Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Ni mwiko kula mnyama pori. Tunakula mbuzi, ng'ombe na kondoo tu hata kuku hatuli.

-Ni mwiko mwanamke kula maini na hata kijana kama mmechinja ukishaandaa maini ndio huanza kuliwa ila mpaka waanze wazee ndio wakupe go ahead na wewe ule. Ukionja maini hata kipande kidogo kabla ya wazee ujue hapo umekula mfugo wote na haitahesabika kama pamechinjwa kitu inabidi ulipe faini ya kutoa mfugo mwingine.

-Mtu wa rika yako (mlietahiriwa pamoja) akikutembelea kwako kama ni usiku unamwachia nyumba (akiwemo mkeo) na wewe utatafuta pakulala. Hapo anaweza kufanya mapenzi na mkeo kama mke akiwa tayari ila haruhusiwi kumlazimisha.

-Ikiwa umeoa na labda ukasafiri na ikatokea mke umemuacha na akapata ujauzito kwa mtu wa rika yako huyo mtoto ni wakwako na ataitwa kwa jina lako na mke akijifungua lazima ufanye mila zote ikiwa ni pamoja na kumchinjia.
Pure Maasai tradition.
 
Mambo ya mila ,
Kwetu ukipata msiba wa mtu muhimu (hasa baba , mama, mwenza au mtoto mtu mzima) lazima unyoe kipara ni wote kwa mwanamke au mwanaume utavaa nguo ya rangi moja mara nyingi huwa naona nyeupe au nyeusi (hapa ukimpoteza baba au mama) kwa mwaka mzima na hutahudhuria sherehe yeyote kwa mwaka mzima yaan hata ukikutana na mtu unajua kabisa anaomboleza ! Kwa hii Generation Z sidhani japo bado kuna watu wanafanya haya mambo.

Hatufagii usiku na kama imekulazimu kufagia basi uchafu haumwagwi mpaka kesho asubuhi , Vyombo havipaswi kubaki na mabaki ya chakula kama havitaoshwa basi uchafu wote usafishwe uishe kabisa !!
Tandu akiingia ndani mkamuua kama ni usiku hampaswi kumtupa nje, hakuna kukata kucha usiku, Hupaswi kupiga mluzi usiku na mwanamke haruhusiwi kupiga mruzi kabisa !!
Huruhusiwi kula chakula kwa kupoza ile kama unapuliza ni ishara ya uroho subiri kipoe utakula .

Ukikuta mnyama amekufa njiani labda paka au mbwa hupaswi kumpita inabidi ukate jani hata moja tu umuwekee usipofanya hivyo ni mkosi !
Ni mengi ila wazazi walivyokua wanayakomalia sasa 😂
Siku moja nikiwa Musoma kulikuwa na mbwa kagongwa na gari barabarani. Basi kila mtu anayepita naona anang'oa majani na kumtupia yule mbwa. Nimeunganisha nukta wewe unatokea wapi mkuu 😀 😀 😀 😀
 
Kwetu ni mwiko kumla mbilikimo! Ama albino!!!..... Na vingine vya kufanana na hivyo(aliejichubua/ama emolo!) Kama wewe ni wa hivyo ... kwangu Pita hivi!.... Ama Tafuta ....utampata ...wa kufanana nawe!!!
 
- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu Pwani.

Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.

Kinyaa.
Yani katika tabia ninayo ichukia ndio hii sasa
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
Ni kabila gani?
 
Ahaa kwa hiyo ishu ni janaba na si manii tena? Maana tulikaririshwa kua shahawa zikimuingia mama mtoto zinaenda moja kwa moja hadi kwenye maziwa ya mama. Mtoto anaponyonya hunyonya maziwa yaliyochanganyika na shahawa hivyo kumfanya adumae.
Tunahitaji uzi wa hii kitu ili tupate ufafanuzi kutoka kwa wachangiaji.
 
1. Ni mwiko kuingia shamba la mtu la miwa au mahindi na kuvunja Kisha kuondoka nayo, inaruhusiwa kama ni miwa basi ikate kdhaa, kaa humohumo shambani kula Kisha uondoke au kama ni mahindi unaruhusiwa kuwasha moto kwenye hilo shamba Kisha kata mahindi yanayokutosheleza kula na kushiba Kisha choma kula maliza, zima moto na uondoke.

2. Mwiko kuhadithia hadithi mchana, utaota mkia.

3. Kwenye ukoo wetu kula utumbo wa mnyama yeyote mwenye miguu minne ni mwiko.

4. Ni mwiko Kupuliza moto kwa pamoja na ikitokea mmepuliza pamoja mmoja anatakiwa kutema mate juu na mwingine chini. Inaaminika msipofanya hivyo basi mtakuja kufa kwa siku moja.

5. Kuna mchezo mmoja tunauita 'buriburi' mnaketi chini kwa mzunguko kunakuwa na kimkaa au kijiwe unakificha kwa mikono nyuma na unaitoa mbele anayekufuatia anaonesha umekificha mkono gani, akipata unampa anaendelea yeye na anayemfuata hivyohivyo. Akikosa basi unakuwa ni ushindi na unaendelea kucheza. Sasa mkitaka kuanza kucheza ni lazima aanzishe mtu ambaye baba yake au mama yake alishatangulia mbele ya haki. Kama wote Wana wazazi basi mtoto wa mwisho kuzaliwa aliyepo hapo ndio huanzisha huo mchezo. Kwahiyo ni mwiko kwa mtu yeyote tu kuanzisha huo mchezo.

6. Kusonta kaburi na kidole ni mwiko.

7. Mwiko kulima usiku yaani jua likizama huruhusiwi kulima.

8. Kupanda mbegu shambani kwa kifaa chenye masizi ni mwiko, huashiria mbegu kutokuota maana ni kama unapanda mbegu zilizokaangwa.

9. Ni mwiko kumruka mtu, ikitokea inabidi urudi kwa kumruka kuelekea ulikotoka (kurudisha mruko [emoji4])

Ipo miiko mingi sana sana. Naweza Andika Kitabu.
Asante kwa nyongeza mkuu. Ila hizo namba 1, 4 na 5 zimenitisha. Na ikitokea mmiliki wa miwa au mahindi akakukuta kwenye shamba lake inakuaje? Anakupongeza au anakuchukulia hatua? Je, akikuchukulia hatua yeye atapata madhira gani?

Na hilo la kumvuka mtu naona lipo kariba kwenye makabila yote aisee!
 
Vingine na onyo tu hakuna laana wala mfano

huruhusiwi kukalia mafiga utaota majipu, kumbe saikolojia tu usiangukie kwenye moto au kuunguzwa na mafiga.

usikalie kinu, kumbe unawezama kwenye kinu ukabanwa uko.

usisimame mlangoni mizimu wakija watakuchukua, kumbe kuepusha msongamano.

usikate mti ovyo ni.mbaya, utunzaji wa mazingira.

Mtu kama amekukusoea akishika jani la isale akikuomba msamaha msamehe, kumbe kuepusha kesi za mda mrefu wakati mwingine ni ujinga unaweza tia katoto ka mtu dudu alafu unaomba yanaisha.
 
ukichinja mbuzi mwaga damu kidogo chini ili mizimu ya mababu nayo ishiriki

hurusiwi kuchinja mbuzi saa sita kamili mchana hadi ipite
 
huruhusiwi kuona uchi wa mzazi wako awe wa kiume au kike ni laana na unapofuka macho. Nashangaa kanda ya ziwa unaoga na dingi yako au maza ako
Kanda ya Ziwa ni kweli wanaoga sana na hakuna shida mkuu. Wala hakuna anayejali.
 
Kwetu mtoto wa kiume hatakiwi aungue kwa moto wa jikoni, akiungua hapati mwanamke 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom