joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Hili ni jambo la kusikitisha na kufedhehesha sana. Kenya ilishindwa kuwakamata na kuwashitaki watu waliohusika katika vurugu za kikabila za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017, ambapo maelfu ya watu waliuliwa kinyama hadi ndani ya makanisa, badala yake serikali ya Jubilee ilitumia pesa nyingi kuwatetea UHURUTO ikiwemo kuwauwa wote waliokuwa tayari kutoa ushahidi dhidi yao.
Kama hiyo haitoshi, hadi Leo makundi makubwa ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na vurugu hizo, bado wanaishi katika kambi za wakimbizi wa ndani na nje ya nchi(Uganda) bila msaada wowote, huku mabilioni ya pesa yakiibiwa na zingine kutumika kujenga miradi isiyokua na faida yoyote kwa wananchi, hii inathibitisha Maneno ya mwalimu Nyerere aliposema Kenya ni "Man eat man society". Kenya masikini na mwananchi wa chini hathaminiki kabisa.