TAKUKURU haiwezi na haina mamlaka ya kubambikizia mtu kesi

Unachekesha kweikwei wewe! Kwani kuna sheria iliyokuwa inafuatwa wakati wa serikali ya Jiwe?! Si ni matamko na kubambika kesi basi! Lakini watu wengi wameteseka hivyo hivyo! Na ndio hizo zilizofutwa, mimi ni mhanga wa kesi za aina hiyo!

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Hizo kesi 147 nimeuliza ziko mahakama ipi, nitajie walau moja tu.
Mtu anaweza kuambiwa kachukua rushwa na anachunguzwa na takukuru na yuko mahabusu bado upelelezi unaendelea, ukikamilika file linaenda kwa DPP ili ipelekwe mahakamani
 
Ndiyo nataka mnisaidie ni kama ipi. Mnasema kuna kesi za nama hiyo kumbe hata moja hamuwezi kuitaja.

Watu wa ajabu kweli nyinyi.

Mtu anaweza kuambiwa kachukua rushwa na anachunguzwa na takukuru na yuko mahabusu bado upelelezi unaendelea, ukikamilika file linaenda kwa DPP ili ipelekwe mahakamani
 
Afadhali wewe naweza kukuelewa kwamba kuna watu waliwekwa huko bila kufuata sheria yoyote japo hunitajii jina la hata mmoja kati ya hao 147.

 
Someni upya
 
Kesi ya ruge na seth ni ngumu,ile chanzo chake ni tume ya bunge
 
Unaongelea sheria kwenye utawala wa dicteta jiwe?
 
Ndiyo maana wanajeshi wakaenda kununua korosho?Hiyo ndiyo kazi yao kweli au kuvamia maduka ya fedha Arusha?
 
Ndiyo nataka mnisaidie ni kama ipi. Mnasema kuna kesi za nama hiyo kumbe hata moja hamuwezi kuitaja.

Watu wa ajabu kweli nyinyi.
Serikali haijazitangaza moja moja imetoa inform of list kuwa zipo 147 Sasa tuzijue ili iweje kwani kesi zote uwa tunaambiwa zinapofunguliwa....hili swali ulitakiwa ulielekeze kwa waziri,mkurugenzi wa takukuru na wote waliopo kwene mfumo wa takukuru wa zilisti sisi tumetajiwa kwa idadi na ni kawaida kwa serikali
 
Mkuu hili swali lingeelekezwa direct kwene mamlaka husika Kama unataka kuzijua kwa tittle hizo kesi maana ni wazi unajua kabisa serikali imezitangaza kwa idadi na sio kwa listing....na tumepokea taarifa ya serikali Kama ilivo
 
Political pressure? Incompetence? What was the reason behind the cases?
 
Hivi unajua mtu anapokamatwa na rushwa, kuna kuwa na mashahidi wangapi wanaokuwepo eneo LA tukio?sasa hapo mtu anabambikiwaje kesi? Yaani ukamatwe kwa rushwa, wachukuliwe mashahidi walioshuhudia zile Pesa ulizokamatwa nazo, zikaguliwe namba, wao wakiona... Wapelekwe wahojiwe watoe maelezo... Then Uje useme umebambikiziwa kesi?

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Ndio hivyo ndugu yangu awam iliyopita walikuwa wanalazimisha kukushikisha rushwa kwa nguvu au kukurushiwa rushwa kwenye gari ilimradi wakubambike kesi ili wapate sifa mbele ya mwendazake!!! Mie nimeshuhudia hayo kwa macho yangu mara hii lakini waliofanyiwa hivyo mahakamani walishinda
 
Na takokukuru wenyewe wanavyopenda media sasa utawaona kila siku mbere ya kamera mara tumekamata huyu,mara yule,mara tumepeleka mahakamani kumbe uongo tu kubambikizia watu kesi
 

Mama Rais wa JMT kasema wamefuta kesi 147 za kubambikia.

Hivi mnatudhania sisi ni mazwazwa eeh?
 
Kwahiyo unashindana na TAKUKURU wenyewe waliosema hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…