TAKUKURU, Polisi waja na muarobaini wa rushwa za barabarani wakishirikiana na wadau

Ushauri wangu ziwekwe camera za kudumu barabarani kama Nairobi zitasaidia kupunguza rushwa ya speed na haya wizi Wa Magari.pili vituo vya polisi USA river,pia ni shida askari wawe wanahamishwa Mara Kwa mara
Utaweka kamera hadi porini? Wanachotakiwa kufanya ni kuwapa motisha watu watakaopeleka vidhibiti vya askari wanaotoa rushwa.
 
Magari yetu ndo kitega uchumi,jiulize kwann daladala ndo zinaonewa sana,ukifika vituoni asubui daladala zimejaa jioni uzioni zishaacha pesa kuingia bure kutoka hela plus ya breakdown hata kama gari ni nzima watalazimisha ivutwe.Wanapenda daladala sababu daladala hawana mda wa kusimama mahakamani watapoteza muda huku gari imezuia kituoni hata kama ni haki yake yuko radhi atolewe pesa kuokoa siku maana kulala kituoni kusubiria haki yako utaipata kwa kuchelewa lkn nawe utapata hasara mfano ukikaa siku 10 utapoteza hesabu ya milioni moja kwa siku kumi,hivo radhi kutoa hata laki 2 ili gari isilale kituoni thus wanapenda daladala sababu ya pesa ya haraka na ya uhakika.Wakifukuzwa kazi au wakistaafu utawaonea huruma sana maana hakuna mirija ya zuluma.
 
Hata uchukue gari zero kilometers wataitoa kasoro lzm iliwe.
 
Mi saa 12 asubuhi natoka home kurudi lazima iwe saa 1 usiku na zaidi,sitaki kabisa kukutana nao.
 
Camera hazipunguzi rushwa,nani atakaekaa mda wote anaangalia camera aache kuchat.Elimu itolewe zaidi nadhani wasikimbilie kulipisha fine bali kutoa onyo ukirudia kosa fine ndo ifuate.Pia fine haipunguzi ukiukaji wa sheria maana mwenye uwezo yeye kulipa si tatizo kama watu wanazinunua torch ili wawahi wanapokwenda nn fine.Fine hazijapunguza makosa ya barabarani labda kuongeza makusanyo,mamlaka zinahaja ya kubuni mbadala utakaowafanya watu waheshimu sheria za barabarani.
 
Hakuna anayependa kutoa rushwa ila shida inakuja pale Trafic anapokuambia anakuandia kosa fulani TZS 30,000 ambalo wewe kabisa unajua ni uongo ila kwa kuwa una haraka badala ya kupoteza muda kubishana naye unaamua kumpa TZS 5,000 akanywe nayo konyagi ifupishe hayo maisha yake.

Mfano hizo tochi zao kuna namna hata kama unatembea 45km/kwa saa yeye atakuonyesha ulikuwa unatembe 55Km/ saa ukipinga sana anakwambe akipe mzunguko wa matairi yako
 
Ukinunua gari lazima mkubali kugawana faida kati ya serikali na askari. Tena askari wanavuta nyingi kuliko mmiliki na serikali. Watu wa daladala ndo twajua.
 
Kwakweli traffic wamekuwa kero barabarani sana sana, kuna sehemu kabla ya kufika Mafinga kuna jamaa huwa anakaa kabisa na kamera yake kajificha angle ambayo haonekani kirahisi na kamera ina stand kabisa.

Sehemu ilivyokaa ni vugumu sana kwa dereva kwanza kuona kibao halafu in zebra haionekani vizuri na wala si sehemu yenye movement ya watu. Magari mengi pale yanapigwa kamera hata kama ulikuwa 51km/h utapigwa faini tena mbili, faini ya kwanza utaambiwa umevuka zebra bila kusimama, faini ya pili utaambiwa umevuka na speed say 55km/h.

Hao ni traffic wengine utakaowakuta mbele na picha zao kwenye simu, ukibishana anakuambia turudi akakuoneshe kibao kilipo! halafu utaambiwa umesamehewa kosa moja lingine unaandikiwa maana wewe ni mbishi sana, hapo mnaanza mjadala sasa wa kupunguziana mpaka anavuta mpunga wake unasepa zako,kuna siku tulishikwa magari zaidi 20, wabishi wanakomolewa kwa kulipa na waungwana wanajadili wanatoa mpunga wanasepa.

Kwa hiyo rushwa ya barabarani haiwezi kuisha sababu ya advantage ya traffic ya kukomoa madereva, naunga mkono labda faini baadhi ya makosa iwe pesa kidogo mfano elfu tano mpaka elfu kumi. Hatari yake lakini ni maderava wabaya na wakorofi wata take advantage kuendesha hovyo maana hawataogopa.

Kiujumla jambo hili lina utata kidogo na busara inahitajika kusolve kwakweli.
 
Watunza sheria wengine wamekuwa wakitumia udhaifu wa sheria kama fursa kwao kushiba.
 
Siungi mkono hoja.Yaani badala ya kumtoa trafiki na huku 5 nilipe faini ya elfu 30 au 50?
 
Njia peke ni kupunguza faini badala ya 30000 wekeni 5000 hapi watu watalipa uzuri. Lakini kwa 30 000 tabu sana kutatua tatizo
Kweli mkuu,tena mi hua sitaki shida akinipiga mkono tu wkt ananiambia lete leseni naiambatanisha na 'kishika uchumba' hapohapo kwny hio leseni,wala hutasikia maneno mengi,atajifanya anazungukia gari afu huyo anasepa zake.
 
Watu wengi ni waoga kubishana na traffic na hii ndio inasababisha rushwa. Kwa hili la app halitamaliza tatizo

Halafu ajali nyingi zinasababishwa na hawa hawa wanaosimamia sheria na barabara. Unakuta gari tairi zimeisha kabisa lakini anaruhusiwa kuendelea na safari baada ya kuwatoa buku. Bus linajaza mpaka watu wanashindwa kupumua na likipata ajali na kuuwa wanasema kosa la dereva wakati limepita sehemu na wao wameliona hilo, ila kwa njaa zao na kwa kuwa shangazi zao hawamo humo they don’t give a toss.

Sheria ziwe kali kwa hao wala rushwa na watoaji pia na adhabu iwe kali haswa.
 
Ila bongo bado fine za gari zina ka uafadhali kiaina,niliona majuzi state attorney wa Rwanda ali-overspeed fine yake akapigwa Rwf 150,000 kama 450,000(laki nne na nusu) za kibongo,nikasema hiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Ila bongo bado fine za gari zina ka uafadhali kiaina,niliona majuzi state attorney wa Rwanda ali-overspeed fine yake akapigwa Rwf 150,000 kama 450,000(laki nne na nusu) za kibongo,nikasema hiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Mkuu fines za makosa ni ndogo sana huko ukifananisha na nchi zingine
Ila tatizo kubwa ni rushwa ambayo watu wameifanya kama way of life
Kama sheria zinafuatwa sawa
Na fine za Tz ni ndogo bado
Jamaa yangu hapa [emoji636] alikamatwa na kosa la drink and drive kafungiwa miezi 14 kuendesha gari na fine ya £9000 kama kama 27m hivi

Hawana utani huku ukivunja sheria utakoma
 
Hiiiiiii £9000 aisee hizo zina wenyewe bongo fine kama hio itabidi wakate kwenye mafao tu,hakuna namna tena.,ila DUI kwa wenzetu naona ni kosa heavy sana mkuu.

Nadhani bado utashi wa kutokomeza rushwa huko mabarabarani bado haujawekewa mkazo,pamoja na boss wa Takukuru kuwekwa mjeda lkn tatizo hili limeshakua sugu.


 

[emoji23][emoji23]
Yaani fine zinapanda tu hazishuki huku na unaweza usisimamishwe na police hata miaka 10 kama huvunji sheria
Na licence zina point 12 na kila kosa wanafyeka baadhi inategemea na kosa lenyewe
Camera zipo kila barabara na magari yote yapo kwenye system ya serikali hata kama huna insurance unadakwa kirahisi sana
Suala bado ni gumu sana huko kwetu mkuu
Police kusimama barabarani umewawekea mlo tu hakuna kingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…