Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Ni mwiko manamke aliyeolewa kurudi kwenu ukikimbia kaka zako wanakupa kipigo wanakurudisha kwa bwana ..japo nowdeizi utaandamwa na wanaharakati mpaka ufe kwa maneno
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
Ni mwiko mwanaume kuimba wakati anakula inaweza kusababisha akaolea mbali
 
Ni mwiko kula mnyama pori. Tunakula mbuzi, ng'ombe na kondoo tu hata kuku hatuli.

-Ni mwiko mwanamke kula maini na hata kijana kama mmechinja ukishaandaa maini ndio huanza kuliwa ila mpaka waanze wazee ndio wakupe go ahead na wewe ule. Ukionja maini hata kipande kidogo kabla ya wazee ujue hapo umekula mfugo wote na haitahesabika kama pamechinjwa kitu inabidi ulipe faini ya kutoa mfugo mwingine.

-Mtu wa rika yako (mlietahiriwa pamoja) akikutembelea kwako kama ni usiku unamwachia nyumba (akiwemo mkeo) na wewe utatafuta pakulala. Hapo anaweza kufanya mapenzi na mkeo kama mke akiwa tayari ila haruhusiwi kumlazimisha.

-Ikiwa umeoa na labda ukasafiri na ikatokea mke umemuacha na akapata ujauzito kwa mtu wa rika yako huyo mtoto ni wakwako na ataitwa kwa jina lako na mke akijifungua lazima ufanye mila zote ikiwa ni pamoja na kumchinjia.
 
Hii yakizamani kidogo (siku hizi haipo).

Mwanamke akifa watoto wake wa kiume wanampaka mafuta ya kondoo kisha anapelekwa porini chini ya mti wenye kivuli halafu anafunikwa na kipande cha ngozi usoni (ili tai wasile macho yake) kisha anaachwa hapo fisi wamtafune.
 
Mambo ya mila ,
Kwetu ukipata msiba wa mtu muhimu (hasa baba , mama, mwenza au mtoto mtu mzima) lazima unyoe kipara ni wote kwa mwanamke au mwanaume utavaa nguo ya rangi moja mara nyingi huwa naona nyeupe au nyeusi (hapa ukimpoteza baba au mama) kwa mwaka mzima na hutahudhuria sherehe yeyote kwa mwaka mzima yaan hata ukikutana na mtu unajua kabisa anaomboleza ! Kwa hii Generation Z sidhani japo bado kuna watu wanafanya haya mambo.

Hatufagii usiku na kama imekulazimu kufagia basi uchafu haumwagwi mpaka kesho asubuhi , Vyombo havipaswi kubaki na mabaki ya chakula kama havitaoshwa basi uchafu wote usafishwe uishe kabisa !!
Tandu akiingia ndani mkamuua kama ni usiku hampaswi kumtupa nje, hakuna kukata kucha usiku, Hupaswi kupiga mluzi usiku na mwanamke haruhusiwi kupiga mruzi kabisa !!
Huruhusiwi kula chakula kwa kupoza ile kama unapuliza ni ishara ya uroho subiri kipoe utakula .

Ukikuta mnyama amekufa njiani labda paka au mbwa hupaswi kumpita inabidi ukate jani hata moja tu umuwekee usipofanya hivyo ni mkosi !
Ni mengi ila wazazi walivyokua wanayakomalia sasa 😂
 
Kwenye kabila letu:
1. Ni mwiko mwanamke aliyejifungua kula nyama ya kuku. Inasemekana akila kuku maziwa yatakuwa hayatoki.
2. Ni marufuku mjamzito kula mayai. Ikiwa atakula mayai, atamzaa mtoto kipara (asiyekuwa na nywele).
Hii ni miiko kwa kabile letu pia
 
Kwetu umasaini ni mwiko kumsalimia mtu mzima kwa mkono ni kichwa , kwetu hamruhusiwi kukaa karibu na watu wazima , sisi ni marufuku kuongea wakati mama anaongea , wakati wakula ni marufuku kuongea na kucheza cheza unatulia wakati wakula na mpaka watu wote wamalize kula ndio unaondoka . Nimarufuku kukiuka mila na desturi zetu
 
Hiyo ya kumvuka mtu ipo na kwetu pia,

Kwetu huruhusiwi kulala kwenye kitanda shingoo ielekee kusini mwa kitanda bali ulale kaskazini mwa kitanda, mzungu wa nne kwetu ni marufuku.

Kwetu hurusiwi kushona nguo usiku.

Unapofiwa na mpendwa wako wote hamruhusiwi kuoga mpaka matanga yaishe kabisa.
Hiyo ya mwisho Ni noma sana
 
Kwetu umasaini ni mwiko kumsalimia mtu mzima kwa mkono ni kichwa , kwetu hamruhusiwi kukaa karibu na watu wazima , sisi ni marufuku kuongea wakati mama anaongea , wakati wakula ni marufuku kuongea na kucheza cheza unatulia wakati wakula na mpaka watu wote wamalize kula ndio unaondoka . Nimarufuku kukiuka mila na desturi zetu
Keiya nditoo
 
Hiyo ya kumvuka mtu ipo na kwetu pia,

Kwetu huruhusiwi kulala kwenye kitanda shingoo ielekee kusini mwa kitanda bali ulale kaskazini mwa kitanda, mzungu wa nne kwetu ni marufuku.

Kwetu hurusiwi kushona nguo usiku.

Unapofiwa na mpendwa wako wote hamruhusiwi kuoga mpaka matanga yaishe kabisa.
Dah hii ya matanga ilikuwepo kwetu enzi hizo na ni pamoja na kutonyoa au kuchana nywele mpaka mwezi(matanga) yaishe.
 
Back
Top Bottom