Mimi ni definition ya INTROVERT kabisa. Mkimya na kiukweli siko social kabisa. Marafiki sina wengi. Niko organised, napenda kila kitu kiwe mahali pake. Ninayo imani (ninaangalia vipindi vya dini na kusoma vitabu vya dini) ila ni mgumu sana masuala ya kwenda kwenye nyumba za ibada. Sipendi kupigiwa pigiwa kelele na watu fanya hiki fanya kile au makelele kwa ujumla, kwa kifupi nina msimamo na ninachoamini. Naweza nikaona unanipigia kelele, nikakwambia OK, nitafikiria ili tu uache kunipigia kelele, ukiondoka ndio imetoka. Sasa kuna baadhi ya wachache wananitafsiri kama nina kiburi kumbe wanashindwa kunielewa. Mimi ninawaelewa nao wanatakiwa wajaribu kunielewa. Napenda kuwapa watu space ila pia napenda nipewe space nami, alafu kuongezea nikipenda nina wivu sana.
Cha kushangaza sina hasira tofauti na watu wengi wanavyodai kuhusu watu wakimya.