DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Movies zinawaharibu sana. Halafu tiss kazi zao sio maonyesho na kwakuwa hawaripoti kwako basi ukabaki kuamini uyaonayo ktk movies.
Kagame akasema akipewa bandari ya Dar kwa mwaka 1, tunaongoza uchumi East Africa. Unafikiri alikuwa anasema kufurahisha genge tu?

 
Dah!
 
We might be naked
 
Hilo la NIDA umeweka too General.

Sio kweli kwamba Ofisi zote za NIDA nchini zina hayo mambo ya Rushwa.

Ni baadhi tu ya watumishi wasiokuwa waaminifu, na ni kwa baadhi tu ya maeneo.

Sio nchi nzima kama ulivyowasilisha.
 
Hauamini kama Bill Gates alikuja Tanzania? Hauamini kama Mo Dewji alitekwa na kuachiwa na watekaji bila watekaji kujulikana? Hauamini kama Jihad John ametua JKNIA mara 2??

Karne hii TISS kusimamia mitihani ya la saba kweli?
Asante, umemjibu huyu @TAwagacarlos vyema kabisa
 
Inawezekana

Inawezekana kweli imetulia lakini utulivu inaweza ikawa ni kwa mazoea ya Tiss ya zamani iliyokuwa imara ila ya sasa kwa kweli ina mahali inafeli maana kuna mambo mengi sana ya hovyo yanafanyika.

Unajua inapofikia hatua mpaka wanyama wanasafirishwa kwenda nje ujue pia hauko salama sana, watu wanafukuzwa Loliondo kumpisha mwarabu au mwekezaji si hali nzuri kwa ustawi wa taifa.

Inatakiwa ifike mahali walinde rasilimali za taifa ili hata vizazi vijavyo vifurahie uwepo wa watangulizi wao, haipendezi walikute taifa limebaki mifupa mitupu.
 
shida huku tuliwapeleka watoto wetu tena waliokuwa wasumbufu badala ya taaluma na vigezo wengi walipebwa japo wapo waliobebwa wamefika kule wakawa watendaji wazuri lakini pia wapo walioingia kwa vigezo wakafika kule wakawa chawa na wapiga zomari wa wakubwa.
 
Yale mabati ni kituko. Life span ya miaka 20 itafikaje pale.

Sasa na zile steel plate walizochomelea ni kama utani. Hata ambae hajaenda VETA hawezi kulipua vile. Wenzao STRABAG walikuwa wanafunga na nuts tena walitumia pipe ili hata hewa iwe ya kutosha mle ndani.
 
Hapa umesema sahihi kabisa. Kinachofanya kazi ni mifumo ya enzi.

Kwa sasa ni laiz a fare..
 
Kawaida inatakiwa TISS wajue leo Bakhresa au Mo Dewji amelala wapi, anafanya nini nk maana hawa jamaa ndio wanaorun uchumi wa nchi kwa biashara zao, wanazalisha ajira nyingi na wanachangia pato kubwa la nchi
Haya Mambo yako Israeli. Kwa Africa bado sana tuendelee kugombania box la kura.
 
Kuna hizi lawama zinarudiwa kila mara kwamba huko TISS wengi wanachomekwa tu. Mimi sijui zina ukweli gani..

Ila kufanyia mzaha taasisi nyeti kama hii, ni kutafuta anguko kila sekta.
Ni jambo la kushangaza na kukera nchi yenye umri wa mtu mzima wenye dhamana wanabehave km maamuma wasiojua wajibu wao kwa nchi..inakuwaje kunakosekana namna nzuri ya kurecruit TISS Staff..inawezekana kauli hizo za kusema watu wanachomekwa ni visingizio vya kujenga excuse pale makosa yanapotokea ionekane yamefanyika kutokana na kutokuwa na watu wenye sifa stahiki lkn kumbe wanafanya makusudi kumeet interest zao..taasisi km hii TISS lazima uwepo mwongozo kikatiba namna inatakiwa iundwe na majukumu yake, huu si muda wa kufanyiana mizaha kwa gharama ya maisha ya watu kupotea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…