Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Bila ya Salamu.
Huwa najiuliza nilichelewa wapi kujiunga na Simba Sc? Mpaka leo nikifikiria nakosa majibu.
Kifupi katika hiki kipindi cha wiki mbili nimeshuhudia chama langu jipya likifanya usajili wa kufuru. Magugu na mapandikizi yaliyokuwa yakihujumu timu yetu yametolewa na kuletwa vyuma vipya virudishe makali ya Simba.
Wahenga walisema Simba halali na njaa ila anaweza kuchelewa kula na hili nimeliamini kwa sajili za kimataifa zinazofanywa kimafia na Tajiri namba moja kijana Africa, namzungumzia si mwingine bali ni Trilionea Mohammed Dewji.
Leo hii ametangazwa beki wa kushoto ,mzaliwa wa mwaka 2000 (Kidume cha 2000) ,mchezaji wa timu ya Taifa ya Burkina Faso ,kinda mwenye miaka 24 , si mwinngine bali ni VALENTIN NOUMA.
Ni left back mwenye nguvu na kasi ya ajabu ya kupanda kushambulia na kuzuia huku akiwa ni specialist wa mipira iliyokufa , africa hakuna wa kumfananisha nae labda kwa karibu uwezo wake unafanana na kiungo wa westham united ,James Ward prowse. Simba sasa hivi licha ya kuwa itapata mabao mengi kutoka kwa viungo na washambuliaji wake bado pia itafaidika kwa magoli yatakayotokana na mipira iliyokufa (dead balls).
Bienvenu Valentin Nouma (aka Van NOMA)
Kazini kwa Tshabalala kuna Kazi.