Taja sifa za wateja wako zinazofurahisha

Taja sifa za wateja wako zinazofurahisha

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
245
Reaction score
457
Kuna wateja ukiwaandikia bei yoyote hawajawahi kubisha. Wao huiitaji jumla tu walipie.

Wateja wengi vijana wenye hela hawapendezi sana. Wengi huvaa kawaida. Ukiona ameng'aa sana jua hamna hela.

Mabodaboda wakitumwa dukani, wao ni kulipia uwe umempiga bei au la!

Kuuzia wanawake wenye kipato cha chini huchosha sana kwani hupenda kudadisi kila bidhaa. Watauliza bei ya vitu kwa muda mrefu.

Kuna wateja wanazijua bei za soko zima hadi kero. Hawa huwapigi bei.
 
Mteja ambae hafai awe mwanamke halafu awe na shida shida...
 
Naomba picha na bei ya jumla ya vitu vyote unavyouza Ok nataka pc moja moja

Nimekutumia picha mbona haunijibu(hapo zimepita dakika 2)

Nakusubiri au siku ukiwepo niambie nije
 
Back
Top Bottom