Kabisa au sehemu hadhara'mgahawa au ymemaliza kula wengine bado wanaendelea ww unachojonoa meno ama unasukutua maji mdomoni..nakereka sana kuna wale hawakufunzwa kutafuna chakula wakiwa wamefumba mdomo unaweza dhani anafua kumbe anakula ni chwa chwa pwa chwa khaa
Kuna wengi sana hawana mafundisho ya maadili kutokea utotoni, nashukuru sisi wa shule za zamani na madrasa tulifunzwa mambo mengi ya kutokukahirisha watu.
Nakumbuka madrasa Ustadh wetu alikuwa na somo kabisa kila siku ya Jumatano mwenyewe akiliita "Kir'h", kwa maana "karaha".
Mengi sana madogo madogo ya kila siku tulifundishwa. Kwenye maadili ya kula tulifundishwa:
1) Tusinawe mikono kabla ya watu wazima.
2) Tusikae kula na watu wazima mpaka tukaribishwe.
3) tusijipitishe watu wanapokula.
4) tukinawa, tusikumute mikono mbele za watu, ikibidi kuikung'uta uebde pembeni kabisa.
5) hakuna kujamba kwa sauti au bila sauti wakati wa kula.
6) Namna ya kukohoa ukiwashwa koo wakati wa kula.
Dah mambo ni mengi sana tulifundishwa, yanayosaidia sana kuwa na tabia "natural" ambazo hazikirihishi wengine.
Sifahamu madrasa na shule za siku hizi kama wana wakati huo.
Shule tulikuwa na somo kabisa linaitwa "domestic science" moja ya mada zake ilikuwa ni "ethics". Hili kwa tuliosoma zamani, tulifundishwa na Mwalim Muhindi, simsahau anaitwa madam Jasmin, alikuwa kijana mtanashati enzi hizo. Alitunfundisha mema mengi sana tena sana.
Nikiwaelekeza vitu wajukuu zangu sasa hivi nilivyofundishwa "primary School" enzi hizo, wananiona mtu wa ajabu.