Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Aisee moja ya Tabia ambazo sizipendi Duniani Ni moja wapo hiyo ndio maana siku hizi Mimi sisalimiani na watu kwa kushikana mikono ukija kunipa Mkono nakupa tano imeisha hiyo
Covid 19 imetuokoa na mengi
Nashukuru mpaka leo simpi mtu mkono tena labda namuheshimu sana Kama akileta wake la sivyo imetoka
Kukumbatia afadhali kama hamjaonana mda mrefu ila mkono hapana kwa kweli
 
Dah hii ya matanga ilikuwepo kwetu enzi hizo na ni pamoja na kutonyoa au kuchana nywele mpaka mwezi(matanga) yaishe.
Kwetu matanga yakiisha lazima kila mtu anyoe kipara....hii haina mjadala
 
Kwetu umasaini ni mwiko kumsalimia mtu mzima kwa mkono ni kichwa , kwetu hamruhusiwi kukaa karibu na watu wazima , sisi ni marufuku kuongea wakati mama anaongea , wakati wakula ni marufuku kuongea na kucheza cheza unatulia wakati wakula na mpaka watu wote wamalize kula ndio unaondoka . Nimarufuku kukiuka mila na desturi zetu
Lakini naona wakubwa ndio wanawashika wadogo vichwa
 
Kwetu ni :
1. Marufuku kulala kwa wakwe au shemeji
2. Ukienda kutembelea wazazi kijijini Marufuku kulala kwenu kama umeshaoa. Ndio maana kijijini kwetu kuna nyumba nyingi kama mjini.
3. Marufuku kumpa mgeni chakula au kinywaji bila wewe kuonja.
4. Marufuku kutosomesha au kutelekeza watoto hata kama ulizaa na chizi.
5. Mtoto akizaliwa ni lazima mzazi apongezwe awe wa nje ya ndoa au ndani. Mtoto ni baraka na ndugu lazima wapokee mgeni.

* wengine wataongezea tunaojuana washajua natokea wapi.
 
Umasaini au mila za kimasai kutema mate kwa mwenzio ni kawaida
Kwa mfano kama mnataka kusalimiana unatemea mate mkono ndio unampa mwenzio mkono hii ni moja ya heshima
Hii ni kwa marafiki
Pia wazee watawatemea watoto waliozaliwa kwenye paji la uso kuwapa Baraka

Na kina baba watawatemea watoto wao wa kike kichwani sio ya ndoa kuwapa Baraka na upendo
 
Umasaini au mila za kimasai kutema mate kwa mwenzio ni kawaida
Kwa mfano kama mnataka kusalimiana unatemea mate mkono ndio unampa mwenzio mkono hii ni moja ya heshima
Hii ni kwa marafiki
Pia wazee watawatemea watoto waliozaliwa kwenye paji la uso kuwapa Baraka

Na kina baba watawatemea watoto wao wa kike kichwani sio ya ndoa kuwapa Baraka na upendo
Enzi za korona hii tamaduni si watapukutika sana
 
Nimeipenda sana mada yako na huu uzi tukiutumia vizuri una fada kubwa sana kijamii.

Hili ni somo ambalo watu wanachukuwa mpaka PhD lipo kwenye "anthropology".
Mada inampinga mnyazi hii.
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
Kuishabikia CCM na kumuita Samia kuwa ni mama wakati ni mama wa Abdul.
 
Mambo ya mila ,
Kwetu ukipata msiba wa mtu muhimu (hasa baba , mama, mwenza au mtoto mtu mzima) lazima unyoe kipara ni wote kwa mwanamke au mwanaume utavaa nguo ya rangi moja mara nyingi huwa naona nyeupe au nyeusi (hapa ukimpoteza baba au mama) kwa mwaka mzima na hutahudhuria sherehe yeyote kwa mwaka mzima yaan hata ukikutana na mtu unajua kabisa anaomboleza ! Kwa hii Generation Z sidhani japo bado kuna watu wanafanya haya mambo.

Hatufagii usiku na kama imekulazimu kufagia basi uchafu haumwagwi mpaka kesho asubuhi , Vyombo havipaswi kubaki na mabaki ya chakula kama havitaoshwa basi uchafu wote usafishwe uishe kabisa !!
Tandu akiingia ndani mkamuua kama ni usiku hampaswi kumtupa nje, hakuna kukata kucha usiku, Hupaswi kupiga mluzi usiku na mwanamke haruhusiwi kupiga mruzi kabisa !!
Huruhusiwi kula chakula kwa kupoza ile kama unapuliza ni ishara ya uroho subiri kipoe utakula .

Ukikuta mnyama amekufa njiani labda paka au mbwa hupaswi kumpita inabidi ukate jani hata moja tu umuwekee usipofanya hivyo ni mkosi !
Ni mengi ila wazazi walivyokua wanayakomalia sasa 😂
Hii kama kwetu hivi 😅😅😅😅😅
Hapo kwenye kupiga mluzi hapo unaweza ukakatwa mdomo kabisa
 
Hii tuliifanyia utafiti wakati tupo shule lakini hatukufanikiwa. Hamna relationship kati ya mtoto anayenyonya na sperm za baba.
Ila kihalisia mtoto kudhoofu kupo. Na ukifatilia kwa nini hutopata jibu.
janaba sio zuri, mama na baba hawamharibu mtoto ispokua mkishatombana mkamalizakama mnaona uvivu kuoga msimruke mtoto kitandani, anabemendeka ikiwa wazaz halisi wa huyo mtoto mmoja wapo akizini bila kuoga janaba
 
Desturi ya nyumbani kwetu ukisonga ugali ukimaliza mwiko lazima uuoshe. Marufuku kuacha mwiko mchafu. Hata sijui ina maana gani ila nimekua nayo mpaka leo nikimaliza kusonga ugali lazima nioshe mwiko kabla hata chakula hakijafika mezani.
sufuria ni uke wako mwiko ni mboo, maana yake huwez ukatombwa ukamaliza bila kusafisha mboo ya bwana, hongera umeandalia vizur, speaking from my experience.
 
sio kw
Kwenye kabila letu:
1. Ni mwiko mwanamke aliyejifungua kula nyama ya kuku. Inasemekana akila kuku maziwa yatakuwa hayatoki.
2. Ni marufuku mjamzito kula mayai. Ikiwa atakula mayai, atamzaa mtoto kipara (asiyekuwa na nywele).
eli
 
Back
Top Bottom