DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Shida ni hapo kwenye kuitoa CCM.
Shida siyo CCM muwe mnaelewa, shughulika na walio nyuma ya ccm, hivi ccm ndio huwa wanavuruga uchaguzi? Ukitaka kuondoa tatizo deal na chanzo cha tatizo usipoteze muda kushughulikia matokeo ya tatizo..ccm ni matokeo ya tatizo si chanzo cha tatizo.
 
Sajo,

Tatizo ni kubwa. Unacheka kama mazuri.

Nimekumbuka kitu... Mtihani wenyewe wa Hisabati Darasa la 7 ni multiple choice (wa kuchagua).

Imagine kitu kama hicho kilipata 'clearance' ya watu wa TISS huko , Hisabati mtihani wa kuchagua, kweli?!

Leo nchi tuna watoto hawajui kuhesabu, wame pass.
Mkuu, mimi nimeangalia TV Series ya Homeland, The Americans, The Spy na kuona namna Secret Service wanavyokua wazalendo kwa nchi zao na namna wanavyopambana kupata habari za kiuchumi au hata kuharibu uchumi wa washindani wao ili nchi itoboe..dah yaani mpaka naona aibu kusema kuwa Tanzania tuna idara inaitwa usalama wa Taifa.

Alikuja Bill Gates hapa akawa Tanga kwenye ishu zake za Maralia, usalama wa Taifa hawajui kama yupo nchini. Alipopigwa picha na watu na zikasambaa mitandaoni ndio JPM akamwalika ikulu. Sasa mtu kama Bill Gates anaingia nchini na kuondoka bila kujikana, hapo tuna TISS kweli?

Kawaida inatakiwa TISS wajue leo Bakhresa au Mo Dewji amelala wapi, anafanya nini nk maana hawa jamaa ndio wanaorun uchumi wa nchi kwa biashara zao, wanazalisha ajira nyingi na wanachangia pato kubwa la nchi. Sasa cha ajabu unaambiwa Mo Dewji ametekwa nje ya gym na usalama wa Taifa wamelala kusubiri kusimamia mitihani.

Tuliambiwa na wamarekani hapa kuwa Jihad John (yule mchinjaji wa ISIS) akiwahi kuingia hapa nchini mara 2 kupitia JKNIA na TISS hawakujua. Sasa unafikiri kuna majasusi wangapi wanaingia nchini kwa njia hizi za wazi, Bandari au Airport na hawajulikani? Tunafahamu wanakuja kufanya vitu gani?
 
Hawa jamaa wanaitwa SINOHYDRO ni Wala rushwa balaaa, Sasa viongozi wengi Sana wakifika wanapewa Chao wanaishia kupiga mkwara fake na kuondoka, mnakumbuka Yule DC Gondwe? Alienda akapiga mkwara Yule mbongo akawa anacheka TU?

Ujenzi wowote nchini ulio chini ya SINOHYDRO au STECOL (NDIO Huyo huyo SINOHYDRO) ni mibovu balaaa na hawajawahi kumaliza on time.

Wana kashfa za kuwanyanyasa wafanyakazi Sana na wale jamaa wa TAMICO hawana Cha kufanya.

Huu mradi wa BRT waliwahi kupata kashfa ya kutumia lami ambayo source yake ilikua nchi ambayo imewekewa vikwazo.

Na NDIO hawa hawa wamepewa SGR bila kutumia utaratibu wa manunuzi, yaani single source, Kuna siku Tanzania itaomboleza wallah.
Mwezi Februali nilipita hapo nikiwa Kwenye Bodaboda mpaka tukawa tunashangaa mimi na boda boda wangu.

Yaani ile njia ya Magari mwendo kasi(lane) imeshakamilika lakini imeshaanza kubanduka cement.
 
Kaombeni visa ya ujerumani au ufaransa iwe gateway ya kufika/kuingia kwingineko duniani... muhame huko na muhamishe na watoto... afrika sio pa kuishi, ni bara la laana! Kila kitu kipo ila majitu yanazidi kuwa mazwazwa na mabazazi kila kukicha. Ule msemo wa mkataa kwao mtumwa tuutathmini na tuutengue rasmi. Sometimes kukataa nyumbani ni chaguo pekee bora lililobaki.
Wewe uko wapi ndugu?
 
Asante kwa kuongeza hii.

Najua wengi walichomekwa kule kufanya kazi ya utambuzi, uchakataji na kulinda maslahi ya wazawa ila kwa kinachoendelea huko, ni aibu hata kusimulia sana.
Lakini wewe si Mwanaccm? Kwa hiyo unaikosoa serikali yako mwenyewe?
 
Back
Top Bottom