1. Ni mwiko kuingia shamba la mtu la miwa au mahindi na kuvunja Kisha kuondoka nayo, inaruhusiwa kama ni miwa basi ikate kdhaa, kaa humohumo shambani kula Kisha uondoke au kama ni mahindi unaruhusiwa kuwasha moto kwenye hilo shamba Kisha kata mahindi yanayokutosheleza kula na kushiba Kisha choma kula maliza, zima moto na uondoke.
2. Mwiko kuhadithia hadithi mchana, utaota mkia.
3. Kwenye ukoo wetu kula utumbo wa mnyama yeyote mwenye miguu minne ni mwiko.
4. Ni mwiko Kupuliza moto kwa pamoja na ikitokea mmepuliza pamoja mmoja anatakiwa kutema mate juu na mwingine chini. Inaaminika msipofanya hivyo basi mtakuja kufa kwa siku moja.
5. Kuna mchezo mmoja tunauita 'buriburi' mnaketi chini kwa mzunguko kunakuwa na kimkaa au kijiwe unakificha kwa mikono nyuma na unaitoa mbele anayekufuatia anaonesha umekificha mkono gani, akipata unampa anaendelea yeye na anayemfuata hivyohivyo. Akikosa basi unakuwa ni ushindi na unaendelea kucheza. Sasa mkitaka kuanza kucheza ni lazima aanzishe mtu ambaye baba yake au mama yake alishatangulia mbele ya haki. Kama wote Wana wazazi basi mtoto wa mwisho kuzaliwa aliyepo hapo ndio huanzisha huo mchezo. Kwahiyo ni mwiko kwa mtu yeyote tu kuanzisha huo mchezo.
6. Kusonta kaburi na kidole ni mwiko.
7. Mwiko kulima usiku yaani jua likizama huruhusiwi kulima.
8. Kupanda mbegu shambani kwa kifaa chenye masizi ni mwiko, huashiria mbegu kutokuota maana ni kama unapanda mbegu zilizokaangwa.
9. Ni mwiko kumruka mtu, ikitokea inabidi urudi kwa kumruka kuelekea ulikotoka (kurudisha mruko [emoji4])
Ipo miiko mingi sana sana. Naweza Andika Kitabu.