DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Dah, inasikitisha,hapa kutakuwa na pesa imetembea tu
Hilo si la kuuliza hao jamaa ni walafi waliopindukia,miaka ya tisini waliuza nyumba ya Wakfu walidai imeuzwa kwa milion 20 lakini cha ajabu aliyeinunua alikwenda kuchukulia mkopo benki wa tshs milioni 200 na nyumba ikiwekwa kama dhamana tena bila hata kuifanyia ukarabati wowote tuhuma hizo zilitolewa na Sheikh Yahya Hussein basi walimshikia bango kupitia mfadhili wao hadi wakaifutia usajili taasisi yake ya Baraza kuu la kuendeleza koran Tanzania (Balukta) na yeye akapigwa mkwara basi kuanzia hapo akaanza kuwa chawa wa Serikali hadi umauti ulipomfikia
Pia miaka ya katikati hapo walimuuzia Manji eneo la Chang'ombe kwa milioni 80 na baadaye Manji aliliuza hilo eneo kwa bilioni na kitu,hii maana yake kuna fedha nyingine wamekula.
Nina uhakika hata ule msikiti uliojengwa pale makao makuu yao wangepewa pesa taslimu wajenge wenyewe ungeishia ghorofa moja tu.
 
Mbona hiyo barua inaonyesha kibali kilisitishwa cha ujenzi wa MADUKA na MSIKITI baada ya kuvunja msikiti wa zamani, issue hapo ni nini hasa mkuu...kiwanja kimeuzwa? au amepewa mwekezaji bila kushirikisha wenye msikiti maana bango la ujenzi linaonyesha CLIENT ni Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre which means kiwanja bado ni mali ya Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre
 
Poleni sana,umoja wenu dhidi ya wala rushwa ndiyo utawapa ushindi.Lakini mliyobaki ktk mapambann ya kudai haki wenzenu wakimezwa na rushwa kwisha.
 
Mwenge Mosque & Islamic centre chini ya Baraza la wadhamini feki(mamluki)!
 
Naona umeamua kosoma barua moja. Hapo kuna barua mbili. Soma tarehe ya kusitisha lini na tarehe ya kuhuwisha lini. Baada ya mzee aliyekuwa anasimamia Msikiti kufariki kwa kifo kisichojuliakana, ndipo wakahuwisha. Soma tena urudi kunielewesha wapi hujaelewa. Hiyo Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre imeandikwa tu ila sio wao. Ni Magumashi ili ionekane wanahusika. Wasingelalamika
 
Milki ya kiwanja bado ni ile ile, kwa mujibu wa bango la ujenzi.
Sasa sijui huyo aliyeuziwa alinunuaje, na anajengaje bila kubadilisha umiliki wa kiwanja,
Tungepata maelezo ya upande wa pili wa huu mgogoro, tungejadili kwa haki,
 
Duh,ukiwasikiliza wanavyoongea utadhani kweli Wana hofu ya Mungu ya dhati,kumbe matapeli wakubwa!
 
Nimesoma kote ila hiyo barua moja unayosema ndo nimeamua kuisoma ni kwamba nimei-link na hilo bango tu, kwa kuwa kwenye issue za ujenzi bango nalo ni sehemu ya ujenzi kwa kuwa linamtambulisha mmilki wa kiwanja na ujenzi unaoendelea ikiwa pamoja na vibali mbalimbali. Na sio kwamba sijasoma ila nimeangalia viashiria vingine vinavyoonyesha umilki baada ya kusoma "Je, Tajiri aliwezaje kununua sehemu na kujenga bila ya kuwa na hati?", ndo nikawa najiuliza issue hapo ni jamaa amekodisha au amenunua (maana umilki ulioandikwa kwenye bango umebaki kwa taasisi)

Ila kwa kuwa umesema "Hiyo Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre imeandikwa tu ila sio wao. Ni Magumashi ili ionekane wanahusika. Wasingelalamika" acha niishie hapa kwa kutokuwa na nia ya kuendelea kutaka kufahamu zaidi.
 
Pambaneni mpaka kieleweke! Uzuri nyie vita mnaiweza! Si mna ile kaulimbiu kwamba “hakuna kumuachia mungu ni jino kwa jino?!”...haya komaeni sasa
Kwani bongo suicide vest hazipo?

Anyway wakiarike kile kikosi cha talibani kiwasaide kazi.

Anyway pole zao hii haikubariki..hope samia kawasikia.


#MaendeleoHayanaChama
 
AAh, sheria itafata mkondo wako, si jambo la kustusha sana, Bakwata mbona wameuza viwanja vya wakf kwa Manji siku nyingi sana.

Silioni tatizo, Waislam kama wana hasira wajenge mwengine mzuri zaidi na mkubwa kuliko uliovunjwa.
Magufuli alivirudisha kwa wenyewe.
 
Poleni! Haya yanatokea Kwa kuwa huyo mama yenu ni rushwa tupu!
 
Hana hadhi ya kuitwa shehe huyo bali tapeli tu
Huyo ana majibu mengi siku ya hukumu kama anaamini
Ila wanamuogopa kwa kutishia ushirikina
Unajua waswahili wanavyoamini mambo hayo
Kijana kuwa makini nakufuatilia sana unapenda sana kunidhalilisha sana
 
Kwani Sheikh Ponda Issa Ponda ANASEMAJE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…