Uchaguzi 2020 TAKUKURU: Ubwabwa wa Hashim Rungwe kwenye kampeni ni Rushwa

Kuufurahisha mwili ili mtu apate kura ni sawasawa na rushwa ya ngono tu.
 
Takukuru wanazuia watu wasile ubwabwa ila anayehonga bodaboda yuko sawa hawajatoa tamko lolote afadhali akae kimya
 
TAKUKURU yenyewe ni BWABWA tu. Rushwa CCM ilitembea hadharani wakati wa mchujo wa wagombea lakini ikashindwa kuishughulikia. Ikabaki kusema "CCM itajishughulikia yenyewe" !!! Pambaf. Kama sio double standards ni nini? TAKUKURU+CCM = BWABWA MCHUZI (RUNGWE B).
 
Takukuru hawana akili Mimi nilishajiandaa kwenda kula wali kuku Sasa kupiga marufuku not fair kabisa wamenibore mxiiiiew zao
 
Wakati mwingine huwa najiuliza hivi aliyeturoga waafrika alizikwa wapi tukatambike kwenye kaburi lake pengine itasaidia kutuondolea upumbavu wetu wa kutojitambua. Hapa sitaki kabisa kuzungumzia kauli ya Afande Siro jana kama vile hatambui nini vyanzo vya uvunjifu wa amani katika chaguzi zetu...
 
Takukuru acheni double standards. Mbona hamkemei anayetangaza ajira kipindi Cha Kampeni? Tuacheni tule wali, msituingilie kwenye Mambo yetu ya Msingi.
 
Wanaona aibu nchi ya kipato cha kati wananchi wake wanakusanywa kwenye kampeni kwa wali nyama, Waache Wananchi wafaidi Maana ikipita ndio mpaka 2025
 
Vipi na ile ahadi ya ajira za walimu wiki ijayo? Tukumbushane kidogo nani kaitoa kwa lengo gani? Kama Rungwe lengo lake ni kuwa watu washibe na wasikilize vizuri, hizi ajira nazo? Kama Rungwe asitoe ubwabwa kipindi hiki cha uchaguzi kwa nini hawa wa kijani wasilazimishwe kutoa hizo ajira mwakani sio kipindi hiki cha uchaguzi ambapo kwa sasa ni rushwa?
 
Kweli nimeamini, kwenye vita usipuuze adui yako yeyote. Hivi kweli Hashimu Rungwe na ubwabwa wake ni tishio la kumshinda mtu yeyote kwenye kinyang'anyiro cha urais?
 
sera lazima iendane na vitendo , hakuna cha rushwa hapa , MH RUNGWE kamatia hapo hapo
 
Mpaka mzee Rungwe wanamwonea wivu duh kweli Tz tunasafari ndefu bado
 
Na milioni 50 kila kijiji haikuwa rushwa?
Uongo si sawa na rushwa?
 
Hivi takukule Wana legitimacy ya kuongelea rushwa kweli. Maana na kumbuka waliwaachia wa kijani mambo ya rushwa wao wakaa kando
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…