Wallace Karia alitumia hila mbaya sana kupata kuwa Rais wa TF. Alitumia nguvu za Serikali kupitia Mkurugenzi wa Mchezo ambaye ni Katibu wa BMT kuhakikisha kuwa wakati wa uchaguzi wa TFF May 2017, Jamal Malinzi anakuwa rumande kwa mashtaka yasiyo na dhamana. Kweli Jamal Malinzi alikamatwa akudunguliwa mashtaka ya kutakatisha fedha (AML).
Kwenye uchaguzi Karia akapita dhidi ya ushindani hafifu. Pia na Michael Wambura naye anashinda kama Makamu wake. Baada ya miezi 6 Karia akamuengua Wambura aliyechaguliwa kihalali kama Makamu wa Rais wa TFF. Hatimaye naye Wambura akaanza kutafuta haki yake kwa kupitia mifumo ya ndani ya TFF na BMT lakini akashindwa. Wambura anaamua kwenda Mahakamani ambako suala lilikuwa lina dalili zote kuwa angeshinda.
Karia alamuwahi kwa kumpeleka TAKUKURU na kifunguliwa mashtaka ya kutakatisha fedha pia. Kiufupi wote Wambura na Malinzi wako huru kwa namna tofauti ila ukweli ni kwamba Wllace KARIA aliwabambikizia zile kashfa ili apate ile nafasi aje kufanya UFISADI bila kudhibitiwa.
Ngoja tusubiri nini kitajiri kutoka TAKUKURU