TAKUKURU: Kwenye TFF kuna hela zimetumika vibaya

TAKUKURU: Kwenye TFF kuna hela zimetumika vibaya

Una maana mchimba kaburi ni magu kupitia takukurupuka😀
Kama ndivyo bora tu aingiemo😀😁😁
Mchimba kaburi ni Wallace Karia aliyewahujumu akina Jamal Malinz na Michael Wamburai ili apate kuwa Mwenyekiti wa TFF.
 
Ila nchi imeoza hii, kila mtu wa kitengo anawaza kutafuna tafuna tu.
 
Hope hao TAKUKURU wanajua masuala ya football huwa hayapelekwi mahakama za kawaida, ndio maana wanawaambia direct warudishe hizo fedha.

Wakijichanganya tutafungiwa na wenye mpira wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ni wazi tu utakwenda Mahakamani kwa sheria za nchi. Kinachokatazwa kwenda Mahakamani ni kama mambo ya rufaa za usajili, maamuzi ya refa, uhamisho wa wachezaji etc.

Kumbuka namna Sepp Blatter na Michel Platini namna Serikali ya Switzerland ilipoingilia kati na kuwasambaratisha
 
Wallace Karia alitumia hila mbaya sana kupata kuwa Rais wa TF. Alitumia nguvu za Serikali kupitia Mkurugenzi wa Mchezo ambaye ni Katibu wa BMT kuhakikisha kuwa wakati wa uchaguzi wa TFF May 2017, Jamal Malinzi anakuwa rumande kwa mashtaka yasiyo na dhamana. Kweli Jamal Malinzi alikamatwa akudunguliwa mashtaka ya kutakatisha fedha (AML).

Kwenye uchaguzi Karia akapita dhidi ya ushindani hafifu. Pia na Michael Wambura naye anashinda kama Makamu wake. Baada ya miezi 6 Karia akamuengua Wambura aliyechaguliwa kihalali kama Makamu wa Rais wa TFF. Hatimaye naye Wambura akaanza kutafuta haki yake kwa kupitia mifumo ya ndani ya TFF na BMT lakini akashindwa. Wambura anaamua kwenda Mahakamani ambako suala lilikuwa lina dalili zote kuwa angeshinda.

Karia alamuwahi kwa kumpeleka TAKUKURU na kifunguliwa mashtaka ya kutakatisha fedha pia. Kiufupi wote Wambura na Malinzi wako huru kwa namna tofauti ila ukweli ni kwamba Wllace KARIA aliwabambikizia zile kashfa ili apate ile nafasi aje kufanya UFISADI bila kudhibitiwa.

Ngoja tusubiri nini kitajiri kutoka TAKUKURU
 
Mkuu ile ilikuwa michuano ya under 17, na Tanzania ndo imeandaa,kuhost michuano kama hiyo africa only come once ,so kupewa hela ya kuweka maandalizi si kitu kibaya.
Huwa najiuliza mbona sijawahi kusikia viongozi wa vyama vingine vya michezo wakituhumiwa ulaji pesa? Je, ni wasafi Sana? Kwanini mpira wa miguu tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanamtaja taja Bashite kuwa nae katia mkono hapo anahusikaje??
 
Back
Top Bottom