Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

Tanzania ya Viwanda.....
Mkuu asante kwa maelezo mazuri kwa wale wanaoogopa kufuga nyoka naona kuna fursa ya ku-supply panya kwenye hilo shamba lako.

Nina maswali machache
1.unao wangapi kwa sasa?
2.uvunaji wa sumu unatumia vifaa gani?
3.vipi namna ya kuhifadhi hiyo sumu?
4.bila shaka unafuga nyoka wa aina tofauti je bei ya sumu inategemeana na aina ya nyoka au wote bei ni moja?
5.vipi kuhusu soko wanunuzi wanaifuata au unawapelekea mwenyewe?
Bei ya sumu hutofautiana kulingana na nyoka.mfano

1.Gram ya puff adder venom ni $202

2.Boomslang bei yake ipo juu kuliko nyoka yeyote yule $4800

3.koboko $500

Hivyo bei ya venom hutofautiana na aina ya nyoka,sasa kazi ni wewe kupata license na kuchagua aina ya nyoka unaowahitaji au kuona watakuletea faida kubwa.

Aidha kuhusu namna ya kutoa sumu ,nyoka hukamatwa kwa ustadi kupitia kifaa special ,fimbo special yenye kibanio na pia nyingine iliyochepuka ambayo husaidia kumbana nyoka shingoni karibu na kichwa ,ukishamkamata nyoka kichwa hatua inayofuata ni kutafuta chombo special cha kuwekea sumu hiyo.mfano umechukua bakuli dogo,au chombo chochote kile unafunga plastic juu yake kama vile mfuniko huku ukiwa umemshika nyoka kichwa na wakati huo mdomo wa nyoka utakuwa wazi usiokuwa na madhara kwako wewe kisha unamuinamisha kwenye chombo husika na fangs za nyoka zitagonga au kuchoma plastic uliyoiweka juu na kumwaga sumu ndani,njia zipo nyingi tu

7fe9c3c06341be68dccedbc5f45c75cc.jpg


6e08da4c7e8100704275964a04cb6520.jpg


Soko ya venom ipo USA ,India ,China ,S.Africa

Lakini wengi hupeleka China sababu huko wengi ndio wanahitaji kwa wingi.

Unapeleka na ufuate utaratibu na sheria mfano December 2016 India waliwakamata smugglers 5 waliokuwa na venom yenye thamani ya $30Million ,walikuwa wanasafirisha kimagendo na walikuwa wanawauzia druglords ambao pia hutumia venom kutengenezea drugs


e5b5e46b4f1318fcd1d37e820a234026.jpg
 
mkuu ninapoishi wapo wengi hadi natamani lukimbia mji.Kwakunisaidia weka kapicha jinsi unavyo wahudumia
 
Back
Top Bottom