Tetesi: TAKUKURU, TISS wadaiwa kuchunguza rushwa ya Wizara ya Nishati kwa Wabunge

Hao TAKUKURU wanatafuta njia ya kumsafisha mchafu, tusichezeane akili, kwanza uchunguzi wao unatia shaka, wote wameteuliwa na mtu mmoja, siamini kama watoto wa nyumba moja wanaweza kuchunguzana.

Hili suala la mitungi ya gas kugaiwa bungeni limetamkwa hadharani na mbunge mwenzao na Spika Tulia pia akalizungumzia, mpaka hapo sioni sababu ya uchunguzi tena, kwanini igaiwe wakati huu akitaka wabunge waipitishe bajeti ya Wizara ya Nishati?

Hawa wanachotaka kufanya ni kuja na majibu ya kisanii, kusema hapakuwepo na tatizo lolote, kama vile wale walioongea walikuwa hawajui wasemalo. Makamba ni corrupt na aligawa hiyo mitungi ya gas kuwahonga wabunge waipitishe bajeti ya Wizara ya Nishati, huu ndio ukweli wangu, sidanganyiki.
 
Taarifa kutoka ndani ya TAKUKURU zinadai kuwa taasisi hiyo imefungua jalada la uchunguzi wa tuhuma kuwa Waziri wa Nishati, January Makamba, alitoa rushwa kwa wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara yake ya 2023/24 wiki iliyopita.

Inadaiwa Makamba alitumia taasisi zilizo chini ya Wizara yake ikiwemo TANESCO, EWURA na TPDC kugawa rushwa kwa wabunge kwa kisingizio cha kufanya semina ya wabunge siku mbili mfululizo kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake.

Pia aligawa mitungi 100 ya gesi kwa kila mbunge kama sehemu ya rushwa hiyo, iliyofanikisha bajeti yake kupitishwa licha ya malalamiko makubwa ya wabunge kuhusu huduma mbovu za kukatikatika kwa umeme na usimamizi hafifu wa sekta ya nishati.

Tayari baadhi ya wabunge wameanza kuhojiwa na TAKUKURU ili kukusanya ushahidi wa rushwa hiyo ya mchana ambayo inakadiriwa kutumia karibu Shilingi Bilioni 2.

Idara ya Usalama wa Taifa, TISS, nayo inasemekena kuwa inachunguza taarifa hizo ili iweze kupeleka faili kwa mamlaka ya uteuzi.
Meno ya umbwa hayaumani
 
Huyu jamaa ni hatari mno kwa Rushwa. Na wao watahongwa tu
 
Huyo yupo kwenye list ya wasiogusika awamu ya 6 hivyo hao Takuukuru na Teeth hawawezi ingia kina hiko maji siyo size Yao. Dereva wa wizara ya Nishati kajua kujizolea maadui uenda akamzidi Bashite.
 
Kama ingekua ni kwa nchi ambazo viongozi wake wanajua wajibu wao na kuwajibika huyu angekua tayali amejiuzulu kupisha uchunguzi na kama ikibainika sio kweli ana safishwa jina lake, lakini huku uswahilini kanyaga twende hata ikigundulika ni kweli sidhani na nitakua mtu wa mwisho kuamini kwamba atachukuliwa hatua zozote za kinidham na kisheria.
 
Huyo yupo kwenye list ya wasiogusika awamu ya 6 hivyo hao Takuukuru na Teeth hawawezi ingia kina hiko maji siyo size Yao. Dereva wa wizara ya Nishati kajua kujizolea maadui uenda akamzidi Bashite.
Sawa tu Makonda na Sabaya wakati wa awamu ya tano.
 
kagawa mitungi ya gesi kwa wabunge , siku chache kabla ya kuwasilisha bajeti yake. Hii haijakaa sawa , Kuna kitu hapa so bule. kwann hakutoa hiyo mitungi mwaka Jana , au mwezi January !? wananchi wanajinunulia kwa jasho lao , Leo wabunge wenye posho , wanapewa bule kabisaaa. Sasa hii kula kwa urefu imezidi Sasa.
 
Vita inaendelea. Ni walewale jamaa zetu wa legacy. Piga kazi January
Fikra kama hizi za kwako ndiyo chanzo cha nchi huu kuwa duni.

Jadili hoja. Mambo ya legacy yanatoka wapi? Wewe sema kama unaona ni halali mbunge kuhongwa mitungi 100 ya gas = 70,000 x 100 = TZS 7m. Je, ni halali mbunge tayari yupo kwenye vikao vya bunge, kuhudhuria semina ya kumwongezea uelewa eti ni lazima alipwe posho.

Sisi wengine toka mwanzo tuliiona ile kuwa ni rushwa ya wazi kabisa.
 
Mimi ningewaona hawa Wanaochunguza wana Akili kama wangeanza Kwanza kumchunguza anayetoa Pesa hovyo kwa Klabu ya Yanga SC, anatoa Ndege kufanya Majukumu ya Kipuuzi yasiyo ya Faida huku Fedha za walipa Kodi Masikini zikitumika kuzilinda.
Ulivyoandika utadhani huwa unapanda hizo ndege na kuchangia pato linalopatikana.
 
Tuone kama kweli wako serious!

Kugawa Mitungi 100 kwa kila mbunge, katika nchi hii masikini kwa kweli ni aibu kwa aliyefanya kitendo hicho na ni aibu kubwa kwa aliyemteua!.

Kama anauwezo wa kugawa mitungi 100 ya gesi bure kwa Wabunge, Je yeye kajipa mitungi mingapi?

Rushwa kwenye utawala wa Samia siku hizi haina aibu!
 
Mbona baada tu yakugawa mitungu hiyo, siku mbili zilizo fuatia prime minister alimsifia na kumtaka achape kazi na asisikilize maneno ya majungu...🤨
 
Taarifa kutoka ndani ya TAKUKURU zinadai kuwa taasisi hiyo imefungua jalada la uchunguzi wa tuhuma kuwa Waziri wa Nishati, January Makamba, alitoa rushwa kwa wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara yake ya 2023/24 wiki iliyopita.

Inadaiwa Makamba alitumia taasisi zilizo chini ya Wizara yake ikiwemo TANESCO, EWURA na TPDC kugawa rushwa kwa wabunge kwa kisingizio cha kufanya semina ya wabunge siku mbili mfululizo kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake.

Pia aligawa mitungi 100 ya gesi kwa kila mbunge kama sehemu ya rushwa hiyo, iliyofanikisha bajeti yake kupitishwa licha ya malalamiko makubwa ya wabunge kuhusu huduma mbovu za kukatikatika kwa umeme na usimamizi hafifu wa sekta ya nishati.

Tayari baadhi ya wabunge wameanza kuhojiwa na TAKUKURU ili kukusanya ushahidi wa rushwa hiyo ya mchana ambayo inakadiriwa kutumia karibu Shilingi Bilioni 2.

Idara ya Usalama wa Taifa, TISS, nayo inasemekena kuwa inachunguza taarifa hizo ili iweze kupeleka faili kwa mamlaka ya uteuzi.
HAKUNA JIPYA CAG KATAJA WALIOPIGA FEDHA ZA UMMA MPAKA LEO KIMYA KAMA VILE REPORT YA CAG ILIKUWA FAKE
 
Mimi ningewaona hawa Wanaochunguza wana Akili kama wangeanza Kwanza kumchunguza anayetoa Pesa hovyo kwa Klabu ya Yanga SC, anatoa Ndege kufanya Majukumu ya Kipuuzi yasiyo ya Faida huku Fedha za walipa Kodi Masikini zikitumika kuzilinda.
Kweli afya ya akili ni tatizo sana
 
Back
Top Bottom