Taja tabia yako ujue nani ana tabia kama yako

Nina tabia ya kipaka paka, Mama akipika nyama sichezi mbali na nyumbani.....akitoka tu kwenda bafuni, nadokoa nyama na kuchota unga kidogo kumpelekea demu wangu wa kitaa apike chakula tule then tucheze mchezo wa baba na Mama.
 
Mi tabia yangu nikijikuna kwapa lazima ninuse, hata kwenye public sijui nitaacha lini wakuu.
 
Hamna kitu sipendi kama dharau, kudharirisha na kudharirishwa. Huu mpka anayevuka yyte yule lazima tukosane mazima.
Nakumbuka zamani nilivyokuwa mdogo hata nikipigwa najikaza nisilie kwa sauti ili tuu watu wasisikie wasije niambia kuwa nilikuwa nalia.
 
Duh hata mi kipindi nipo 4m one nilikuwa kama wewe. Tuliomaliza primary, wote walichaguliwa shule tofauti na niliyoenda mimi hivyo nilikuwa mpweke sana lakini baadae (form 2) nikaanza kupata marafiki nikaanza kubadilika badae nikawa napendwa na darasa kwa ule upole wangu. Ilifika hatua teacher akija kutembeza mkong'oto class kutokana na kelele,wanadarasa walikuwa wanamwambia "teacher huyo unamuonea huwa hapigagi kelele,huwa anajisomea"[emoji2] [emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…