiko kumruka mtu, ikitokea inabidi urudi kwa kumruka kuelekea ulikotoka (kurudisha mruko [emoji4])
Ipo miiko mingi sana sana. Naweza Andika Kitabu.
Hii nafikiri ni ndani ya Morogoro kama nitakuwa sahihi...
Sambamba na yote hapo, pia...
1. Ni mwiko kuingia shamba lenye mahindi baada ya kunyolewa, mpaka siku ya pili.
2. Ni mwiko kuburuza kuni au kamba na kuingia nayo ndani.
3. Ni mwiko kusimama wakati wakubwa wamekaa, au kukaa wakati wakubwa wamesimama.
4. Ni mwiko kukalia kaburi.
5. Ni mwiko kuacha mchi kwenye kinu usiku.
6. Ni mwiko kuua chura, mbayuwayu na vunjachungu.
7. Ni mwiko kukaa au kusimama mlangoni.
8. Ni mwiko kutokea dirishani.
9. Ni mwiko kupima kimo cha MTU kwa kiganja, tumia kiwiko.
10. Tuna majina ya Mizimu ambayo ni mwiko kutamka kwa kujifurahisha au kujiapiza huku unajua unadanganya, YATAKUFIKA TU UTAJUTIA.
11. Ukiwa na njaa njiani, ingia shambani kwa MTU, kata muwa au chimba muhogo ule ila usitoke nao, hata kipande kimoja. Ikiwezekana panda pegu.
12. Usiache nguo usiku nje, ulizofua.
13. Usilipite kaburi la babu au chifu bila kukata jani lolote na kuliweka juu ya kaburi. Hasa kama ni wa ukoo wako.
14. Ni mwiko kutupa chakula, hakikisha unakimaliza au unatafuta MTU.
15. Usimruke mtoto.
16. Usiimbe wala kuongea chooni, au kupiga mluzi.
17. Ni mwiko kumpiga mtoto kwa fagio.
18. Ni mwiko kuchezea chakula, hata kama hutakitupa. Mfano kulirusharusha tonge kisha ule.
19. Ni mwiko kurusha chochote nje kutokea ndani.
20. Ni mwiko kutoka au kuingia ndani ya nyumba kwa kukimbia.
21.....