LESIRIAMU
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 9,006
- 14,536
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kuwe na mapitio ya maeneo ya mwendo mdogo (50km/hr). Kuna baadhi ya vipande vya Barabara hamna haja ya hiyo speed limit. Na kuna maeneo mengi mno ya speed limit ya 50km/hr ambapo inakuwa kama kero kwa watumia barabaraCamera hazipunguzi rushwa,nani atakaekaa mda wote anaangalia camera aache kuchat.Elimu itolewe zaidi nadhani wasikimbilie kulipisha fine bali kutoa onyo ukirudia kosa fine ndo ifuate.Pia fine haipunguzi ukiukaji wa sheria maana mwenye uwezo yeye kulipa si tatizo kama watu wanazinunua torch ili wawahi wanapokwenda nn fine.Fine hazijapunguza makosa ya barabarani labda kuongeza makusanyo,mamlaka zinahaja ya kubuni mbadala utakaowafanya watu waheshimu sheria za barabarani.
Ni mbunge gani wa Ccm atakae toa wazo zuri kama lako?? Wao wana fikiri kutoza faini kubwa ni kupunguza makosa barabarani.. Hawaoni kama ni kutengeneza ulaji kwa wanao simamia hizo sheria..Kwa kweli Dar imezidi. Nilikwenda Dar na gari askari akatusimamisha akaangali kama inadaiwa faini akakuta hakuna akangalia matairi safi, kila kitu kiko safi lakini jibu alilotujibu alisema haiwezekani hii gari itembee bila fani. Gari bovu nikamuuliza ubovu wake ni nini niambie nikarekebishe. Yeye anangangania leseni nikampa cha ajabu aliniandikia faini bila kunielekeza cha kurekebisha. Niliumia roho sana.
Ombi langu kama wanataka rushwa iishe basi wawewanawaelewesha wamiliki wa magari makosa ya magari yao ikiwezekana upande wa faini ya pesa ifutwe iandikwe onyo na kitu kibovu ili irekebishwe.
La pili kama ni kosa la dereva liandikwe kwenye leseni yake isiingie kwenye gari. Kama ni kosa la kondakta na yeye aandikiwe kwenye upande wake. Kama ni kosa la gari liandikiwe naaelezo yawepo kwamba linakosa gani ili mmiliki aelewe.
Wamiliki wa magari wanapata shida ya kulipa mafaini ambayo sio kosa la gari.
Asanteni
Nilisikia wakishapewa hawakai nazo mfukoni ila wanakimbilia kuweka M Pesa.Kuna mambo yanfanyika unashangaa,juz jtano nilikuwa natoka tanesco substation ya makumbusho karibu na usalama wa taifa ,nikaingiza gari kwa njia mbili kufika makumbusho trafiki akanisimamisha akaomba leseni nikamuuliza kosa langu akasema nimetanua kule juu nikamwambia natoka tanesco ,hakuelewa nikamwambia lesen sikup sbb Sina kosa akaendelea kusimamisha magar Zaid ya 7 kila gar akaanza kufinyiwa aisee ilikuwa aibu jaman ,mim niliyegoma nilikaa nusu saa nzima,baadae nikaona upuuzi nikaondoka zangu nikasbria anikimbize na pikipiki hakutokea,ila hapo kashanichelewesha sana.ushaur wangu kwa IGP hawa polisi wana uonevu mkubwa sana barabaran ,Kuna chuki kubwa kati ya trafik na wenye magar,jaribu trafiki wakimaliza kuongoza magari wawe kituo kimoja kwa ajili ya ukaguzi,iyo sehem ifungwe kamera,takukuru tafuteni waendesha daladala,kirkuu,fuso wanajua mengi sana na mtapunguza rushwa kwa kiwango kikubwa
Aibu kubwa sana,wakubwa hawajaamua kuvalia njuga ili sualaNilisikia wakishapewa hawakai nazo mfukoni ila wanakimbilia kuweka M Pesa.
Ninaona watafute adhabu nyingine. Hawajui hicho chombo kinahitaji matengenezo. Wanajali mifuko yao.
Unashangaa jero? Mie traffic kesha chukua maembe ya kula baada ya kukomaa na akaona hapati hata mia na ndani ya gari (nikiwa natokea Tabora) kuna embe zilizo iva nimenunua niliishia kucheka tuu.Dah Kuna askari mmja tigo aka Rambo
Sjui kama karudishwa kazini maana alisimamishwa uzuri wake analamba mpk jero haachi hela
Ova
Well said CONTROLA, huo ndioukweli kwani hii si mara ya kwanza kwa hizi opersheni. Tumeziona nyingi lakini hazina any impact kwenye maisha ya watumia barabara, iwe madereva au abiria. Waache kutupotezea muda.Sijaelewa TAKUKURU watakuwa makonda kwa muda au wata play part ya abiria na dereva
Hapa sidhani kabisa kama kuna utatuzi.
Mgeni akija nyumbani hata ukifanya kosa Huchapwi,subiri aage unaweza ukatamani muondoke wote.
Hawa takukuru wanataka kutupalia makaa halafu wasepe watuache barabarani tunapambana na matrafki
Ingekua zoezi hili endelevu na uhakika hpo sawa ila kwa TZ yetu hii kila jambo linaanzishwa kwa nguvu
Ila mwisho haujulikani...Sijui
Daladala za Iringa kero sana zile Zinazoenda ipogolo, stend, pamoja na zile za kalenga tosamaganga.Iringa rushwa imetamalaki,gari zinaanza kisimamisha kuanzia stend na polis hawajali bora basi hata wawe watano lkn utakuta gari imejaza mpaka mnabanana hasa daladala za iringa mjin polis wanazagaa tu,juzi nimeenda kwa majukum yangu kunastend mpya saiz n balaaa,gari imejaa lkn haiondoki stend mpaka ijaze wa kusimamisha na polis wanaangalia tu mpaka nilishangaa
Ni kweli askari wa barabarani ni kero mkuu.Yaani hawapo barabarani kwa nia ya kudhibiti ajali,lakini wapo kwa ajili ya kukusanya fedha.Ndio maana kila uchao wanabuni mbinu mpya za kuchukua rushwa.Kwa jinsi hali ilivyo,haiwezekani kabisa kumaliza rushwa barabarani.Tuta acha je kutoa Rushwa? Rushwa tunatoa kwa sababu ya utatu huo huo.
Mosi, Serikali (faini 30,000), dereva hana uwezo wa kutoa faini ya 30,000 na askari yuko tayari kupokea rushwa ya 5,000-10,000. Binafsi nitatoa rushwa kuliko kulipa faini ambayo kiuhalisia hiyo fedha sina. Wakifanya faini 10,000 nitailipa.
Pili, ili tuache kutoa rushwa, ni lazima serikali ipambane kuhakikisha kuwa polisi wanaacha kubambika makosa kwa waendesha vyombo vya barabarani. Trafiki anaanza, leseni (hiyo), triangle (hiyo), sticker ya usalama (hiyo), breki (zipo), siti (haina mchubuko), kwanini umepakia mzigo umepita urefu wa bodi? Unatakiwa ulipe faini (30,000).
Au tairi zinaelekea kuisha (faini), gari rangi imebabuka (faini), kioo kimegongwa na changarawe na kuonyesha kanyota bila kupasuka (faini), pale nyuma uliovertake pasiporuhusiwa (wakati gari uliovertake ilipaki pembeni).
Hii inakuwa karaha sana kwa kuwa huwezi kuwa mtakatifu kwa haya watakayo askari wetu wenye njaa kali. Mwisho wa siku ni kuishia kutoa rishwa ili japo ubakize hela ya sembe kwa ajili ya watoto. Ningekuwa naweze nisingepita barabarani kabisa kuepukana na polisi hawa wenye kero za kutosha.
Kuna wale madada wawili askari trafic njia ya Dodoma-Dar yaani porini pale hawaogopi wamesimama wawili tu....ni eneo kabla hujaikuta njia panda ya kwenda kiteto,au kuna siku niliwakuta katika eneo la ranchi ya kongwa wakanisimamisha wakakagua leseni kama nina deni nikafikiria upande mwingine ni hatari sana kwa usalama waoKukomesha Traffic wawe wanakaa sehemu zenye CCTV camera ndipo wasimamishe magari na kukagua.Hili la kusimama popote linachangia Sana Rushwa.
Pia ziwekwe kamera automatic fixed sehemu.za spidi limit Askari traffic waondolewe wakafanye Kazi zingine badala ya hiyo ya kuvizia na kamera zao.
Maeneo ya mataa na zebra zifungwe kamera za CCTV traffic police waondolewe