GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #61
Yote kwa yote YANGA bingwa
Hilo Wanasimba wote tunalijua labda awe tu Mwanasimba ' mwendawazimu ' ndiyo atalibishia. Labda tu nianze kuwa wa Kwanza kuwapeni ' Kongole / Pongezi ' zangu za dhati kabisa wana Yanga FC wote mliopo humu JF kwa Kesho kuchukua tena ' Ubingwa ' wa VPL na safari hii mkiwa mmeweka nadhani rekodi ya ' Kipekee ' kabisa ya kulichukua Kombe kwa mara ya Tatu mfululizo na sasa linaenda kuwa ' Mali ' yenu pale Jangwani. Hongereni sana ila jitahidi sasa muijenge Timu yenu iwe ya ' Ushindani ' zaidi hasa Kimataifa na mfike mbali ili muweze kuwauza Wachezaji wenu na kuitangaza pia Tanzania huko Kimataifa.
Wanasimba wenzangu Mimi sijazoea ' Unafiki ' na sifa kuu huwa ni ' kunyoosha ' na kuwa ' mkweli ' daima. Ubingwa huu wa VPL tumeukosa wala siyo kwa sababu sijui za TFF au Referees bali tumeukosa kwa ' upuuzi ' wa Watu wawili tu Rais Aveva na Makamu wake Kaburu hasa kwa ' Kuendekeza ' Makundi yao ndani ya Klabu hali ambayo kuna wakati ilipelekea Wachezaji wetu nao ' kugawanyika ' na kuweza kucheza chini ya Viwango vyao kwa ' amri ' za hawa Viongozi wawili kitu ambacho kilituathiri mno katika mechi zatu mbili za mzunguko wa Kwanza na mechi zetu tatu za mzunguko huu wa pili unaoenda kumalizika Weekend hii.
Tunachotakiwa kukifanya tu sasa ni kuiombea Timu yetu angalau iifunge Mbao FC katika Fainali ya ASFC ili nasi tucheze Shirikisho ambapo kama tutafanya vizuri na tukiwa na Kikosi kizuri basi Simba SC inaweza hata ' kupenya ' na kuingia Makundi ya Champions League na pengine hata kuweza kukutana na ' Mahasimu ' wetu Yanga FC na kwa pamoja tukaipeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa hali ambayo itawapa ' exposure ' kubwa Wachezaji wetu na hata kununuliwa na Vilabu vya nje ili hatimae mwishoni Tanzania iwe na Kikosi imara katika Timu yetu ya Taifa ( Taifa Stars )
Yanga FC hongereni sana na pongezi zenu nyingi kwani nina uhakika 100% iwe mvua au jua Kesho pale Taifa ' mnatawazwa ' tena kuwa ' Machampioni ' wa VPL. Na niwaombe tu Kiungwana kabisa Wanasimba wenzangu popote pale mtakapokuwa kuwa Kesho Yanga FC ikishatawazwa tu kuwa ' Mabingwa ' mfuatae ' Mshabiki ' yoyote yule wa Yanga FC unayemjua na mwambie tu Kiuanamichezo kuwa Hongera na Pongezi kubwa kwa kuwa Mabingwa tena bila hata ya kuchukia kwani hakuna ubishi na tuweke ' ushabiki ' maandazi wetu pembeni Yanga FC kwa aina ya Kikosi chao na wanavyojua ' Kujipanga ' walistahili na wanastahili kuwa ' Mabingwa ' wa VPL.