Takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye kutafuta hata shughuli, yaani yupo tu

Takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye kutafuta hata shughuli, yaani yupo tu

Nikiwa kama kichwa cha familia, nyumbani kwangu ni sheria zangu, na linapokuja swala la sheria kwa wageni huwa zimekazwa mno kwa wageni wa kiume ambao ni miaka 28+ maaana hawa tayari ni wanauume na asili yetu ni kupambana ili kujitegemea......changamoto za kimaisha na harakati za kiupambanaji wakati mwingine zinapelekea kujikwaa lakini ni mwiko kukata tamaa kusimama kwenye asili yetu huku mipango na malengo vinabakia vichwani mwetu.
Umekurupuka mzee Kuna sababu nyingi na Hali nyingi.... Ushawahi jiuliza Kama ni mfanya kazi yupo kikazi mikoani huko vijijini kaamua kuomba likizo ili aje apunge hewa huko unako ishi Kama ni mjini lkn Sasa hapo kosa lake Nini......?

Au Kama ni mkulima kalima zake huko kamaliza kulima Hadi kavuna Sasa mazao yapo ghalani na huko bush watu wakisha vuna ndio wanaingia likizo na kutafuta sehemu za kwenda kupata upepo na wengi wao wanakimbilia dar kusubiri msimu mwingine wa kilimo Sasa hapo kosa lake Nini......?

Au viugali anavyo kula hapo vinakuuma .....?
 
Nikiwa kama kichwa cha familia, nyumbani kwangu ni sheria zangu, na linapokuja swala la sheria kwa wageni huwa zimekazwa mno kwa wageni wa kiume ambao ni miaka 28+ maaana hawa tayari ni wanauume na asili yetu ni kupambana ili kujitegemea......changamoto za kimaisha na harakati za kiupambanaji wakati mwingine zinapelekea kujikwaa lakini ni mwiko kukata tamaa kusimama kwenye asili yetu huku mipango na malengo vinabakia vichwani mwetu.

Ni takribani wiki 2 zilizopitata nilipata ugeni wa kaka yake mke wangu mwenye miaka 33

Alifika mida ya saa 2 bila taarifa na niwe muwazi kwamba hata mgao wa chakula ulivurugika, namjali sana house girl wangu namchukilia kama mwanafamilia na wife alikuwa kapata ugeni, hivyo ilibidi niende kula mgahawani.

Usiku ule ule tukiwa chumbani nilikuwa namhoji wife kwanini ndugu yake kaja bila taarifa ila nikapotezea nikijua labda atakaa siku 2 au 3.

Kuna vyumba vya wageni vimejitenga na nyumba kuu ndiko tulipompa hifadhi, na choo / bafu ni humo humo.

Sasa ni takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye akitafuta hata shughuli, yani yupo tu.

Wife akimuuliza hali, yeye anasema kaja kutusalimia huwa nabaki kukuna kichwa tu

Asili ya sisi wanauume ni kujitegemea......changamoto za kimaisha na harakati za kiupambanaji wakati mwingine zinapelekea kujikwaa lakini ni mwiko kukata tamaa kusimama kwenye asili yetu huku mipango na malengo vinabakia vichwani mwetu

sasa navyomoona mwanaume mwenzangu yupo comfortable na hali ya kuwa tegemezi na hana tatizo lolote la kumfanya asishughulike, binafsi najisikia vibaya.
Duuh
 
Cha Kwanza tafuta uhakika kuwa ni shemeji yako wa kweli ama umehifadhi x WA mkeo 😂😂😂
Pili ongea nae kiuchunguzi kama ni shemeji yako je, atokako ni heri? Maana ujio wa ghafla bila taarifa ni kama mtu amekimbia tukio.

Ikiwa ni mtu amekuja kwa amani na ni mtu mwema ok,mtoe out ongea nae kiume, usikie ratiba zake kama anaonekana hana mipango yoyote ya kuondoka sawa,mtumie kwa faida yako
Inategemea uko wapi unaweza mfyatulisha matofali na kuchoma then kuyauza, ama kwa mjini kanunue viatu vya mtumba mpe akauze aakazungushe, kwa kutembeza ama kumwaga chino mahali fulani,kuanzia Mchana mpk saa 4 usiku
Kama akikomaa miezi sita mtafutie chumba mlipie kianzio
 
Back
Top Bottom