DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
2. Mradi wa mwendokasi Mbagala.
Huu mradi nendeni mchunguze, ni mbovu na umejengwa chini ya viwango vibaya mno.
Hawa jamaa wanaitwa SINOHYDRO ni Wala rushwa balaaa, Sasa viongozi wengi Sana wakifika wanapewa Chao wanaishia kupiga mkwara fake na kuondoka, mnakumbuka Yule DC Gondwe? Alienda akapiga mkwara Yule mbongo akawa anacheka TU?

Ujenzi wowote nchini ulio chini ya SINOHYDRO au STECOL (NDIO Huyo huyo SINOHYDRO) ni mibovu balaaa na hawajawahi kumaliza on time.

Wana kashfa za kuwanyanyasa wafanyakazi Sana na wale jamaa wa TAMICO hawana Cha kufanya.

Huu mradi wa BRT waliwahi kupata kashfa ya kutumia lami ambayo source yake ilikua nchi ambayo imewekewa vikwazo.

Na NDIO hawa hawa wamepewa SGR bila kutumia utaratibu wa manunuzi, yaani single source, Kuna siku Tanzania itaomboleza wallah.
 
Kwa hali hii ambayo nchi inapitia, uongozi mbovu, rushwa, ubinafsi, ufisadi, nepotism na vetting mbovu, uonevu nk tatizo ni TISS.
Chanzo cha tatizo ni muundo usiofaa tulio nao, yaani tunachagua mtu mmoja (Rais)wakati wa uchaguzi mkuu halafu anakuta pale ikulu timu ya watu (TISS) wengine wana miaka hata 20 wako hapo.
Cha kushangaza TISS siku zote wanadai kazi zao ni ngumu, hivi kuna mtu anapenda kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu, hata km analipwa vizuri..kwa nini hatuoni wao TISS kuomba kubadilishiwa kazi kwa sabab ya kazi ngumu wanazofanya? hapa kuna hila..na Kati ya mambo wanamwambia Rais mpya ni kuwa wao (TISS) ndio wamefanya yeye Rais afike hapo, maana yake, bila wao asingefika hapo na hivyo wao ndio wanao urais wake..rejea maneno ya Rais wa awamu ya 5 akilalamikia kuwa anachomekewa watu wasiofaa kwenye uteuzi(waziri mpya kushindwa kusoma kiapo) na imetokea Rais mstaafu anakuwa na watu wake wengi ndani ya TISS ili aendelee kuongoza ndicho kinachotokea Tanzania..na inavyoonekana TISS inaundwa na kundi kubwa la vijana yaani ni under age kulingana na nature ya kazi wanazopaswa kufanya TISS kwa nchi, ndii maana uonevu ni mwingi sana Tanzania.
Kuna nchi moja ndani ya SADC Rais mpya alipoingia ikulu kwanza alibadilisha intelligence team yote, tumeona hata Rais Tinubu amefanya hivyo..
Pili, Rais huyo mpya aliteua intelligence team wote wapya na kazi ya kwanza aliyowaambia wafanye ni kwenda kila kata na kijiji ndani nchi kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaambia wananchi KAZI ZAO NI ZIPI KWA NCHI..
Hivi tunavyoongea Rais mstaafu wa nchi hiyo na baadhi ya maafisa wakubwa wastaafu akiwemo chifu wa intelligence mstaafu wako uhamishoni wamekimbia nchi..
Hivi ndivyo wanaojua uongozi na wana ajenda ya maendeleo wanapochaguliwa hufanya mara tu wanapoanza urais..
Tanzania imekwama sabab kubwa ni vested interest za wastaafu kupitia TISS angalia baadhi ya mawaziri hata tu tathmini ndogo ya face value judgement kuona km wanastahili kuwa mawaziri inakupa jibu HAWASTAHILI..lakini hao ndio TISS inawataka wale wasiojielewa anasukumwa tu km boya!
Hii shida ya bandari kutokuwa na tija inayopelekea kutafuta wawekezaji chanzo ni TISS angalia huyo DG wa sasa wa TPA bado mtoto hana sifa kabisa za nafasi hiyo, na sabab za kuweka mtu wa aina hii ni wao TISS kuwa na access ya kuinfluence utendaji na maamuzi yake throughout, a similar case hata kwa spika wa bunge..taifa lenye umri zaidi ya miaka 60 eti halina watu wazima wenye sifa za kuwa spika au DG wa TPA..si kweli!
Dawa ni wananchi kudeal na issue ya TISS wanavyopatikana wakati Rais mpya akichaguliwa na kazi zao kwa ujumla..tusipofanya hivi, nchi itakwama zaidi ya hapa tulipo.
Duuh, Naipenda sana nchi yangu .... hapo kwenye upatikanaji wa maafisa usalama walifanyie kazi aisee, watu ni weupe
 
Kwa hali hii ambayo nchi inapitia, uongozi mbovu, rushwa, ubinafsi, ufisadi, nepotism na vetting mbovu, uonevu nk TISS ndio chanzo cha hayo yote na tatizo linapoanzia ni muundo tulio nao, yaani tunachagua mtu mmoja (Rais)wakati wa uchaguzi mkuu halafu anakuta pale ikulu timu ya watu (TISS) wengine wana miaka hata 20 wako hapo.
TISS siku zote wanadai kazi zao ni ngumu, hivi kuna mtu anapenda kufanya kazi ngumu hata km analipwa vizuri..kwa nini hatuoni wao kuomba kubadilishiwa kazi kwa sabab ya kazi ngumu wanazofanya?Kati ya mambo wanamwambia Rais mpya ni kuwa wao (TISS) ndio wamefanya yeye Rais afike hapo, maana yake, bila wao asingefika hapo na hivyo wao ndio wanao urais wake..rejea maneno ya Rais wa awamu ya 5 akilalamikia kuwa anachomekewa watu wasiofaa kwenye uteuzi(waziri mpya kushindwa kusoma kiapo) na imetokea Rais mstaafu anakuwa na watu wake wengi ndani ya TISS ili aendelee kuongoza ndicho kinachotokea Tanzania..
Kuna nchi moja ndani ya SADC Rais mpya alipoingia ikulu alianza kwanza kubadilisha intelligence team yote, tumeona hata Rais Tinubu amefanya hivyo..
Pili, Rais huyo mpya aliteua intelligence team wote wapya na kazi ya kwanza aliyowaambia wafanye ni kwenda kila kata na kijiji ndani nchi kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaambia wananchi KAZI ZAO NI ZIPI KWA NCHI..
Hivi tunavyoongea Rais mstaafu wa nchi hiyo na baadhi ya maafisa wakubwa wastaafu akiwemo chifu wa intelligence mstaafu wako uhamishoni wamekimbia nchi..
Hivi ndivyo wanaojua uongozi na wana ajenda ya maendeleo wanapochaguliwa hufanya mara tu wanapoanza urais..
Tanzania imekwama sabab kubwa ni vested interest za wastaafu kupitia TISS angalia baadhi ya mawaziri hata tu tathmini ndogo ya face value judgement kuona km wanastahili kuwa mawaziri inakupa jibu HAWASTAHILI..lakini hao ndio TISS inawataka wale wasiojielewa anasukumwa tu km boya!
Hii shida ya bandari kutokuwa na tija inayopelekea kutafuta wawekezaji chanzo ni TISS angalia huyo DG wa sasa wa TPA bado mtoto hana sifa kabisa za nafasi hiyo, na sabab za kuweka mtu wa aina hii ni wao TISS kuwa na access ya kuinfluence utendaji na maamuzi yake throughout, a similar case hata kwa spika wa bunge..taifa lenye umri zaidi ya miaka 60 eti halina watu wazima wenye sifa za kuwa spika au DG wa TPA..si kweli!
Dawa ni wananchi kudeal na issue ya TISS wanavyopatikana wakati Rais mpya akichaguliwa na kazi zao kwa ujumla..tusipofanya hivi, nchi itakwama zaidi ya hapa tulipo.
Bwana Mwesigwa kada wa UVCC/afisa wa TISS aliwahi kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wa TPDC.
Kila siku huwa narudia kusema humu ndani, ila naonekana kama kichaa. Bila kuiondoa kinguvu ile MIZEE YA COLD-WAR kwenye mfumo hatuwezi kufika popote kama taifa.

Binafsi, huwa napenda mbinu aliyoitumia Xi Jinping baada ya kuingia madarakani. Alivunjilia mbali idara ya ujasusi (The 610 Office) yenye maofisa 15,000 iliyokuwa inatumiwa na Raisi Mstaafu Jiang Zemin na genge lake la Shanghai (The Shanghai Clique) kuongoza nchi kwa mlango wa nyuma. Intelijensia imevunjwa na Jiang Zemin na mtoto wake fisadi wakatikwa kizuizini. Bila kufanya hivi napa Tanzania kwa bwana yule hatuwezi kufika nchi ya ahadi.

Xi Jinping akaenda mbali, akamshughulikia Waziri Zhou Yonkang ambaye alikuwa anaongoza (The 610 Office) na kikosi maalumu chenye askari 8,00,000 ambao wanatumika kuidhibiti Tibet na Xinjiang. Huyu jamaa alipoona Xi amekuwa Raisi na ameanza kugusa wakubwa kama Bo Xilai, akaanza kuvikusanya vikosi vya maelfu ya makomandoo wakisingizia mazoezi, kumbe wanataka kufanya yao kimyakimya. Bahati mbaya wakawaiwa na kukatwa vichwa.

Huyu Bo Xilai ni mtu aliyekulia ndani ya mfumo kwasababu baba yake alikuwa ni kigogo wa serikali ya Raisi Mao. Ilitegemewa yeye ndiyo aje kuwa Raisi wa China, lakini akakosa. Jamaa alikuwa na nguvu kubwa mno, maana ndani ya china alitumia mifumo ya kijasusi kujijenga kisiasa. Ilifika kipindi alikuwa anadukua hadi mawasiliano ya Raisi aliyepo madaraka Hu Jintao, na kupeleka taarifa kwa Jiang Zemin ambaye ndiye alikuwa The God-Father wa genge la Shanghai. Unamdukua Raisi na kumtishia kweli, ??? HAIWEZEKANI HATA KIDOGO.

Mpaka sasa, Xi Jinping ameshughulikia maofisa na makada wa Uchina wasiopungua milioni 5 ambao walihusiana na Jiang Zemin, Zhou Yonkang na Bo Xilai. Majasusi wote ambao walikuwa wanijifanya ni watiifu kwa genge la Raisi Mstaafu walipigwa risasi hadharani, kunyongwa, kufungwa au kupelekwa Laogai (The Gulag). Bila kufanya hivi sidhani kama angetawala hata mwaka mmoja.

Huku kwetu ni kinyume kabisa, waliohujumu nchi na wahaini, wanajengewa makasri ya mabilioni ya fedha, huku wake na watoto zao wanapewa ubunge na uwaziri. Kiufupi tu, kuna changamoto kubwa mno ambayo bila kutumia mkono wa chuma haiwezi kuisha.


 
Kaombeni visa ya ujerumani au ufaransa iwe gateway ya kufika/kuingia kwingineko duniani... muhame huko na muhamishe na watoto... afrika sio pa kuishi, ni bara la laana! Kila kitu kipo ila majitu yanazidi kuwa mazwazwa na mabazazi kila kukicha. Ule msemo wa mkataa kwao mtumwa tuutathmini na tuutengue rasmi. Sometimes kukataa nyumbani ni chaguo pekee bora lililobaki.
 
NIDA inasimamiwa na TISS kwa asilimia 80%

Hivyo tukubali kwamba vijana wetu wa usalama wameshaasi viapo vyao na sasa wanaimega keki ya Taifa bila ruhusa
Asante kwa kuongeza hii.

Najua wengi walichomekwa kule kufanya kazi ya utambuzi, uchakataji na kulinda maslahi ya wazawa ila kwa kinachoendelea huko, ni aibu hata kusimulia sana.
 
Katika yote takukuru yanawahusu zaidi, ila Suala la NIDA linawahusu upande wa nani anayepewa kitambulisho.
 
Kaombeni visa ya ujerumani au ufaransa iwe gateway ya kufika/kuingia kwingineko duniani... muhame huko na muhamishe na watoto... afrika sio pa kuishi, ni bara la laana! Kila kitu kipo ila majitu yanazidi kuwa mazwazwa na mabazazi kila kukicha. Ule msemo wa mkataa kwao mtumwa tuutathmini na tuutengue rasmi. Sometimes kukataa nyumbani ni chaguo pekee bora lililobaki.
Dah unatoa mapendekezo makali na magumu kweli kweli!

Kuna siku nimeshuhudia basi Zima wamelipishwa nauli na cha juu, ilihali tiketi zikaandikwa with 3,000/- less, hakuna aliyekuwa anahoji. Imagine basi zima, wanaume kwa wanawake, nilisikitika sana.
Hii nchi hii, acha tu
 
Wapo ila sijui tumekwama wapi kama nchi. Tatizo linaumiza wananchi wengi na hawajali chochote!
Rais alihalalisha rushwa kwa matamshi yake bila kujua athari yake “ Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake “
Matokeo ya kauli ile ni kuzorota kwa huduma kwa jamii katika taasisi zote.

Huwezi kupata huduma toka maofisini mpaka polisi bila kutoa hongo! Hali imekuwa mbaya sana baada ya kuondoka Magufuli ; kwani sio siri kuwa enzi zake ukali wake uliwafanya watumishi kuwa na woga hivyo kutimiza wajibu wao.
 
Bwana Mwesigwa kada wa UVCC/afisa wa TISS aliwahi kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wa TPDC.
Kila siku huwa narudia kusema humu ndani, ila naonekana kama kichaa. Bila kuiondoa kinguvu ile MIZEE YA COLD-WAR kwenye mfumo hatuwezi kufika popote kama taifa.

Binafsi, huwa napenda mbinu aliyoitumia Xi Jinping baada ya kuingia madarakani. Alivunjilia mbali idara ya ujasusi (The 610 Office) yenye maofisa 15,000 iliyokuwa inatumiwa na Raisi Mstaafu Jiang Zemin na genge lake la Shanghai (The Shanghai Clique) kuongoza nchi kwa mlango wa nyuma. Intelijensia imevunjwa na Jiang Zemin na kijana wake fisadi wakatikwa kizuizini.

Akaenda mbali, akamshughulikia Waziri Zhou Yonkang ambaye alikuwa anaongoza (The 610 Office) na kikosi maalumu chenye askari 8,00,000 ambao wanatumika kuidhibiti Tibet na Xinjiang. Huyu jamaa alipoona Xi amekuwa Raisi na ameanza kugusa wakubwa, akaanza kuvikusanya vikosi wakisingizia mazoezi, kumbe wanataka kufanya yao kimyakimya. Bahati mbaya wakawaiwa.

Mpaka sasa, Xi Jinping ameshughulikia maofisa na makada wa Uchina wasiopungua milioni 5. Kiukweli, bila kufanya hivi sidhani kama angetawala. Huku kwetu ni kinyume kabisa, waliohujumu nchi wanajengewa nyumba na wake zao na watoto wao kupewa ubunge na uwaziri. Kiufupi tu, kuna changamoto kubwa mno..


Ulioandika hapa ni kweli kabisa.

Kuna vituko nchi hii, hadi wkt mwingine unasema labda tunaigiza maisha.

Kuna mheshimiwa mmoja mchambuzi wa masuala mtambuka, aliwahi kuniambia, akasema, nanukuu, "kaka nchi hii ukiivunja vunja CCM na TISS, nakuhakikishia itaanza kupata maendeleo makubwa sana".

Alisisitiza kwamba ktk uchambuzi wake, TISS na CCM wameiharibu nchi hii pakubwa sana kiasi ambacho huwezi kufikiri kawaida.


Kuna mengi sana sijaweza kuandika yote, yanasikitisha sana.
 
Mabati ya Mbagala BRT ni ya kampuni ya SGS Mabati. Nilishangaa sana, maana hata huku mitaani, hiyo kampuni haipo katika makampuni yanayotoa mabati bora. Yaani mwananchi wa kawaida tu kama haba hela ya kumudu ALAF au SUN SHARE basi anaona aende DRAGON au KIBOKO, ndio afuate huyo SGS.

Sasa tunashangaa inakuwaje Serikali kabisa kutumia mabati ya SGS??
 
Ulioandika hapa ni kweli kabisa.

Kuna vituko nchi hii, hadi wkt mwingine unasema labda tunaigiza maisha.

Kuna mheshimiwa mmoja mchambuzi wa masuala mtambuka, aliwahi kuniambia, akasema, nanukuu, "kaka nchi hii ukiivunja vunja CCM na TISS, nakuhakikishia itaanza kupata maendeleo makubwa sana".

Alisisitiza kwamba ktk uchambuzi wake, TISS na CCM wameiharibu nchi hii pakubwa sana kiasi ambacho huwezi kufikiri kawaida.


Kuna mengi sana sijaweza kuandika yote, yanasikitisha sana.
Shida ni hapo kwenye kuitoa CCM.
 
Ni usiku mnene. Naamua kuandika DOKEZO hili.
Kwa uchungu wa yanayoendelea katika nchi yangu.

Katika mada hii, nitaomba wachangiaji kujadili kwa uwazi kabisa, na kuongezea mifano mingine baada ya hii nitakayokuwa nimeiweka hapa.

Lengo ni Nia njema kabisa kurekebisha pale tulipokosea na kusaidia WaTz ambao wanakosa kufaidi matunda ya nchi yao.

Hapa chini ni jinsi ambavyo mambo ya ovyo yanafanywa wazi na TISS wala hawafanyi kazi yao iliyotukuka.

1. NIDA na Utoaji wa NAMBA/Vitambulisho vya Taifa.

Hili jambo ni kubwa sana. Mimi nimelithibitisha. Na wote wanaofika kuhudumiwa katika ofisi zote za NIDA nchi nzima wanasema wazi.
Iko hivi, huwezi kufanikisha kupata namba ya NIDA ikiwa huna kiasi flani cha fedha. Na huwezi kupata ile ID ikiwa huna kiasi kikubwa zaidi cha fedha.
Yani utaenda utafuata taratibu zote na kuwa na viambatanisho vyote, lakini huwezi kupata kimojawapo kati ya hivyo bila fedha.
Kiufupi hadi mlinzi wa getini anajua hilo.
Baadhi ya Ofisi za NIDA DSM kupata namba ya NIDA inaanzia sh. 150,000/-. Kupata ID ni kuanzia sh. 500,000/-
Lakini kadri utakavyoongeza dau maana yake utawahishiwa zaidi mchakato wako.

Kwanza hakuna huduma pale, zaidi ukifika upangwe foleni na walinzi, ukiingia unakuta mtu anachat tu, hadi jioni uambiwe njoo tena kesho.

Haya yana muda mrefu yanafanywa wazi kabisa. Hatari hii ni kwamba sasa hata mgeni je, akiwa na milion zake mbili si anapewa zake ID kama MTz??

Mh. Rais wetu ni msikivu, je, ulishasikia amepewa ripoti hii akashindwa kuifanyia kazi?!

Nani wa kumpelekea ripoti kama sio TISS?

2. Mradi wa mwendokasi Mbagala.
Huu mradi nendeni mchunguze, ni mbovu na umejengwa chini ya viwango vibaya mno.

Uchunguzi unaonesha baadhi ya miundombinu kuanza kuharibika hata kabla ya matumizi rasmi kuanza.
Wasichokijua ni kwamba hii miradi ya miundombinu ya barabara huwa na zaidi ya miaka 20 ya uhai kabla ya marekebisho.
Sasa ukifika pale ukakuta baadhi ya beacon zimeanguka, kumeguka, n.k, Unajiuliza shida ni nini? Bajeti ndogo ya ujenzi? Lakini hilo linakataa kwa sababu hizi fedha ni mkopo tumepata kutoka Benki ya Dunia (WB), hawawezi kutenga fedha chini ya inayotakiwa.!
Sasa vile vituo vya abiria ndio utacheka kabisa. Mabati ni chini ya viwango, hizo frame walizichomelea ni chini ya viwango, uchomeleaji wenyewe ni wa dizaini za fundi maiko.

Hata wakibisha, nawahakikishieni, barabara ya mwendokasi ya Posta KIMARA itadumu, na hii ya Mbagala itakuja kuharibika mapema kabla yake. Tuko hapa mtakuja kuthibitisha panapo uhai.

Sasa kwa hali hii, utasema Rais wetu alivyo msikivu, ana hii ripoti mezani kweli? Na hatujasikia akichukua hatua zozote?

3. UHABA wa petrol sasa hivi nchini.

Hapa siandiki sana.
Fahamuni kwamba mafuta yapo. Si mlisikia hata Waziri anasema hakuna upungufu wa petrol. Si amesema mara nyingi tu!

Sasa Mimi na wewe tuulizane, Waziri anasema yapo, vituoni ukifika hakuna, yapo wapi? Eeh...

Jamaa wana mafuta, ila hawatoi kuyauza. Wanasubiri bei mpya za August, zipande usiku wa leo tarehe 31/07/2023 ndio wataanza kutoa mafuta.

Sasa "syndicate" ya namna hii, hapo unasema TISS wapo na wananchi, au wametuma ripoti Rais hajachukua hatua?!

Achaneni na mambo ya ooh Dola $ kuadimika, hiyo inaathiri uagizaji wa mzigo mpya. Sio stock iliyopo ambayo huagizwa miezi mitatu au zaidi nyuma.

4. Nauli za mabasi za LATRA.

Hivi mnajua mabasi yote ya mikoani katika stendi zote za mikoani wanachaji nauli zaidi ya zile zilizoidhinishwa na LATRA?!

USHAHIDI upo.

Hapa namaanisha hata LATRA na mapolisi wanalijua hilo. Je, ni fungu wanapewa au kuamua kuacha tu unyang'anyi huu uendelee?!

Nasisitiza iko hivyo, stendi zote, mikoa yote.

Nenda Dsm, Mwanza, Morogoro, Iringa, Dodoma, Tabora, Kagera, Mbeya, Arusha, Tanga, Mtwara, Kigoma, n.k, kote huko wana 'overcharge'.

Sasa kama watu wa mabasi wanaona nauli zilizopangwa ni ndogo, haziwapi faida, si bora LATRA ipitishe hizo hizo wanazolipishwa wananchi ili ifahamike moja.

Je, unataka kusema ripoti za haya zipo mezani kwa mh. Rais ila jinsi alivyo anajali watu wake kweli asichukue hatua.?!

Narudia ripoti hii ni kwa Nia njema ya kujenga Taifa letu.

Ukweli huduma za umma zimezorota kiasi kikubwa, tusifiche tatizo na wananchi wengi wanaumia sana na hili.

Naomba kuhitimisha hapo kwa leo.

Karibuni wachangiaji kwa mengi zaidi.
Mimi nimethibitisha hilo la NIDA nikiwa nafuatilia ili mwanangu aende chuo.
ukitaka kujua kama ripoti zipo mezani au la
jiulize swali hili,Je ripoti ya mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ipo mezani au la?
ukipata majibu ndipo utajua kama hilo suala la usikivu ni halisi au siasa.
 
Na kusimamia mitihani ya darasa la 7 na kidato cha nne. Anakuja DSO kabisa kusaini ile bahasha kuwa haijafunguliwa😃😃
Sajo,

Tatizo ni kubwa. Unacheka kama mazuri.

Nimekumbuka kitu... Mtihani wenyewe wa Hisabati Darasa la 7 ni multiple choice (wa kuchagua).

Imagine kitu kama hicho kilipata 'clearance' ya watu wa TISS huko , Hisabati mtihani wa kuchagua, kweli?!

Leo nchi tuna watoto hawajui kuhesabu, wame pass.
 
Mimi nimethibitisha hilo la NIDA nikiwa nafuatilia ili mwanangu aende chuo.
ukitaka kujua kama ripoti zipo mezani au la
jiulize swali hili,Je ripoti ya mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ipo mezani au la?
ukipata majibu ndipo utajua kama hilo suala la usikivu ni halisi au siasa.
Asante kwa UTHIBITISHO na USHAHIDI.
 
Acha ubahili. Unaendekeza ubahili halafu unakuja lia lia hapa. Utakuja pata kitambulisho ukiwa umezeeka sana au umefariki wakuchukulie ndugu zako.
Yes, umemueleza ukweli. Akienda na sh. 500,000/- anapata ID ndani ya wiki kadhaa tu.
 
Jambo jingine ninaloliona kuwa ni shida,ni vyombo vya dola kuwa sehemu ya vyama vya siasa.

si ajabu na hao tisu ni makada,na wanatekeleza ilani.

Kusema ukweli kuna mwenyekiti wa chama wa kijiji fulani mkoa wa pwani amenitapeli kiwanja,na siku ananifanyia utapeli huo, alikuwa amevaa nguo ya chama,nikajua nimepata kumbe nikawa nimepatikana.

sasa kumbe kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.

Tutulie,tuendelee kunawa mikono kwa maji tiririka kuepuka corona maana inaua.
 
KWA NINI UNAANDIKA UONGO,MAJUZI NIMEKWENDA OFISI ZA NIDA UKONGA,WAMEFANYIA PROCESS ZOTE FREE TENA KWA HARAKA WAMENIPA WIKI MBILI NIKACHUKUWE NAMBA,KWANZA ID ITAFUATA.
#ACHENI UONGO NA UPOTOSHAJI.
Kwanza hakuna ofisi za NIDA UKONGA, zipo gongo la mboto (kituo panaitwa MOMBASA) .

Sasa ukitaka niandike mazito ya hapo utajuta.
 
Back
Top Bottom