Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Kwetu mkishazaa hampaswi kusex mpaka mtoto apewe dawa gani sijui au mpaka msubiri aache kunyonya. La sivyo mtamharibu (kiswahili kubemenda). Hiyo ni mwiko nimetamani sana kufuatilia kwenye jamii nyingin3 bado sijapata jibu.
Hii tuliifanyia utafiti wakati tupo shule lakini hatukufanikiwa. Hamna relationship kati ya mtoto anayenyonya na sperm za baba.
Ila kihalisia mtoto kudhoofu kupo. Na ukifatilia kwa nini hutopata jibu.
 
Hii tuliifanyia utafiti wakati tupo shule lakini hatukufanikiwa. Hamna relationship kati ya mtoto anayenyonya na sperm za baba.
Ila kihalisia mtoto kudhoofu kupo. Na ukifatilia kwa nini hutopata jibu.
Kiislam, mwanamke akimaliza "nifas" (post-partum bleeding) anakoga, anajitoharisha anaanza kusali, kufunga na kuingiliana na mumewe., haina muda maalum, isipokuwa wengi huku kwetu huiita na kungoja siku "arubaini".
 
Hii tuliifanyia utafiti wakati tupo shule lakini hatukufanikiwa. Hamna relationship kati ya mtoto anayenyonya na sperm za baba.
Ila kihalisia mtoto kudhoofu kupo. Na ukifatilia kwa nini hutopata jibu.
Hii huwakuta jamii zingine kama waarabu,wazungu,wachina?
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
Duh naamini nitajifunza mengi kupita huu Uzi, japo fact zenu zngine znatisha kwakweli
 
Kwenye jamii yangu;

1.Mtoto harusiwi kupanda kwenye paa la nyumba ya wazazi wake.Ikitokea amependa Basi lazima hiyo nyumba ibomolewe ijengwe nyingine.

2.Bundi aktua kwenye mti uliopo kwenye boma Ni dalili mbaya hususan msiba.

3.Ni mwiko kuchanja kuni Usiku kwa kutumia shoka.

4.Ukizini na mke wa jamaa uliyetahiri naye siku Moja( kwetu tunaita bakoki) hutakiwi kwenda kumuona akiwa mgonjwa.Ukifanya hivyo lazima Atakufa.
 
Wakuria ukoo wa wakira.
1. Mwanamke haruhusiwi kupanda juu ya nyumba kuezeka. Hata kama mumewe alishafariki anatafuta wanaume wamuezekee.
2. Ni marufuku kukata au kuharibu mti wenye matunda ambao tayari umezaa matunda(una matunda kwa muda huo)
3. Kuwapiga wazazi laana yake sio ya dunia hii na haisafishiki hata kwa damu.
4. Ni marufuku mwanaume uliyeoa kulala upande wa ukutani. Hii Mara nyingi ni ikiwa kuna dharura basi usimvuke mkeo(familia) kwani huenda hutarudi salama.
5. Ukiwa umetengewa chakula na mkeo,Mara ghafla yowe,mwano au nduru kuashiria hatari kweny jamii basi innashauriwa uonje japo kidogo kutia suna.. Usiache chakula bila kukigusa....ni mkosi.
6. Mwanaume uliyeoa ni lazima uwe na silaha yoyote ndani sime au panga.
Kwa sasa ni hayo kutokea sirari border
 
Sidhani kama ni miiko kweli kwamba utapata mabalaa hapana.

Bali ni taratibu au malezi ya kumjengea mtu tabia nzuri tu naamini tukizifuata hizo basi ni wazi tutakuwa na jamii Bora sana.

Kuhusu Jogoo kuwika nje ya muda tuliouzoea ni dhahania tu, kwakuwa viumbe nao huwa wanaota ndoto kama ilivyo kwa binadamu.

Bundi ni Moja ya ndege wasiopendwa na jamii nyingi kwakuwa yeye mawindo yake huyafanya usiku kama ilivyo kwa baadhi ya viumbe,pia wanahusishwa zaidi na ushirikina, lakini ni ndege wa kawaida hata akilia karibu yako sidhani kama Kuna ishu yeyote.
 
- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu Pwani.

Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.

Kinyaa.
Daah kuna watu involuntarily ndio udhaifu wao huo na inatokea arbitrarily
 
Kutoosha vyombo usiku ni nuksi, mkipika chakula wakati wa kula jioni msimalize chote mbakize Kwa ajili ya mizimu yenu yaani wafu ndugu zenu wa familia, pia mwiko kupita ukimuona mtu wa jinsia tofauti au mtu mzima akiwa anakojoa kwenye njia, usimvuke mtu miguu yake
 
1. Kwetu ni mwiko kufagia jioni jua linapozama.
2. Vile vile kupiga mswaki baada ya saa sita ni mwiko.
3. Masharti ni mengi mno.
Hii ya kutofagia usiku hata kwetu ipo mkuu. Hebu taja nyingine zaidi watu wajifunze.

Kwetu mtu akiwa amelala chini usimvuke. Ukimvuka inasemekana hakuwi (harefuki). Ili ku undo au ku reverse hilo tatizo la kutokuwa, unatakiwa kumvuka kwa mara ya pili kuelekea upande uliomvukia.
 
Desturi ya nyumbani kwetu ukisonga ugali ukimaliza mwiko lazima uuoshe. Marufuku kuacha mwiko mchafu. Hata sijui ina maana gani ila nimekua nayo mpaka leo nikimaliza kusonga ugali lazima nioshe mwiko kabla hata chakula hakijafika mezani.
 
Back
Top Bottom