Tajiri Zackaria Hans poppe amerejea rasmi Simba

Yote kwa yote YANGA bingwa

Hilo Wanasimba wote tunalijua labda awe tu Mwanasimba ' mwendawazimu ' ndiyo atalibishia. Labda tu nianze kuwa wa Kwanza kuwapeni ' Kongole / Pongezi ' zangu za dhati kabisa wana Yanga FC wote mliopo humu JF kwa Kesho kuchukua tena ' Ubingwa ' wa VPL na safari hii mkiwa mmeweka nadhani rekodi ya ' Kipekee ' kabisa ya kulichukua Kombe kwa mara ya Tatu mfululizo na sasa linaenda kuwa ' Mali ' yenu pale Jangwani. Hongereni sana ila jitahidi sasa muijenge Timu yenu iwe ya ' Ushindani ' zaidi hasa Kimataifa na mfike mbali ili muweze kuwauza Wachezaji wenu na kuitangaza pia Tanzania huko Kimataifa.

Wanasimba wenzangu Mimi sijazoea ' Unafiki ' na sifa kuu huwa ni ' kunyoosha ' na kuwa ' mkweli ' daima. Ubingwa huu wa VPL tumeukosa wala siyo kwa sababu sijui za TFF au Referees bali tumeukosa kwa ' upuuzi ' wa Watu wawili tu Rais Aveva na Makamu wake Kaburu hasa kwa ' Kuendekeza ' Makundi yao ndani ya Klabu hali ambayo kuna wakati ilipelekea Wachezaji wetu nao ' kugawanyika ' na kuweza kucheza chini ya Viwango vyao kwa ' amri ' za hawa Viongozi wawili kitu ambacho kilituathiri mno katika mechi zatu mbili za mzunguko wa Kwanza na mechi zetu tatu za mzunguko huu wa pili unaoenda kumalizika Weekend hii.

Tunachotakiwa kukifanya tu sasa ni kuiombea Timu yetu angalau iifunge Mbao FC katika Fainali ya ASFC ili nasi tucheze Shirikisho ambapo kama tutafanya vizuri na tukiwa na Kikosi kizuri basi Simba SC inaweza hata ' kupenya ' na kuingia Makundi ya Champions League na pengine hata kuweza kukutana na ' Mahasimu ' wetu Yanga FC na kwa pamoja tukaipeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa hali ambayo itawapa ' exposure ' kubwa Wachezaji wetu na hata kununuliwa na Vilabu vya nje ili hatimae mwishoni Tanzania iwe na Kikosi imara katika Timu yetu ya Taifa ( Taifa Stars )

Yanga FC hongereni sana na pongezi zenu nyingi kwani nina uhakika 100% iwe mvua au jua Kesho pale Taifa ' mnatawazwa ' tena kuwa ' Machampioni ' wa VPL. Na niwaombe tu Kiungwana kabisa Wanasimba wenzangu popote pale mtakapokuwa kuwa Kesho Yanga FC ikishatawazwa tu kuwa ' Mabingwa ' mfuatae ' Mshabiki ' yoyote yule wa Yanga FC unayemjua na mwambie tu Kiuanamichezo kuwa Hongera na Pongezi kubwa kwa kuwa Mabingwa tena bila hata ya kuchukia kwani hakuna ubishi na tuweke ' ushabiki ' maandazi wetu pembeni Yanga FC kwa aina ya Kikosi chao na wanavyojua ' Kujipanga ' walistahili na wanastahili kuwa ' Mabingwa ' wa VPL.
 
Hivi hii ni mara ya ngapi kwa yeye kutishia kujiuzuru, halafu anabembelezwa na wanachama abatirishe uhamuzi wake - hii inaleta taswira gani kwenye klabu ya simba - kuna tatizo gani hasa?
 
Nyie mabwege kweli,hivi kunamijitu na mbupu zao bado yanashabikia Mpira Wa bongo kweli??
 
Nyie mabwege kweli,hivi kunamijitu na mbupu zao bado yanashabikia Mpira Wa bongo kweli??

Nadhani ID yako ungejiita ' Doggy ' ingekupendeza mno kwani hata hata uliyoyaandika hapa unaweza kuyapata sana katika ' Ubongo ' wa Mbwa aliyetukuka.
 
Hapo ndio munapoharibu watani uchawi na hirizi havina nafasi kwenye dunia ya sayansi na teknologia Jiongeze mtani au m utaendelea kuusikia ubingwa kwenye redio tu
 
Hans Poppe alitaka kumpindua Julius Nyerere....akafungwa Kwa miaka karibu 12....akaachiwa baada ya muundo wa vyama vingi
 

mkuu wakikupa majibu ya haya maswali unitag.
 

Mkuu kwa kumwaga povu hujambo, miaka mnne na mbwembwe zile za kumtoa Aden mkijiona ndio muarobaini wapi kiongozi, mmebaki mapovu mara table tennis, oooooh mara fulani wetu, ni wakati muafaka bado hamjachelewa nendeni mkamuombe radhi Aden, laana itawatafuna
 
Inaonyesha jinsi gani hawastahiri kuwa mabingwa, viongozi hawana misimamo. Watasubiri sana.
 
Kafanya maamuzi kama ya bwana yule le bashite professeri 'wanachama wakikuomba urudi shurti utii' in le profeseri's voice
 

Hans-Lipumba
 
Povu tupu, tena la OMO
 
Who told you I am a real intellectual? Who told you you are an intellectual?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…