Taarifa kutoka ndani ya TAKUKURU zinadai kuwa taasisi hiyo imefungua jalada la uchunguzi wa tuhuma kuwa Waziri wa Nishati, January Makamba, alitoa rushwa kwa wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara yake ya 2023/24 wiki iliyopita.
Inadaiwa Makamba alitumia taasisi zilizo chini ya Wizara yake ikiwemo TANESCO, EWURA na TPDC kugawa rushwa kwa wabunge kwa kisingizio cha kufanya semina ya wabunge siku mbili mfululizo kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake.
Pia aligawa mitungi 100 ya gesi kwa kila mbunge kama sehemu ya rushwa hiyo, iliyofanikisha bajeti yake kupitishwa licha ya malalamiko makubwa ya wabunge kuhusu huduma mbovu za kukatikatika kwa umeme na usimamizi hafifu wa sekta ya nishati.
Tayari baadhi ya wabunge wameanza kuhojiwa na TAKUKURU ili kukusanya ushahidi wa rushwa hiyo ya mchana ambayo inakadiriwa kutumia karibu Shilingi Bilioni 2.
Idara ya Usalama wa Taifa, TISS, nayo inasemekena kuwa inachunguza taarifa hizo ili iweze kupeleka faili kwa mamlaka ya uteuzi.