DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
2. Mradi wa mwendokasi Mbagala.
Huu mradi nendeni mchunguze, ni mbovu na umejengwa chini ya viwango vibaya mno.
Hawa jamaa wanaitwa SINOHYDRO ni Wala rushwa balaaa, Sasa viongozi wengi Sana wakifika wanapewa Chao wanaishia kupiga mkwara fake na kuondoka, mnakumbuka Yule DC Gondwe? Alienda akapiga mkwara Yule mbongo akawa anacheka TU?

Ujenzi wowote nchini ulio chini ya SINOHYDRO au STECOL (NDIO Huyo huyo SINOHYDRO) ni mibovu balaaa na hawajawahi kumaliza on time.

Wana kashfa za kuwanyanyasa wafanyakazi Sana na wale jamaa wa TAMICO hawana Cha kufanya.

Huu mradi wa BRT waliwahi kupata kashfa ya kutumia lami ambayo source yake ilikua nchi ambayo imewekewa vikwazo.

Na NDIO hawa hawa wamepewa SGR bila kutumia utaratibu wa manunuzi, yaani single source, Kuna siku Tanzania itaomboleza wallah.
 
Duuh, Naipenda sana nchi yangu .... hapo kwenye upatikanaji wa maafisa usalama walifanyie kazi aisee, watu ni weupe
 
Bwana Mwesigwa kada wa UVCC/afisa wa TISS aliwahi kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wa TPDC.
Kila siku huwa narudia kusema humu ndani, ila naonekana kama kichaa. Bila kuiondoa kinguvu ile MIZEE YA COLD-WAR kwenye mfumo hatuwezi kufika popote kama taifa.

Binafsi, huwa napenda mbinu aliyoitumia Xi Jinping baada ya kuingia madarakani. Alivunjilia mbali idara ya ujasusi (The 610 Office) yenye maofisa 15,000 iliyokuwa inatumiwa na Raisi Mstaafu Jiang Zemin na genge lake la Shanghai (The Shanghai Clique) kuongoza nchi kwa mlango wa nyuma. Intelijensia imevunjwa na Jiang Zemin na mtoto wake fisadi wakatikwa kizuizini. Bila kufanya hivi napa Tanzania kwa bwana yule hatuwezi kufika nchi ya ahadi.

Xi Jinping akaenda mbali, akamshughulikia Waziri Zhou Yonkang ambaye alikuwa anaongoza (The 610 Office) na kikosi maalumu chenye askari 8,00,000 ambao wanatumika kuidhibiti Tibet na Xinjiang. Huyu jamaa alipoona Xi amekuwa Raisi na ameanza kugusa wakubwa kama Bo Xilai, akaanza kuvikusanya vikosi vya maelfu ya makomandoo wakisingizia mazoezi, kumbe wanataka kufanya yao kimyakimya. Bahati mbaya wakawaiwa na kukatwa vichwa.

Huyu Bo Xilai ni mtu aliyekulia ndani ya mfumo kwasababu baba yake alikuwa ni kigogo wa serikali ya Raisi Mao. Ilitegemewa yeye ndiyo aje kuwa Raisi wa China, lakini akakosa. Jamaa alikuwa na nguvu kubwa mno, maana ndani ya china alitumia mifumo ya kijasusi kujijenga kisiasa. Ilifika kipindi alikuwa anadukua hadi mawasiliano ya Raisi aliyepo madaraka Hu Jintao, na kupeleka taarifa kwa Jiang Zemin ambaye ndiye alikuwa The God-Father wa genge la Shanghai. Unamdukua Raisi na kumtishia kweli, ??? HAIWEZEKANI HATA KIDOGO.

Mpaka sasa, Xi Jinping ameshughulikia maofisa na makada wa Uchina wasiopungua milioni 5 ambao walihusiana na Jiang Zemin, Zhou Yonkang na Bo Xilai. Majasusi wote ambao walikuwa wanijifanya ni watiifu kwa genge la Raisi Mstaafu walipigwa risasi hadharani, kunyongwa, kufungwa au kupelekwa Laogai (The Gulag). Bila kufanya hivi sidhani kama angetawala hata mwaka mmoja.

Huku kwetu ni kinyume kabisa, waliohujumu nchi na wahaini, wanajengewa makasri ya mabilioni ya fedha, huku wake na watoto zao wanapewa ubunge na uwaziri. Kiufupi tu, kuna changamoto kubwa mno ambayo bila kutumia mkono wa chuma haiwezi kuisha.


 
Kaombeni visa ya ujerumani au ufaransa iwe gateway ya kufika/kuingia kwingineko duniani... muhame huko na muhamishe na watoto... afrika sio pa kuishi, ni bara la laana! Kila kitu kipo ila majitu yanazidi kuwa mazwazwa na mabazazi kila kukicha. Ule msemo wa mkataa kwao mtumwa tuutathmini na tuutengue rasmi. Sometimes kukataa nyumbani ni chaguo pekee bora lililobaki.
 
NIDA inasimamiwa na TISS kwa asilimia 80%

Hivyo tukubali kwamba vijana wetu wa usalama wameshaasi viapo vyao na sasa wanaimega keki ya Taifa bila ruhusa
Asante kwa kuongeza hii.

Najua wengi walichomekwa kule kufanya kazi ya utambuzi, uchakataji na kulinda maslahi ya wazawa ila kwa kinachoendelea huko, ni aibu hata kusimulia sana.
 
Katika yote takukuru yanawahusu zaidi, ila Suala la NIDA linawahusu upande wa nani anayepewa kitambulisho.
 
Dah unatoa mapendekezo makali na magumu kweli kweli!

Kuna siku nimeshuhudia basi Zima wamelipishwa nauli na cha juu, ilihali tiketi zikaandikwa with 3,000/- less, hakuna aliyekuwa anahoji. Imagine basi zima, wanaume kwa wanawake, nilisikitika sana.
Hii nchi hii, acha tu
 
Wapo ila sijui tumekwama wapi kama nchi. Tatizo linaumiza wananchi wengi na hawajali chochote!
Rais alihalalisha rushwa kwa matamshi yake bila kujua athari yake “ Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake “
Matokeo ya kauli ile ni kuzorota kwa huduma kwa jamii katika taasisi zote.

Huwezi kupata huduma toka maofisini mpaka polisi bila kutoa hongo! Hali imekuwa mbaya sana baada ya kuondoka Magufuli ; kwani sio siri kuwa enzi zake ukali wake uliwafanya watumishi kuwa na woga hivyo kutimiza wajibu wao.
 
Ulioandika hapa ni kweli kabisa.

Kuna vituko nchi hii, hadi wkt mwingine unasema labda tunaigiza maisha.

Kuna mheshimiwa mmoja mchambuzi wa masuala mtambuka, aliwahi kuniambia, akasema, nanukuu, "kaka nchi hii ukiivunja vunja CCM na TISS, nakuhakikishia itaanza kupata maendeleo makubwa sana".

Alisisitiza kwamba ktk uchambuzi wake, TISS na CCM wameiharibu nchi hii pakubwa sana kiasi ambacho huwezi kufikiri kawaida.


Kuna mengi sana sijaweza kuandika yote, yanasikitisha sana.
 
Mabati ya Mbagala BRT ni ya kampuni ya SGS Mabati. Nilishangaa sana, maana hata huku mitaani, hiyo kampuni haipo katika makampuni yanayotoa mabati bora. Yaani mwananchi wa kawaida tu kama haba hela ya kumudu ALAF au SUN SHARE basi anaona aende DRAGON au KIBOKO, ndio afuate huyo SGS.

Sasa tunashangaa inakuwaje Serikali kabisa kutumia mabati ya SGS??
 
Shida ni hapo kwenye kuitoa CCM.
 
Mimi nimethibitisha hilo la NIDA nikiwa nafuatilia ili mwanangu aende chuo.
ukitaka kujua kama ripoti zipo mezani au la
jiulize swali hili,Je ripoti ya mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ipo mezani au la?
ukipata majibu ndipo utajua kama hilo suala la usikivu ni halisi au siasa.
 
Na kusimamia mitihani ya darasa la 7 na kidato cha nne. Anakuja DSO kabisa kusaini ile bahasha kuwa haijafunguliwa😃😃
Sajo,

Tatizo ni kubwa. Unacheka kama mazuri.

Nimekumbuka kitu... Mtihani wenyewe wa Hisabati Darasa la 7 ni multiple choice (wa kuchagua).

Imagine kitu kama hicho kilipata 'clearance' ya watu wa TISS huko , Hisabati mtihani wa kuchagua, kweli?!

Leo nchi tuna watoto hawajui kuhesabu, wame pass.
 
Asante kwa UTHIBITISHO na USHAHIDI.
 
Acha ubahili. Unaendekeza ubahili halafu unakuja lia lia hapa. Utakuja pata kitambulisho ukiwa umezeeka sana au umefariki wakuchukulie ndugu zako.
Yes, umemueleza ukweli. Akienda na sh. 500,000/- anapata ID ndani ya wiki kadhaa tu.
 
Jambo jingine ninaloliona kuwa ni shida,ni vyombo vya dola kuwa sehemu ya vyama vya siasa.

si ajabu na hao tisu ni makada,na wanatekeleza ilani.

Kusema ukweli kuna mwenyekiti wa chama wa kijiji fulani mkoa wa pwani amenitapeli kiwanja,na siku ananifanyia utapeli huo, alikuwa amevaa nguo ya chama,nikajua nimepata kumbe nikawa nimepatikana.

sasa kumbe kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.

Tutulie,tuendelee kunawa mikono kwa maji tiririka kuepuka corona maana inaua.
 
KWA NINI UNAANDIKA UONGO,MAJUZI NIMEKWENDA OFISI ZA NIDA UKONGA,WAMEFANYIA PROCESS ZOTE FREE TENA KWA HARAKA WAMENIPA WIKI MBILI NIKACHUKUWE NAMBA,KWANZA ID ITAFUATA.
#ACHENI UONGO NA UPOTOSHAJI.
Kwanza hakuna ofisi za NIDA UKONGA, zipo gongo la mboto (kituo panaitwa MOMBASA) .

Sasa ukitaka niandike mazito ya hapo utajuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…