DOKEZO TAKUKURU Nendeni Mikocheni Sekondari mkaone Walimu wanavyodai Rushwa Waziwazi Kwa Waliomaliza Form4

DOKEZO TAKUKURU Nendeni Mikocheni Sekondari mkaone Walimu wanavyodai Rushwa Waziwazi Kwa Waliomaliza Form4

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waanze kwanza na taharifa ya CAG
😆😆😆😆,
Mkuu hivi vitoto vinavyogongwa Rushwa tangu vikiwa Sekondari ndio vinavyokuja kuwasumbua Takukuru na CAG wajao.
 
Kwema Wakuu,

Hapa mtaani nilipo kuna ka binti kamemaliza Form4 na majibu ndio yametoka siku chache zilizopita. Shule aliyomaliza inaitwa Mikocheni Sekondari, na ilipo ni njia ya Kawe (Old Bagamoyo Road) kituo kimoja kabla ya Clouds.

Sasa wanafunzi hawa waliomaliza form 4 ili wakabidhiwe Leaving Certificates zao basi inabidi wapite kwa walimu wao mbalimbali na idara mbalimbali pia kusainisha "Clearance Forms", zikishasainiwa pote ndipo wapewe Leaving Certificate.

Walimu kwa kujua kua Wanafunzi wanazihitaji hizo Clearance Certificates wana mchezo wa kuwadai Chochote wanafunzi hao kisha ndio wawasainie. Wanaita hela ya soda lakini imekua ni lazima na mwanafunzi ukiweka ngumu kutoa chochote kitu basi husainiwi.

Iliwahi kutokea hapo kabla kua Wanafunzi kadhaa huchangishana, kuandika majina yao na kukusanya form kisha mmoja huzipeleka kwa mwalimu husika kusaini.

Hata kama ndio motisha lakini isiwe lazima basi, kama mwanafunzi kweli humdai basi ni wajibu wako kumsainia form yake bila kudai chochote kitu.

Watu mnaopokea mishahara Mnajidhalilisha kumkomalia mwanafunzi ambae hana kazi yoyote akupe wewe hela ya soda wakati ni wajibu wako.
Unaweza ukakuta Mzazi TAKUKURU, na yeye ameshotoa hicho unachokiita RUSHWA.
 
Walimu nao wameona wajilipe Kwa namna hyo eti hivi ni haki kweli, imagine nchi Ina wafanyakazi wa Takukuru lkn hawafanyi chochote. Ivi ni lini umeskia Takukuru wamekamata mtu Kwa Rushwa ivi karibuni
Mambo ya kujiongeza [emoji1]

Ova
 
Ulipata zeroo?!!!kama huna KAZI na cheti[emoji2][emoji2][emoji2][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125] nakutania broohhh
😄😁😄kwani
 
Kwema Wakuu,

Hapa mtaani nilipo kuna ka binti kamemaliza Form4 na majibu ndio yametoka siku chache zilizopita. Shule aliyomaliza inaitwa Mikocheni Sekondari, na ilipo ni njia ya Kawe (Old Bagamoyo Road) kituo kimoja kabla ya Clouds.

Sasa wanafunzi hawa waliomaliza form 4 ili wakabidhiwe Leaving Certificates zao basi inabidi wapite kwa walimu wao mbalimbali na idara mbalimbali pia kusainisha "Clearance Forms", zikishasainiwa pote ndipo wapewe Leaving Certificate.

Walimu kwa kujua kua Wanafunzi wanazihitaji hizo Clearance Certificates wana mchezo wa kuwadai Chochote wanafunzi hao kisha ndio wawasainie. Wanaita hela ya soda lakini imekua ni lazima na mwanafunzi ukiweka ngumu kutoa chochote kitu basi husainiwi.

Iliwahi kutokea hapo kabla kua Wanafunzi kadhaa huchangishana, kuandika majina yao na kukusanya form kisha mmoja huzipeleka kwa mwalimu husika kusaini.

Hata kama ndio motisha lakini isiwe lazima basi, kama mwanafunzi kweli humdai basi ni wajibu wako kumsainia form yake bila kudai chochote kitu.

Watu mnaopokea mishahara Mnajidhalilisha kumkomalia mwanafunzi ambae hana kazi yoyote akupe wewe hela ya soda wakati ni wajibu wako.
Acha unoko kwa issue ndogo
 
Mpwayungu njoo huku uwashauri walimu mambo wanayostahili kufanya
 
Nikajua yakuburashia viatu kumbe ya Pepsi tu acha roho mbaya [emoji16]
 
Nikajua yakuburashia viatu kumbe ya Pepsi tu acha roho mbaya [emoji16]
Hizi shule darasa moja hufika mpaka 120. Hawa wote wakitoa buku buku kumpa kila mwalimu kwani wanakunywa soda kreti ngapi?
 
Huu ni uongo.....mwanao anadaiwa huyo
Wewe ni mwalimu wa pale imekugusa kua exposed. Sina mtoto au ndugu anaesoma hapo. Ngoja TAKUKURU watakapofika hapo wakawahoji ndio mtaelewa.
Screenshot_20230806-130757.jpg
 
Wewe unaoushahidi?

Au umesimuliwa na mtoto wako ambaye pengine alitaka pesa ya matumizi yake binafsi ila akasingizia Waalimu wanataka Rushwa ndo apewe leaving certificate?

Usipende kuchafua taasisi pasipo na ushahidi.

Kumaliza shule mwanao isiwe kigezo Cha kuwadharirisha Waalimu.

Walimu wamekufundishia mtoto wako miaka minne halafu Leo unakuja kuwazushia maneno ya kuwadharirisha kiasi hiki?
Hao ni Wale wazazi lia lia, wao ni kulalamika tu

Hata Mwanae akimwomba hela ya kununua kitabu cha Physics au Biology Practical atamnyima na kusema Waalimu watakula hizo pesa

Hovyo sana
 
Rushwa na michango ya lazima kwa wanafunzi kwenye mashule yote siku hizi imekuwa kawaida.
 
Walimu wakiwagongea vibinti vyenu mnalalamika... Wakiwagongea wake zenu wanapo peleka watoto shule mnalalamika... Wanadai hela kama police na daktari bado mnalalamika...? 😂😂😂
 
Back
Top Bottom