Taja tabia yako/mazoea yako fulani hivi ambayo huyapendi na unasumbuka kuiacha/kuyaacha please don't be shy someone might give you a solution here

Fanya uiache,
 
Ni mimi kabisa aisee, muda wote nipo na furaha,sio kama najisifu ni hivyo nipo simple.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]mie huyo.
 
Nikiwa Niko idle au Brainstorming Niko na Tabia ya Kung'ata au kula Kucha mpaka Damu sometimes..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],kung'ata kucha nashukuru now nimeacha maana ilikuwa too much,
 
Mbona wengine tulikuwa tunamiandiko kuwazidi maticha[emoji23]

Lkn now tukiandika kama bata kapita,

Sema unaweza jirekebisha.
 
Nahisi Nina tabia mbaya sana

Huwa sipendi kupangiwa pangiwa mambo, wala kupingwa hoja zangu kiufipi nasimama na Ninacho kiamini

Hii tabia imenifanya niogope hata kuchangia hoja na Mara zote Hua na chagua kukaaa kimya

Hata Hua nikienda likizo kusalimia wazazi, unakuta nimepanga kukaa wiki 2, Naishia kukaa wiki 1 tu, sababu naogopa kubishana bishana na wazazi

Ilifika stage Wazazi ndugu na jamaa waliona nawadharau

Nimechagua kua niwe kimya tu
 
Bora wewe mkuu mimi kutongoza huwa siwez labda mwenyew uingie kwenye point zangu swala la kutongoza huwa naona kama naishusha value yangu
Pole sana mkuu. Hii hali inanisumbua sana.
 
Mimi kuvuta sigara chakula(Tungi).Nakerwa ila kuacha ngumu sana!
 
mimi bwana,nina penda pombe ya MNAZI,yaani ata kama nina pesa za bia naona bia kama maji tu,,,mimi mchaga lakini baada ya kuanza urafiki wa karibu na rafiki yangu patel wa pale kisutu,,,,niliupenda sana mnazi hasa tabia ya mnazi pale inapokuwa imetulia tumboni,tumbo linakuwa kama linajifinyajifinya hadi raha,,,,,,mimi naishi maeneo ya pugu mwakanga kwa ivo ikifika ijumaa tu naenda kwa ubanda wa mama semeni aua mama utajiju na kuana kulamba hiyo ki2,siku za kazi tunaenda na patel karibu na soko la kisutu pale karibu na ofisi ndogo ya ccm na gorofa la kizamani tunakaa sebuleni ka mama chupli{jina lake la utani huku tunaangalia filam za kidosi mpaka saa moja usiku nachukua bodaboda mpaka tazara then napanda mwakembe la kuelekea mpka mwakanga kuungana na waswahili wenzangu wa huko}''''''sasa tatizo linaanzia hapa,,,,ukinywa mnazi unaachia ushuzi sana na unatoka kwa muda mrefu so njia unazopita inatakiwa ziwe na vurugu au pilika iliukiachia ushuzi usisiskike kwa kweli tabia hii ya kuachia ushuzi inanikera sana ingawa kuacha mnazi ni ngumu,,,,,,ila tatizo litakalonilazimisha kuacha hii pombe nimabadiliko ya nywele,nywele zinakuwa kama sufi,,,huwezi amini mimi na patel nywele zinafanana kasoro mimi mweusi,,,,,kwa hii tabia ya nywele nauchukia mnazi!
 
Wewe ni mtu mwongo. Hiyo sio tabia ni dhambi.
 
Wakuu bado napambana nishinde hii tabia ya kuonea huruma wanawake. Ukiachilia mbali wapenzi wanaonipiga vizinga ila kuna hawa single maza huwa wakiniambia shida zao najikuta tu nimesaidia. Nimejitahidi kuwa mgumu lakini naona ni kama vile kitu kipo damuni. Au nifungue charity organisation?
 
Hasira, kwangu hili tatizo linanisumbua sana natamani kuwa mtulivu hata kwenye wakati mgumu ila nikishakuwa na hasira nakuwa mtu tofauti kabisa 😒
Mimi pia nina hasira ila nimebadili mfumo siku hizi.... badala ya kuwakiana na watu huwa navumilia na kuishia kuvunja mahusiano. Tangu mwaka 2020 nimepoteza watu wengi sana kwenye circle yangu ila namshukuru Mungu kuniletea watu wengine.
 
Mie dada wa kazi hata nimfokee hachukulii serious 🤣🤣🤣 Nikitaka nimseme serious hadi nialike watu wenye heshima zao🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…