Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

Watu awamu ya tano imewavuruga vya kutosha, soon mtaanza kufuga majini ya kuuza
 
Mhmm kumbe uongozi wa magufuli utapelekea kweli watu kuwa wabunifu tutafupa mpaka siafu mwaka huu
Hahahaaaaa naomba mkuru akaze Kabisa kamba watu tuanzishe hadi kilimo cha kunguni
 
Max kuanzisha jf unatuletea balaa, samahani mleta mada wenzio tupo kwa anko magu we baki hukohuko china kwa hu ji ntao
 
Safi sana, kwa hii rangi tutafahamu mambo mengi mazuri yatakayo tupa jina katika nyanja mbali mbali
 
Mkuu mbona hujatutajia pia HASARA ya kufuga nyoka? Hasara kubwa ya kufuga nyoka ni kwamba nyoka mwenye sumu anaweza kukugonga wewe mmiliki, shamba boy wa shamba lako nyoka au mtu yeyote atakayekutana naye (mtoto wako, mama yako, mke/mume wako, nk) na kupoteza maisha ndani ya dakika 5 tu hata kabla hujapatiwa huduma ya kwanza au kufikishwa hospitalini. Kwa hiyo, nyoka ni kiumbe hatari sana...ukimuona popote muue na kumtupia mbali kabisa.
 
View attachment 502154
Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana.Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake.
View attachment 502152
Gram moja ya "snake venom " kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000

*Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka

1.zingatia hali ya joto na hewa .
View attachment 502150
Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku,

2.mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara

Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi.Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata.

3.Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 .Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai.


Faida 3 za ufugaji wa nyoka

1.uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa.

2.hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu kama panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa.

Dawa ya kuua sumu ya nyoka itengenezwayo kutoka kwa sumu ya nyoka, yaani anti-venom, ndiyo tiba bora pekee ya kuumwa na nyoka.
View attachment 502151
**Mwisho nawashauri ndugu zangu sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui.Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana.




mkuu nimekua nikipata mafunzo mbali mbali juu yA hii mifugo at the end of this year nitakua mekamilisha taratibu zote na mifugo itakua mabandani
 
Huu mradi ni mtihani. Ni kama kumkamua simba wa porini maziwa
 
Ahsante kwa wazo la fursa lakini HAPANA!! Si kheri ungeniambia nifuge akina Faru John... nyoka?! Hapana aisee!!!!

Navuta picha siku limetokea janga lolote lile kisha nyoka wote haoooooo; nje ya banda!!!!
 
Kama naanza kukuelewa, nimegundua hata tatizo la mboga nyumbani litaisha!
 
Uzi wa kipekee kbs huu..
Dondoo ulizotoa ni nzuri na zinatia Hamasa ya kufanya hki kilimo..
Sema Hujasema pengine mtaji wa Kuanzia ni km kiasi gani hv?..
Na Hli suala linahitaji UJASIRI SIO KIDOGO, Ukizingatia wengi hatujakuzwa ktk mazingira ya kuwachukulia nyoka km RAFIKI na sio MAADUI
hvyo akili zishakua nA hali ya TAHARUKI juu ya hawa VIUMBE
Na yapaswa kufunDishwa kabisa kwa muDa Mrefu sio kitoto
[HASHTAG]#Thanx[/HASHTAG]
 
Mie babu yangu anafugaga majini mpaka sasa yanafika majini 7860 je tunaweza kupata mteja tufanye nae biashara?
 
Back
Top Bottom