Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

kwetu

ukifagia usiku ndani usitupe matakataka nje yaache kwenye kona ya mlango utamwaga asbh

ukifagiwa uwanja hakikisha umezoa mataka unavyoacha kuku akayachakua ndio riziki yako itakavyokua utaikisanya usijue imeenda wapi

ni mwiko mjamzto kukaa kizingitini akiwa leba mtoto atakwama

mjamzito haruhusiwi kuchungulia nje akiwa ndani mtoto atakua anachungulia na kurud wakat wa kuzaliwa

siku ya harusi mume hupikia pishi maalum huitwa kombe, linakua kama n pilau chini kunawekwa kisosi na nyama tele ila ubwabwa wa moto sana sasa bwana harusi anatakiwa aingize mkono bila kutoa akitoe hiko kisos kupimwa urijali wake

mama yako akikusemea maneno ya kukulaani huyaondoa kwa kuchota maj kwenye kata kopo lenye mkono wa kushikia akiyaonda huku umempa mgongo ukiwa umesimama kizingitini kisha anakumwagia hayo maji mgongo tena ukitoka ukae nje dk kadhaa ndipo uingie inaaminika hiolaana ameivunja

ni mwiko kuvaa nusu uchi kwa mwanamke au msichana ambaye hajaolewa utavaa hivyo kwa mumeo

ni mwiko kusonga ugali ile sufuria ikawa inatoa sauti haitakiw
 
Impinge hata mnyaji.

Mradi sisi inatupa fursa kubwa sana ya kuonesha na kufundisha mila na desturi za Kisslam, tosha kabisa.
Muda wote unawaza kutoa vitu KWA njia ya haja kubwa jana ulisema ukiijua dunia utahara. Wakati sisi tunapambana kuijua dunia wewe unasema utahara ukiijua that's y mnapinga elimu.
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
Hii miiko ni ya kabila gani, boss
 
- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu Pwani.

Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.

Kinyaa.
Kwenu ni wapi?
 
Muda wote unawaza kutoa vitu KWA njia ya haja kubwa jana ulisema ukiijua dunia utahara. Wakati sisi tunapambana kuijua dunia wewe unasema utahara ukiijua that's y mnapinga elimu.
Kanisome tena. Usini "misquote".
 
kwetu

ukifagia usiku ndani usitupe matakataka nje yaache kwenye kona ya mlango utamwaga asbh

ukifagiwa uwanja hakikisha umezoa mataka unavyoacha kuku akayachakua ndio riziki yako itakavyokua utaikisanya usijue imeenda wapi

ni mwiko mjamzto kukaa kizingitini akiwa leba mtoto atakwama

mjamzito haruhusiwi kuchungulia nje akiwa ndani mtoto atakua anachungulia na kurud wakat wa kuzaliwa

siku ya harusi mume hupikia pishi maalum huitwa kombe, linakua kama n pilau chini kunawekwa kisosi na nyama tele ila ubwabwa wa moto sana sasa bwana harusi anatakiwa aingize mkono bila kutoa akitoe hiko kisos kupimwa urijali wake

mama yako akikusemea maneno ya kukulaani huyaondoa kwa kuchota maj kwenye kata kopo lenye mkono wa kushikia akiyaonda huku umempa mgongo ukiwa umesimama kizingitini kisha anakumwagia hayo maji mgongo tena ukitoka ukae nje dk kadhaa ndipo uingie inaaminika hiolaana ameivunja

ni mwiko kuvaa nusu uchi kwa mwanamke au msichana ambaye hajaolewa utavaa hivyo kwa mumeo

ni mwiko kusonga ugali ile sufuria ikawa inatoa sauti haitakiw
Hizi ndiyo mila za wakwere?
 
Ujinga upi huo?

Pwani ndipo ustaarabu ulipotokea.

Mjinga ni wewe, hata unavyoandika unaandika kijinga.
Kama mtoto wa miaka 13 akiwa haendi shule mnamfukuza nyumbani, mnataka aende wapi?

Jukumu la kumsomesha huyo mtoto ni lake au la mzazi?

Kama hamna uwezo wa kumsomesha huyo mtoto kwa nini mlimzaa?
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
Ukioa munyamahanga, it's your own risk.
 
Back
Top Bottom