DOKEZO TAKUKURU Nendeni Mikocheni Sekondari mkaone Walimu wanavyodai Rushwa Waziwazi Kwa Waliomaliza Form4

DOKEZO TAKUKURU Nendeni Mikocheni Sekondari mkaone Walimu wanavyodai Rushwa Waziwazi Kwa Waliomaliza Form4

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwema Wakuu,

Hapa mtaani nilipo kuna ka binti kamemaliza Form4 na majibu ndio yametoka siku chache zilizopita. Shule aliyomaliza inaitwa Mikocheni Sekondari, na ilipo ni njia ya Kawe (Old Bagamoyo Road) kituo kimoja kabla ya Clouds.

Sasa wanafunzi hawa waliomaliza form 4 ili wakabidhiwe Leaving Certificates zao basi inabidi wapite kwa walimu wao mbalimbali na idara mbalimbali pia kusainisha "Clearance Forms", zikishasainiwa pote ndipo wapewe Leaving Certificate.

Walimu kwa kujua kua Wanafunzi wanazihitaji hizo Clearance Certificates wana mchezo wa kuwadai Chochote wanafunzi hao kisha ndio wawasainie. Wanaita hela ya soda lakini imekua ni lazima na mwanafunzi ukiweka ngumu kutoa chochote kitu basi husainiwi.

Iliwahi kutokea hapo kabla kua Wanafunzi kadhaa huchangishana, kuandika majina yao na kukusanya form kisha mmoja huzipeleka kwa mwalimu husika kusaini.

Hata kama ndio motisha lakini isiwe lazima basi, kama mwanafunzi kweli humdai basi ni wajibu wako kumsainia form yake bila kudai chochote kitu.

Watu mnaopokea mishahara Mnajidhalilisha kumkomalia mwanafunzi ambae hana kazi yoyote akupe wewe hela ya soda wakati ni wajibu wako.
Wawarekodi na simu Kila ofisi wanayoenda watege sound recording
 
Form 4 wa mwaka huu wanamaliza Nov kama sikosei
Selection za mwisho zilizotoka ni za Form 4 wa mwaka 2022. Kuna documents zinahitajika nadhan kwenye shule wanakoenda ndio maana Sasa wanahangaikia mashuleni walikotoka.
 
Back
Top Bottom